Tafuta

2023.03.13 Uwakilishi wa Kitabu cha Padre Spadaro kwa uwepo wa Kardinali Parolin na Waziri Mkuu wa Italia Bi Meloni. 2023.03.13 Uwakilishi wa Kitabu cha Padre Spadaro kwa uwepo wa Kardinali Parolin na Waziri Mkuu wa Italia Bi Meloni. 

Kard.Parolin:ni kufanya majaribio ya ubunifu ili kuibua mazungumzo ya amani

Katibu wa Vatican akizungumza na waandishi wa habari pembezoni mwa uwasilishaji wa kitabu cha Padre Spadaro alisema:“Tunajaribu kutumia ubunifu wetu wote kuamsha upya mazungumzo ya amani."Kwa upande wa suala la uhamiaji:tunapaswa kuendelea na sera ya kukaribisha.Kuhusu makubaliano na China:Pande zote mbili zinataka kuendelea.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kwa mujibu wa Kardinali Pietro Parolin  Katibu wa Vatican amekumbusha kuwa Vatican ina maono tofauti ikilinganishwa na mataifa binafsi, kwa sababu ina maono ya ulimwengu na mtazamo tofauti wa kutafuta amani. Amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari pembezoni mwa uwasilishaji wa kitabu cha Padre Spadaro katika ukumbi wa La Civiltà Cattolica. Kwa mujibu wa Kardinali Parolin akizungumza kuhusu migogoro ya Ulaya alisema: “Papa Francisko anataka kwenda Moscow na Kyiv, kwa sababu anaamini kwamba huduma ya amani inawezekana tu kufanywa ikiwa atafaulu kukutana na marais hao wawili, Vladimir Putin na Volodymyr Zelensky, alisisitiza  Katibu wa Vatican. Na akitafakari kuhusu   miaka kumi ya Upapa wa Fransisko unaoadhimishwa tarehe 13 Machi, aliufafanua  kuwa wa nguvu sana kwamba, amelipatia Kanisa fursa ya kusikilizwa ulimwenguni”.

Kuhusu suala la uhamiaji, pia lilikuwa ni mada ya mkutano wa nchi mbili kati ya Parolin na Waziri Mkuu wa Italia Bi Giorgia Meloni kando ya uwasilishaji wa kitabu, kulingana na Kardinali, ambaye alisema maelekezo ya Papa yanapaswa kutafsiriwa katika sera za serikali. Hii ilisisitizwa jinsi sera mara nyingi huzuia na kupungua, wakati inahitajika kuendelea na sera iliyo wazi zaidi na ya kukaribisha. Katibu wa Vatican akijibu swali lingine, alikumbuka umuhimu wa makubaliano yaliyofikiwa wakati huu wa Papa kati ya Vatican na China. Kardinali Parolin alionesha uwepo wa mtazamo wa matumaini na mazungumzo ambayo pande zote mbili zinataka kuendelea. Kwa kifupi alisema: “Tunaomba tu kwamba Wakatoliki wanaweza kuwa Wakatoliki wenye uhusiano na kanisa la ulimwenguni wote”.

Akizungumzia ziara iliyopangwa kufanyika mwishoni mwa  mwezi Aprili huko Beijing na Askofu wa Hong Kong, Monsinyo Stephen Chow, kwanza baada ya miaka mingi, Kardinali Parolin alifafanua kuwa ni kufikiwa kwa mwelekeo huo wa kawaida wa kanisa huko Hong Kong ambao unapaswa kuwa daraja kati ya China na Kanisa zima na kwa hiyo ishara chanya ambayo amefurahishwa sana. Zaidi ya hayo, kulingana na Kadinali huyo, Ziara ya Papa Francisko ya  kwenda Mongolia inawezekana, hata kama uamuzi wa uhakika ambao bado haujafanywa. Hatimaye kuhusu kura ya maaskofu wa Ujerumani, mwishoni mwa mchakato wa sinodi, kuidhinisha baraka kwa  watu wenye jinsia moja.  Kardinali  Parolin amebainisha kuwa Vatican ilikuwa tayari imejieleza wazi juu ya suala hilo, akibainisha kwamba mazungumzo yataendelea ndani ya mchakato wa safari ya sinodi ya Kanisa la ulimwengu. Kanisa mahalia haliwezi kufanya uamuzi kama huo unaohusisha nidhamu ya Kanisa la ulimwengu wote”, alihitimisha.

14 March 2023, 16:30