Tafuta

Picha ni wakati wa Ziara ya kitume ya Papa Francisko nchini Canada na mkutano na watu Asilia mnamo Julai 2022. Picha ni wakati wa Ziara ya kitume ya Papa Francisko nchini Canada na mkutano na watu Asilia mnamo Julai 2022.  (Vatican Media)

Kanisa linatetea watu Asilia&Fundisho la Ugunduzi ambalo sio ya Kikatoliki

Katika Ujumbe wa Pamoja wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu na la Maendeleo Fungamani ya Binadamu:Wakristo wengi wamefanya vitendo viovu dhidi ya watu wa kiasilia.Maandishi ya Kipapa ya karne ya XV ambayo waliwapatia watawala wa kikoloni mali ya watu wa asilia ni hati za kisiasa,zilizotumiwa kwa matendo maovu.

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

Katika Andiko la Pamoja lililopewa jina “Fundisho la Ugunduzi” la Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu pamoja na Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Huduma Fungamani ya Binadamu lililochapishwa Alhamisi tarehe 30 Machi 2023 linabainisha kwamba “Shukrani kwa msaada wa watu wa kiasilia Kanisa limepata mwamko mkubwa zaidi wa mateso yao, ya zamani na ya sasa, kutokana na kunyang’anywa ardhi zao ... wakati, ulikuwa unalenga kuondoa tamaduni zao kwani tayari mnamo 1537 Papa Paulo III alitangaza kwa dhati kwamba wenyeji hawapaswi kufanywa watumwa au kuibiwa mali zao”. Katika hati hiyo inasema kwamba “Fundisho  la Ugunduzi”, nadharia ambayo ilisaidia kuhalalisha kunyang'anywa kwa watu wa asilia  na watawala wakoloni, sio sehemu ya mafundisho ya Kanisa Katoliki na kwamba hati za kipapa ambazo zilikuwa zikikubaliwa wakati wa utawala wa kikoloni hazikuwahi kuwa za Majisterio.

Hii ni  hati muhimu ambayo,  kwa miezi minane baada ya ziara ya kitume ya Papa Francisko nchini Canada, inathibitisha wazi kukataa kwa Kanisa Katoliki mawazo ya ukoloni. Katika historia, inakumbukwa, Mapapa ambao wamekemea vitendo vya unyanyasaji, ukandamizaji, dhuluma ya kijamii na utumwa, ikiwa ni pamoja na wale wanaliofanyiwa watu wa kiasilia. Nakulikuwa pia na mifano mingi ya maaskofu, mapadre, watawa na walei ambao walitoa maisha yao kutetea hadhi ya watu hao. Lakini inakumbusha pia kwamba  haikosi kutaja kuwa Wakristo wengi wamefanya matendo maovu dhidi ya watu wa kiasilia ambao Mapapa wa hivi karibuni wameomba msamaha kwa matukio mengi.

Kuhusiana na “Fundisho la Ugunduzi”, wanathibitisha kuwa dhana ya kisheria ya 'ugunduzi' ilijadiliwa na nguvu za kikoloni kuanzia karne ya 16 na kupatikana kwa maelezo maalum katika mahakama ya karne ya 19 ya mahakama za nchi mbalimbali, kulingana na ambayo ugunduzi wa ardhi na walowezi ulitoa haki ya kipekee ya kuzima, kwa ununuzi au unyakuzi, hatimiliki au umiliki wa ardhi hizo na watu wa kiasilia. Kulingana na baadhi ya wasomi, ‘Fundisho’ hili lilipata msingi wake katika hati mbalimbali za kipapa, hasa Hati ya  Nicholas V ‘Dum Diversas’ (1452) na ‘Romanus Pontifex’ (1455), na ile ya Alexander VI ‘Inter Caetera’ ( 1493). Haya ni matendo ambayo Mapapa hawa wawili waliwaidhinisha watawala wa Ureno na Wahispania kumiliki mali katika nchi zilizotawaliwa na wakoloni kwa kuwatiisha watu asilia.

Kwa hiyo maelezo yanabainisha kuwa “Utafiti wa kihistoria unaonesha wazi, kwamba hati za Kipapa zinazohusika, zilizoandikwa katika kipindi maalum cha kihistoria na kuhusishwa na masuala ya kisiasa, ambazpo hazijawahi kuchukuliwa kuwa maneno ya imani ya Kikatoliki.” Wakati huo huo, Kanisa linatambua kwamba Hati hizi za kipapa hazikuonesha ipasavyo hadhi na haki sawa za watu wa kiasilia”. Na wanaongeza kuwa “yaliyomo katika hati hizo yalitumiwa kwa madhumuni ya kisiasa na mamlaka ya kikoloni kwa kushindana kati yao, ili kuhalalisha vitendo viovu dhidi ya watu wa kiasilia, wakati mwingine vilifanywa bila upinzani wa mamlaka ya kikanisa”. Kwa hiyo Mabaraza haya mawili ya Kipapa yanaandika kwamba ni sawa, kutambua makosa haya, kwa kutambua madhara ya kutisha ya sera za uigaji na uchungu waliouhisi watu wa kiasili, na kuomba msamaha.”

Hata hivyp pia maneno ya Papa Francisko yananukuliwakuwa: “Kamwe Jumuiya ya Kikristo haitaweza tena kujiruhusu kuambukizwa na wazo kwamba tamaduni moja ni bora kuliko nyingine, au kwamba ni halali kutumia njia za kulazimisha wengine”. Na wanakumbusha kwamba “bila shaka, mahakama ya Kanisa inaunga mkono heshima inayostahili kila mwanadamu na Kanisa kwa hiyo inakataa dhana hizo ambazo hazitambui haki za asili za watu wa kiasilia ikiwa ni pamoja na kile kinachojulikana kama “fundisho la ugunduzi”.

Hatimaye katika ujumbe huo nataja matamko nyingi na yaliyorudiwa ya Kanisa na Mapapa kupendelea haki za watu wa kiasilia, kuanzia na ile iliyomo kwenye Hati ya “Sublimis Deus ya Paulo III (1537), ambaye alitangaza kwa dhati kwamba watu asilia  hawakupaswa kwa njia yoyote kunyimwa uhuru wao au milki ya mali zao, hata kama wao si wa imani ya Kikristo; na kwamba wanaweza na lazima, kwa uhuru na uhalali, kufurahia uhuru wao na milki ya mali zao; wala hawapaswi kufanywa watumwa kwa njia yoyote ile; ikiwa kinyume chake kitatokea, kitakuwa batili na hakitakuwa na athari yoyote.” Hivi karibuni mshikamano wa Kanisa na watu wa kiasili umesababisha Vatican kuunga mkono kwa dhati kanuni zilizomo katika Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Watu wa Kiasilia”. Utekelezaji wao ungeboresha hali ya maisha na kusaidia kulinda haki za watu hawa.

30 March 2023, 17:17