Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 25 Machi 2023 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mheshimiwa Régis Kévin Bakyono, Balozi mpya wa Burkina Faso mjini Vatican. Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 25 Machi 2023 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mheshimiwa Régis Kévin Bakyono, Balozi mpya wa Burkina Faso mjini Vatican.  (Vatican Media)

Mheshimiwa Régis Kévin Bakyono Awasilisha Hati za Utambulisho Kwa Papa Francisko

Balozi Régis Kévin Bakyono alizaliwa tarehe 7 Mei 1977 ameoa na amebahatika kupata watoto wawili kama zawadi kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Baada ya masomo na majiundo yake katika medani mbalimbali za maisha, kunako mwaka 2023 anamalizia masomo kwa ajili ya Shahada ya Uzamivu katika Fasihi Andishi. Ni kiongozi mwenye uzoefu mkubwa katika masuala ya uongozi kitaifa na kimataifa. Sekretarieti kuu ya Vatican inamkaribisha kwa mikono miwili.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 25 Machi 2023 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mheshimiwa Régis Kévin Bakyono, Balozi mpya wa Burkina Faso mjini Vatican. Itakumbukwa kwamba, Balozi Régis Kévin Bakyono alizaliwa tarehe 7 Mei 1977 ameoa na amebahatika kupata watoto wawili kama zawadi kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Baada ya masomo na majiundo yake katika medani mbalimbali za maisha, kunako mwaka 2023 anamalizia masomo kwa ajili ya Shahada ya Uzamivu katika Fasihi Andishi.

Balozi Regis Bakyono awasilisha hati za utambulisho.
Balozi Regis Bakyono awasilisha hati za utambulisho.

Tangu mwaka 2002 amebahatika kufanya kazi mbalimbali nchini Burkina Faso kama: Mtafiti, Mshauri katika Mashirika ya Kimataifa, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa; Mkuu wa Kitengo katika Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kati ya Mwaka 2022 hadi mwaka 2023 aliteuliwa kuwa ni Mtaalam mshauri wa mambo ya kiufundi katika masuala ya ushirikiano na mafungamano ya Kikanda Barani Afrika.

Hati za Utambulisho

 

25 March 2023, 15:49