Ask.Mkuu Caccia:wanawake wanaweza kutoa mchango wa kipekee wa amani!
Na Angella Rwezaual; - Vatican.
Mwakilishi wa kudumu wa Vatican Askofu Mkuu Gabriele Caccia katika makao ya Umoja wa Mataifa wa Baraza la Usalama,alitoa hotuba yake Mjadala wa wazi kuhusu “Wanawake, amani na usalama: Kuelekea maadhimisho ya miaka 25 ya azimio 1325 (2000)”. Tarehe 7 Machi 2023 huko New York Marekani. Katika hotuba hiyo aisema ni kwa wakati na inafaa kwamba tutathmini upya jinsi bora ya kushughulikia mahitaji ya kipekee ya wanawake katika migogoro na jukumu lao muhimu katika kuzuia na kutatua. Katika miaka michache iliyopita, unyanyasaji-ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia-dhidi ya wanawake na wasichana umeongezeka, wakati uwakilishi wa wanawake katika michakato ya amani umepungua, na kuoneesha kwamba mbinu ya sasa inapungua.
Askofu Caccia alisema kwamba Papa Francisko mwezi Januari akiwahutubia Baraza la Wanadiplomasia lililoidhinishwa Vatican alisema, “wakati haki za binadamu zinatambuliwa kikamilifu kwa wote, wanawake wanaweza kutoa mchango wao wa kipekee kwa maisha ya jamii na kuwa washirika wa kwanza wa amani.” Vilevile akiwa ziara ya kitume huko DRC na Sudan Kusini ilionesha uwezo wa wanawake kubadilisha jamii zenye jeuri kuwa za amani, wakati “wanapolindwa, kuheshimiwa, na kuthaminiwa.” Ili kufungua uwezo huo, Baraza hilo lazima lihakikishe kwamba wanawake, hasa mama wanaojua jinsi maisha yanavyozalishwa na kulindwa wanapata fursa za kushiriki kikamilifu katika michakato ya amani na katika nyanja zote za "maisha ya kisiasa na michakato ya kufanya maamuzi.
Ajenda ya Wanawake na Amani na Usalama haiwezi kutekelezwa kwa mafanikio isipokuwa vichochezi vya msingi vinavyochangia hali mbaya ya wanawake na wasichana vitakapo shughulikiwa. Haya ni pamoja na sio tu migogoro kama vile vita vya kuchukiza nchini Ukraine na migogoro inayosahaulika mara kwa mara katika Afrika na Mashariki ya Kati, lakini pia misimamo mikali na upotevu wa rasilimali zaidi kuelekea matumizi ya silaha, ikiwa ni pamoja na silaha za nyuklia, ambazo madhara yake yanaathiri wanawake na wasichana. Askofu mkuu akihitimisha alirejea tena maneno ya Baba Mtakatifu Francisko, anayetambua kwamba “upendo mwororo wa akina mama, wanaoupa tiulimwengu uhai, na uwepo wa wanawake ni njia mbadala ya kweli ya mantiki mbaya ya mamlaka inayoongoza kwenye vita.