Tafuta

2023.02.03 Mkutano wa Kibara huko Austalia wa Sinodi. 2023.02.03 Mkutano wa Kibara huko Austalia wa Sinodi. 

Kard.Grech kwa Makanisa ya Australia:sinodi lazima iongoze katika utume

Katika ujumbe wake kwa njia ya video,Kardinali Grech,Katibu Mkuu wa Sinodi amewahutubia Maaskofu walioanza mkutano wao wa kibara huko Suva katika Visiwa vya Fiji hadi tarehe 10 Februari.Ujasiri ushinde,bila woga wa kusema,kusikiliza,kubadilisha mawazo yao.Misa na hotuba ya utangulizi wa Kardinali Czerny.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kanisa katika awamu hii ya kihistoria iwe mfano wa vigae vilivyounganishwa  pamoja na katika sinodi na inaweza kueleweka kutoka katika jiografia na kutokana na mwingiliano wa mkutano wa siku hizi. Kuna mkutano mwingine wa  bara la Ulaya unaokwenda  sambamba katika juma hili huko Praga na kivitendo katika viwanja vingine kunzia tarehe 5 Februari  hadi Ijumaa ijayo huko Suva katika Visiwa vya Fiji, katika Baraza Kuu la Maaskofu wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki wa bara la Australia(FCBCO). Kati ya  mada zake kuu,  kitovu ni Sinodi. Ndivyo ameanza kueleza ujumbe wake kwa njia ya video, Kardinali Mario Grech, Katibu wa Sinodi ya Maaskofu, akieleza kwa namna ya pekee maaskofu  wa Australia, New Zeland, Papua New Guinea, Visiwa vya Solomoni, lakini pia hata maeneo mengine ya Bahari ya Pasifiki.

Wajumbe wa utambuzi na kuandika katika Mkutano wa Shirikisho la Mabaraza ya Maasjofu Austalia na visiwa vyake
Wajumbe wa utambuzi na kuandika katika Mkutano wa Shirikisho la Mabaraza ya Maasjofu Austalia na visiwa vyake

Kardinali Grech amethibitisha juu ya mtazamo wa kupendeza wa sinodi ambao kwayo wanaweza kuiishi makabiliano, yale ya mazungumzo, njia pekee ambayo wanaweza kukua kama Kanisa. Katibu mkuu wa Sinodi ya Maaskofu amesema mtindo wa mazungumzo hayo, yaliyoundwa na unyoofu wa hotuba, yaambatane na unyenyekevu wa kusikiliza. Hili ni muhimu katika Sinodi zote na pia ni muhimu wakati wa Mikutano ya kibara. Kwa hiyo ushauri wake ni kwamba wasiogope kuzungumza, kusikiliza, wajitahidi kuwakaribisha na kuwaelewa wengine. Na wasiogope kubadilisha mawazo yao kulingana na kile wanachosikia. Kwa upande wake amezidi kusisitiza kuwa sinodi inafanya kazi inapoelekezwa kwenye huduma ya utume, na kwamba zoezi hilo la utambuzi wa kikanisa ndilo ambalo Mkutano wa  mabara yanaitwa kupitia na  ndivyo inavyoweza zaidi kuwa na uwezo kutambua kile ambacho Roho anachochochea Makanisa ya kila bara, na ndivyo Mkutano wa Sinodi utakavyokuwa wa kusisimua zaidi  mwezi Oktoba ujao, amehitimisha Kardinali Grech katika ujumbe wake kwa njia ya Video.

Kard Grech
Kard Grech

Saa kumi jioni kwa saa mahali za Fiji, naye Kardinali Czerny  ambaye alikuwa ameongoza Misa ya ufunguzi asubuhi na mahubiri yaliyohusu wito wa Kikristo kuwa chumvi na nuru ya ulimwengu, alizindua kazi ya Baraza la Maaskofu wa Australia kwa hotuba iliyojikita katika mada mbili:  ya kwanza kuhusu mabadiliko ya tabianchi na sinodi. Katika mada ya kwanza, Kadinali Czerny alichukua maoni yake kutoka katika Waraka wa Kitume wa Laudato si' na kutokana na  dhana kuu inayojiwakilisha jina la Baraza lake la Kipapa analoliongoza la Huduma ya maendeleo fungamani ya  mwanadamu.

Bara la Ausralia na visiwa vyake
Bara la Ausralia na visiwa vyake

Ikiwa ardhi ya kifahari ya Fiji ambayo mwenyeji wa mkutano wa maaskofu ni mfano wa ardhi iliyobarikiwa na Mungu, utajiri huu wenye aina nyingi na rasilimali, alisisitiza, inaonesha kwa kulinganisha upande wa pili wa sarafu, unyonyaji usio endelevu na usio wa haki, ambao unakumbusha majanga mengine kama vile uharamia baharini, uchafuzi wa bahari, mmomonyoko wa pwani na zaidi ya yote uhamiaji wa kukata tamaa wa wahamiaji wa mabadiliko ya Tabianchi, aliorodhesha hayo Kadinali Czerny. Kwa hiyo katika wimbi la mafundisho ya Papa Francisko,  Kardinali aliwahimiza wachungaji kukemea mazingira yote ambayo maisha na asili vinatishiwa na kutangaza mtazamo wa ulinzi wa  kazi ya Uumbaji kwa kujifunza, na zaidi kupitia kwa na kaka na dada zetu wa kiasili, ambao wametunza kazi ya Uumbaji kwa karne nyingi.

Jitihada za kukaripia na kutangaza mabaya

Jitihada hizo za  kukaripia na kutangaza, aliendelea Kardinali Czerny, hata hivyo zinahitaji awamu ya kutafakari, ya utambuzi, sahihi wa mchakato wa sinodi na hiyo ni kipengele kilichosisitizwa vyema, huku akikumbuka, katika barua iliyotumwa siku chake zilizopita na Makardinali Grech na Hollerich. Kwa hiyo Sinodi kimsingi ina maana ya kufanya mabadiliko, kuwa na uongofu wa kichungaji na kimisionari wa Kanisa zima, ambalo unamaanisha upya wa mawazo, mitazamo, mazoea na miundo kwa sababu hivyo ndivyo Mungu anatarajia kwa Kanisa la leo hii. Kusudi la Sinodi, alihitimisha, Kardinali Czerny, ni kupanda ndoto, kuamsha unabii na maono, kufanya tumaini kusitawi, kutia moyo uaminifu, kuponya majeraha, kusuka mahusiano, na kuamsha mapambazuko ya matumaini.

Mkutano wa Kibara kuhusu sinodi huko Suva na Fiji
05 February 2023, 14:57