Stempu mpya za Vatican:Miaka kumi ya Papa,Jubilei 2025 na 550 ya Copernicus
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Ni kutoa heshima kwa miaka 10 ya upapa kupitia wingi wa alama. Bahasha ya philatelic ya 2023 ya Vatican inafanya kumbukumbu ya miaka kumi ya kuchaguliwa kwa Papa Francisko itakayoadhimishwa mapema karibuni mwezi ujao. Ni mchoro mwepesi mweusi na mweupe unaopiga picha wakati Papa anapokea pete ya Mvuvi, mwanzoni mwa upapa wake. Pete ina mapokeo ya milenia na inawakilisha Petro, mvuvi wa roho (Mt 4, 18-19; Mk 1, 16-17). Inavaliwa kwenye kidole cha kila Papa ili kufanya muhtasari ndani yake yenyewe maana ya mthibitishaji wa imani, akiifanya kwa upya kazi aliyokabidhiwa mtume Petro kwanza ya kuwathibitisha imani ndugu zake (Lk 22:32). Muhuri wa thamani, pamoja na kufutwa kwa philatelic,una msemo ambao Kardinali Hummes alimwambia Kardinali Bergoglio wakati alipochaguliwa kuwa Papa: “Usiwasahau maskini.”
Misa tarehe 19 Machi 2013
Na tena ili kuadhimisha miaka 10 ya Upapa, mfululizo wa stempu nne zimetolewa, kila moja ikiwa na picha ya Papa Francisko katika fursa mbali mbali kama vile: Misa ya tarehe 19 Machi 2013, mwanzo wa majisterio yake; huku akibusu Injili kuadhimisha Siku ya Neno iliyoanzishwa kwa Waraka wa Kitume wa Misericordia et misera” wa tarehe 20 Novemba 2016, na kuweka Dominika ya tatu Januari na Motu Proprio Aperuit illis ya tarehe 30 Septemba 2019; chapisho la tatu huku Papa Fransisko akipatanisha mtu aliyetubu, hivyo kukumbuka mpango uliotokana na Jubilei ya Huruma, ya “masaa 24 kwa ajili ya Bwana” na kuhimiza waamini, hasa wale wadogo, kukaribia sakramenti ya Upatanisho.
Uwakilishi wa kumbu kumbu ya ziara za Papa
Hatimaye, katika thamani ya nne, Papa Francisko anawakilishwa akiwa katika kumbukumbu wakati wa ziara yake ya kwanza ya kichungaji huko Lampedusa, mnamo tarehe 8 Agosti 2013, kabla ya kutupa shada la maua baharini ambako wakimbizi wengi wamefariki. Stempu iliyoweka alama ya posta inasherehekea Pasaka 2023, ambayo pia imechochewa na kumbukumbu ya miaka kumi ya kuchaguliwa kwa Papa Francisko, inatolewa tena kazi ya msanii wa Hispania Raúl Berzosa, iliyoundwa kwa hafla hiyo, ambayo inawakilisha taswira inayotambulika ya Ufufuko wa Bwana, ikifafanuliwa na kifungu kutoka Injili ya Luka na picha: “Hakika Bwana amefufuka na kumtokea Simoni!” ( Lk 24:34 ). Thamani hii pia, pamoja na sura ya Petro mbele ya Kristo mfufuka, inahusishwa na utume wa upapa; kwa mfano, kondoo katika sehemu ya mbele inahusu kukabidhiwa kwa Petro ili kulisha kondoo wa zizi lake (Yn 21:17).
Afrika ni hatua ya msingi katika safari ya kuelekea Jubilei ya matumaini
Ni rangi ya Bluu kali inayotawala kwenye kipeperushi, kilichojaa marejeo ya Afrika. Sura ya Yesu Kristo ananyoosha mkono wake kuelekea mstari wa watu wanaotembea kuelekea kwake, ili kuwakilisha hija bora kuelekea Jubilei itakayofanyika mwaka wa 2025. Baada ya kutengeneza ile ya visiwa vya Astalia kufungua njia ya Asia, iliyotolewa tena katika masuala ya miaka iliyopita na vipeperushi sawa sasa tunafikia bara la Afrika. Katikati, muhuri unaonesha ramani ya bara la Afrika, marudio ya safari ya mwisho ya kitume ya Papa Francisko, na karibu na hiyo picha ya kahawia ya Mama yetu wa Afrika, picha ya shaba iliyotolewa mnamo mwaka wa 1840 kwa Dupuch, Askofu wa kwanza wa Algiers, na kwenye chumba chake nakala ya sanamu iliyotengenezwa mnamo 1750 na mchongaji wa Kifaransa Edmé Bouchardon.
Mama yetu wa Afrika
Baada ya kutangazwa kwa Dogma juu ya Mama Mkingiwa dhambi ya asili mnamo tarehe 8 Desemba 1854 na Papa Pio IX, picha ya Bikira iliwekwa katika Kanisa Kuu kwenye kikanisa la huko Algiers, mahali pa hija kama Mama Yetu wa Afrika. Madhabahu yaliyojaa vitu vya ibada na mahujaji pia wa imani ya Kiislamu, kwa hiyo ni ishara ya mazungumzo na kukutana, ambayo yametiwa muhuri na maandishi katika kanisa: kwamba “Mama yetu wa Afrika, utuombee sisi na Waislamu”, pia imeripotiwa kwa Kiarabu na katika lugha ya cabile. Hata alama ya posta inachukua tema sawa na hiyo kuwa : bara la Afrika na sura mbili kama mahujaji wanaoshikilia msalaba.
Uhusiano mzuri kati ya sayansi na imani
Hatimaye, kipeperushi na alama maalum ya posta inasherehekea kumbukumbu ya miaka 550 ya kuzaliwa kwa Nicolaus Copernicus. Ni suala la pamoja na Poland, mahali pa kuzaliwa kwa mtaalimungu, mwanahisabati na mnajimu wa karne ya 15. Copernicus, alizaliwa hukoToruń mnamo 1473, ndiye mwandishi wa hati ya unajimu juu ya mapinduzi ya nyanja za anga ma ,zunguko wake iliyochapishwa mnamo 1543, ambayo alionesha nadharia ya heliocentric dhidi ya ile iliyoungwa mkono hadi wakati huo katikati ya ulimwengu.
Kanisa halidai kushika maendeleo ya ajabu ya sayansi
Maadhimisho haya sio tu kuhusu kupongeza mwanasayansi mkuu lakini pia juu ya kufanya kwa upya tafakari ya uhusiano kati ya sayansi na imani. Baba Mtakatifu Francisko aliandika katika Waraka wa Kitume wa Evangelii Gaudium: “Kanisa halidai kushika maendeleo ya ajabu ya sayansi, kinyume chake, Kanisa linafurahi na hata kushangilia kwa kutambua uwezo mkubwa ambao Mungu ametoa kwa akili ya Binadamu”. Picha iliyooneshwa kwenye picha ndogo ya philatelic inazalisha tena kazi ya mchoraji wa Kipolandi Jan Matejko, aliyeishi katika karne ya 19, yaani Mtaalamu wa nyota Copernicus au Mazungumzo na Mungu iliyofanywa kati ya 1871 na 1873 katika tukio la kuadhimisha miaka 400 ya kuzaliwa kwake.