Kongamano Kimataifa:Wachungaji na waamini walei wanaitwa kutembea pamoja
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Kuanzia tarehe 16-18 Februari 2023 kutakuwa na Kongamano linaongozwa na tema:“Wachungaji na waamini walei wanaitwa kutembea pamoja.” Jumanne tarehe 14 Februari 2023, limewakilishwakwa maana hiyo Kongamano hilo la Kimataifa, kwa ajili ya Marais na wahusika wa Tume za Maaskofu kwa ajili ya Walei, ambapo litawaona wajumbe 210 kutoka ulimwenguni kote, ambapo litafanyika katika ukumbi mpya wa Sinodi mjini Vatican. Hawa wanatoka katika Mabaraza ya maaskofu 74 na Harakati za kikanisa 29 na mwisho wa mkutano huo Papa atakwenda katika Ukumbi kusikiliza washiriki wa mkutano huo.
Kongamano hilolimeandaliwa na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha. Kwa hiyo waliowakilisha Kongamano ni Kardinali Kevin Farrell, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Walei, Familia na Maisha; Dk. Linda Ghisoni, Katibu msaizidi wa Baraza hilo, Kardinali Gérald C. Lacroix, Askofu Mkuu wa Québec, Canada, na Mjumbe wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Walei, Familia na Maisha; Dk. Andrea Poretti, Mlei na mhusika wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio nchini Argentina.
Ufunguzi wa uwakilishi
Katika kufungua uwakilishi wa kongamano hilo kwa vyombo vya habari Vatican, Kardinali Kevin Farrell, alizindua kwa mada ya siku hiyo kwenye Ofisi ya Habari Vatican, kwamba “bado haijawa jambo la kawaida la kufanya kazi bega kwa bega, akitazama tema inayoongoza Kongamano hilo: “Wachungaji na waamini Walei wameitwa kutembea pamoja ” Katika mada ya sinodi, Kardinali amefikiria kwamba kuna utume mwingi ambao mapadre hawana uwezo wa kuutekeleza na ni bora kuwakabidhi walei. Aliendelea kusema Kardinali Farrell , huku akijibu swali la waandishi wa habari kwamba ushiriki wa Walei katika maisha ya Kanisa linasalia kuwa la hapa na pale, likifanya kazi kwa shughuli fulani iliyowekewa mipaka iliyokabidhiwa kutoka juu. Kwa hakika, mada inalingana kikamilifu na mada kwa ujumla ya Sinodi kuhusu hatua za kibara ambazo zinaendelea kufanyika katika majuma haya na kuendelea.
Ushirikiano na waamini na wachungaji
Kardinali Farrell alisisitizia ushirikiano mkubwa kati ya waamini walei na wachungaji katika katekesi, na pia katika liturujia, au katika shughuli za upendo, katika njia ambayo tayari imeoneshwa na Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican. Hili ni suala linalochukuliwa kuwa muhimu kwa wakati huu na ambalo liko karibu sana na moyo wa Papa, kiasi kwamba aliomba waziwazi kuwepo katika Ukumbi siku ya tatu na kusikiliza sauti za wageni hao.
Afrika itawakilishwa na nchi 20, kutoka Asia 13 , 7kutoka Amerika Kaskazini na Amerika ya Kati, 7 kutoka Amerika Kusini na 24 kutoka Ulaya. Kwa hiyo kuna jumla ya wajumbe 210 waliosajiliwa (walei 107, mapadre 36 na maaskofu 67) wakiwa ni kutoka mabaraza 74 ya maaskofu na harakati za kikanisa 29. Haya yote yataleta utajiri wao wa Karama na taratibu za elimu zenye ufanisi wanazoshiriki, alisema hayo Bi Linda Ghisoni, katibu Msaidizi wa Baraza hilo akisaidia walei wengi kuishi uwajibikaji tendaji katika maisha ya Kanisa. Zaidi ya hayo, hotuba 16 fupi za kushirikisha uzoefu zilikuwa tayari zinaendelea katika mabara, kuanzia Papua New Guinea hadi Mexico, Madagacar hadi India, kutoka Brazil hadi Poland, kutoka Guatemala hadi Ufaransa.
Kukuza michakato ya pamoja ya kufanya maamuzi
Kongamano si kieleleza kile cha kifu cha 132 cha Katiba ya Kitume ya Evangelium ya Praedicate, alieleza Bi Ghisoni, ambacho kilisisitiza haja ya kuamsha ufahamu wa kuwa wa kundi moja ambalo ni Kanisa. “Tunahitaji kuhamasisha michakato ya pamoja, ya kufanya maamuzi isiyo ya kisekta”, lilikuwa pendekezo lake Andrea Poretti, mlei na anayewajibika katika Jumuiya ya Mtakatifu Egidio nchini Argentina, pia alizungumza, huku akisimulia jitihada ya kihistoria ya kujikita pamoja na maskini na kwa ajili ya amani kama mfano halisi wa ushirikiano huo. Utume wa walei kanisani haupaswi kupunguzwa kwa jukumu la utendaji tu, kama vilekwa wachungaji hawawezi kuchukuliwa kuwa wasimamizi”, alitoa maoni yake Kardinali Gérald C. Lacroix.