Tafuta

2023.02.15 Padre Michel Jalakh, Katibu mpya wa Baraza la Kipapala Makanisa ya Mashariki. 2023.02.15 Padre Michel Jalakh, Katibu mpya wa Baraza la Kipapala Makanisa ya Mashariki. 

Katibu mpya wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki

Padre Michel Jalakh, O.A.M., ametuliwa na Papa kuwa Katibu wa Baraza la Kipapa la Mashariki ya kati.Kabla ya uteuzi huo alikuwa Gambera wa Chuo Kikuu cha Antonine huko Baabda nchini Lebanon

Na Angella Rwezaula;- Vatican.

Jumatano tarehe 15 Februari 2023, Baba Mtakatifu amemteua Katibu wa Baraza la makanisa ya Mashariki ya Kati  Padre Michel Jalakh, O.A.M., ambaye hadi uteuzi huo alikuwa Gambera wa Chuo Kikuu cha Antonine huko Baabda nchini Lebanon.

Wasifu wake

Padre Jalakh alizaliwa tarehe 27 Agosti 1966 huko Baouchrieh Lebanon. Tarehe 15 Agoti 1983 alifunga nadhiri za kwanza katika Shirika la Antony Maroniti na tarehe 21 Aprili 1991 alipewa daraja la upadre. Tangu Desemba 2022 hadi Julai 2008 alikuwa kama Katibu kwenye Baraza la Kipapa la  Makanisa ya Mashariki.

Masomo yake ya  anayo Shaahada ya Masomo ya Kikanisa katika Taasisi ya Kipapa Mashariki Roma, Italia mnamo 2008. Tangu 2013 hadi 2018 alikuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Mashariki na Mjumbe wa Tume ya Kiekumene ya Mahusiano  ya Mapatriaki Katoliki, na  Baraza la Maaskofu wa Lebanon. Profesa wa Chuo Kikuu cha Antonine huko Baabda, na alikuwa gambera tangu 2017.

15 February 2023, 13:38