Tafuta

2021.01.11 Bambino Gesu’: Bi Mariella Enoc aliyekuwa Rais wa Hospitali ya Kipapa amejiuzulu. 2021.01.11 Bambino Gesu’: Bi Mariella Enoc aliyekuwa Rais wa Hospitali ya Kipapa amejiuzulu. 

Hospitali ya Bambino Gesù:Rais Mariella Enoc amejiuzulu

Alitangaza:“Ni kitendo cha uwajibikaji,kwa sababu niliona ni jambo la manufaa kwa hospitali kutazamia mwisho wa mamlaka yangu ili kuhakikisha kwamba kazi kubwa ya Kituo kipya cha Gianicolo kinafanywa na yeyote ambaye ana jukumu la kutekeleza.Kwa wakati huu ukaribu wa Baba Mtakatifu unanisaidia sana”

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Mariella Enoc amejiuzulu kutoka katika urais wa Hospitali ya Kipapa ya Bambino Gesù, ambapo Yeye mwenyewe alilekeza kuwa ni  muhimu kwa manufaa ya hospitali kwa kutazamia mwisho wa jukumu lake ili kuweza kuhakikisha kuwa shughuli kubwa ya makao makuu mapya yaliyo  Gianicolo yaendeshwe na yeyote ambaye ana jukumu la kukamilika kwake.  Siku zilizopita kwa mujibu wa taarifa wa vyombo vya habari  Vatican alisema kwamba alikutana na Katibu wa Vatican na siku chache zilizopita na Baba Mtakatifu Francisko na kuwaeleza wao, kwamba ilikuwa vizuri kwa Hospitali hiyo kutazamia mwisho  wake wa jukumu hilo. Kwa mujibu wake alisema Hospitali inakabiliwa na wakati wa ukuaji mkubwa na mipango mingi inaendelea na kwa hivyo anaamini kwamba wanaweza kuelewa kwamba nia yake ni kitendo cha uwajibikaji na upendo kwa ajili ya Bambino Gesu’. Kwa hiyo aliongeza kusema kuwa “Katika wakati huu ninasaidiwa na ukaribu wa Baba Mtakatifu”.

Aliteuliwa kuongoza Hospitali ya Kipapa mnamo Februari 2015

Bi Mariella Enoc aliteuliwa kuongoza Hospitali ya Kipapa,  ya Bambino Gesù mnamo Februari 2015. Mamlaka hayo yalisasishwa tena mnamo 2017 na 2021 na yalikuwa yanakwisha mwaka huu,  kwa idhini ya taarifa za kifedha za 2023. Ni jitihada yake kubwa ya kutoa msukumo mpya kwa hospitali hiyo. Mnamo Julai mwaka 2022, ripoti ya uendelevu ya hospitali ya watoto kwa 2021 iliwasilishwa, na karibu huduma milioni mbili na nusu ya wagonjwa wa nje na 28,000 ya wagonjwa wa kulazwa hospitalini, ambapo 30% kati yao  ni kutoka nje ya mkoa, zaidi ya 31,500 za upasuaji na kuingilia kati , usafirishaji wa dharura wa watoto wachanga mia tatu, 126 kupitia helicopta ya Vatican. Kwa upande wa upandikizaji wa viungo, seli na tishu, 358 zilifanywa, ambazo lazima ziongezwe zile za moyo bandia 7. Kwa upande wa shughuli za kisayansi, miradi ya utafiti ilikuwa na alama  + 28%, kwa uangalifu maalum kwa magonjwa adimu na saratani, na majaribio ya kliniki + 50%, yanayohusisha wagonjwa wapya 3,517.

Hospitali inasaidia watoto na familia ndani na nje ya Italia

Katika mahojiano na vyombo vya habari vya Vatican mnamo  Desemba 2022, alisimulia  juu ya uangalifu wa kipekee kwa watoto na familia zao, hasa wakati wa Noeli: “Katika hospitali yetu, familia zinaweza kukaa karibu na watoto wao. Hata katika uangalizi maalum, mshiriki wa familia anaweza kukaa karibu na mtoto na huu ni uchaguzi ambao nilikuwa naupinga sana lakini kiukweli ilieleweka badala yake ni msaada ambao uwepo huo unawapa watoto kupambania kufa na kupona. Hivyo tunahakikisha wanaweza kuwa pamoja. Tunasaidia pia familia wanaotoka mbali, ambazo wakati mwingine ni familia ya  mama tu au baba pekee, ambao huingia kwenye mzunguko wa familia nyingine zote ili mwishowe mtu ahisi ladha ya familia iliyopanuliwa”. Bi Enoc vile vile alisisitiza  juu ya ukaribisho wa watoto wengi wa Kiukreni waliokimbia nchi yao kwa sababu ya vita.

Nyadhifa nyingine katika jamii

Bi Enoc alizaliwa huko Novara, Italia mnamo  mwaka 1944. Baada ya masomo ya kiutamaduni na utabibu, alifanya kazi mfululizo katika usimamizi na usimamizi wa vituo vya Kiafya. Tangu 2012 amekuwa msimamizi maalum wa Hospitali ya Valduce huko Como Italia  na alikuwa kwa miaka 10 katika Hospitali ya Cottolengo huko Torino. Alikuwa rais wa Confindustria Piemonte Tangu 2008 hadi 2012. Daima akifanya kazi katika sekta ya upendo, alikuwa makamu wa rais wa Mfuko wa Cariplo kuanzia 2004 hadi Mei 2019 na makamu wa rais wachama cha Mfuko wa  Cini tangu 2008 hadi 2020. Kwa sasa ni mwanachama Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Padre Gnocchi na Rais wa Mfuko wa ISMU.

Hospitali ya Kipapa ilizaliwa 1869

Hospitali ya watoto ya Kipapa ya Bambino Gesù, ilizaliwa mnamo mwaka wa 1869 kwa mpango wa wafalme Salviati, na ilitolewa kwa zawadi kwa Vatican mnamo  mwaka 1924, ikawa kwa nia na madhumuni yote  ya Hospitali ya Papa. Ikiwa na vitanda 607, maeneo 5  katika (Gianicolo, Mtakatifu  Paolo na Baldelli,  jijini Roma; Palidoro na Mtakatifu Marinella (kwenye pwani ya Mkoa wa Lazio) na uwepo wa utaalam wote wa watoto, kwa umakini mkubwa katika  ugumu wa hali ya juu, ambapo  leo hii ndio kituo kikuu cha utafiti wa  afya ya watoto, vijana barubaru barani Ulaya, na ni mahali pa kumbukumbu kwa ajili ya afya ya watoto kutoka Italia na nchi za nje.

Rais wa Hospitali ya Bambino Gesu ajiuzulu
05 February 2023, 14:42