Chama cha Mfuko wa Joseph Ratzinger,kushiriki miza ya kumuombea Papa Benedikto XVI
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Jumanne tarehe 31 Januari 2023 wanachama wa Mfuko wa Joseph Ratinger wameshiriki Misa Takatifu katika Groto za Vatican,i liyoongozwa na Askofu Mkuu Georg Gänswein kwa ajili ya kumuombea Hayati Papa Mstaafu Benedikito XVI ikiwa ni mwezi mmoja tangu alipoitwa na Mungu Baba Mwenyezi mnamo tarehe 31 Desemba 2022. Katika mahubiri yake, Askofu Mkuu Gänswein na ambaye alimsindikiza kipinid chote hiki hadi kifo chake, amekumbuka sura ya Mtakatifu Benedikito Giuseppe Labre, aliyefariki jijini Roma mnamo tarehe 16 Aprili 1783 (tarehe 16 Aprili ilikuwa ni tarehe ya kuzaliwa kwa Joseph Ratzinger), Mtakatifu ambaye Papa Mstaafu alishirikisha jina la Ubatizo, Yosefu na ambapo baadaye alichukua jina la Upapa wake Benedikto. Licha ya kuhisi ukosefu wake kimwili, Askofu Mkuu Gänswein alibainisha jinsi gani Papa Benedikito XVI kwake yeye leo hii anamwihisi uwepo wake kiroho.
Mwishoni mwa misa hiyo iliyohudhuriwa na ‘Memores Domini’ ambaye alimsaidia Papa Mstaafu Benedikto XVI katika miaka ya upapa wake na kisha katika nyumba ya Monasteri ya Mater Ecclesiae, katibu wake Sista Birgit Wansing na watu wengine ambao, kama mapadre wasaidizi wa misa walikuwa karibu naye kwa muda wa miaka mingi, walijiunda kwa pamoja katika maombi kwenye kaburi lake.