Askofu mkuu Tomasz Grysa, Balozi wa Vatican Visiwa Vya Ushelisheli
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu mkuu Tomasz Grysa, kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Seychelles “Visiwa vya Ushelisheli” na ataendelea kuwa pia Balozi wa Vatican nchini Madagascar na Mwakilishi wa Kitume kwenye Visiwa vya Comoro na vile vya Réunion. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Tomasz Grysa alizaliwa tarehe 16 Oktoba 1970 huko katika Jimbo kuuu la Poznań nchini Poland. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kipadre tarehe 25 Mei 1995 akapewa Daraja Takatatifu ya Upadre.
Tarehe 27 Septemba 2022 akateuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi wa Vatican nchini Madagascar na Mwakilishi wa Kitume kwenye Visiwa vya Comoro. Akawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu tarehe 1 Novemba 2022 na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican. Na tarehe 9 Februari 2023, Baba Mtakatifu amemteuwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Madagascar na Mwakilishi wa Kitume kwenye Visiwa vya Comoro na vile vya Réunion.