Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa sana Padre Jean-Marie Vianney kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Kibungo, Rwanda. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa sana Padre Jean-Marie Vianney kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Kibungo, Rwanda.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Askofu Jean-Marie Vianney Twagirayezu, Jimbo Katoliki la Kibungo, Rwanda

Askofu mteule Jean-Marie Vianney Twagirayezu alizaliwa kunako tarehe 21 Julai 1960, Jimboni Nyundo. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 8 Oktoba 1995 akapewa Daraja takatifu ya Upadre, kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Nyundo. Tangu wakati huo kama Padre amewahi kuwa Paroko katika Parokia ya Muramba na Kibingo kati ya Mwaka 1995-1997. Huduma!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ametemtea Mheshimiwa sana Padre Jean-Marie Vianney Twagirayezu, kutoka Jimbo Katoliki la Nyundo, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Kibungo, lililoko nchini Rwanda. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteule Jean-Marie Vianney Twagirayezu, alikuwa ni Katibu mtendaji wa Shirika la Misaada ya Kanisa Katoliki nchini Rwanda, Caritas Rwanda. Itakumbukwa kwamba, Askofu mteule Jean-Marie Vianney Twagirayezu alizaliwa kunako tarehe 21 Julai 1960, Jimboni Nyundo. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 8 Oktoba 1995 akapewa Daraja takatifu ya Upadre, kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Nyundo. Tangu wakati huo kama Padre amewahi kuwa Paroko katika Parokia ya Muramba na Kibingo kati ya Mwaka 1995-1997.

Huduma ya Injili ya Upendo kwa watu wa Mungu
Huduma ya Injili ya Upendo kwa watu wa Mungu

Baadaye alitumwa kujiendeleza kwa masomo nchini Ubelgiji kati ya Mwaka 1997 hadi mwaka 2000 na kujipatia Shahada ya Uzamili katika Taalimungu Uchungaji kutoka Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Louvain, “Université Catholique de Louvain, Belgium.” Baadaye aliteuliwa kuwa ni Mkurugenzi wa Caritas Jimbo Katoliki la Nyundo kati yam waka 2000 hadi mwaka 2009. Mchumi wa Jimbo kati ya Mwaka 2002 hadi mwaka 2009. Baadaye alitumwa tena kwenda nchini Ubelgiji kujiendeleza katika masuala uchumi na hivyo kujipatia tena Shahada ya Uzamili katika Masuala ya Kuratibu Miradi, kati ya mwaka 2009 hadi mwaka 2016. Tangu mwaka 2016 hadi uteuzi wake, tarehe 20 Februari 2023 amekuwa ni Katibu Mtendaji wa Caritas Rwanda.

Uteuzi Rwanda
20 February 2023, 15:37