Tafuta

2023.01.27 Zakia Seddiki  wakati wa kusalimiana na Papa Francisko siku ya kutoa ushuhuda juu ya kifo cha mme wake Balozi Luca Attanasio aliyeuawa Goma DRC 2023.01.27 Zakia Seddiki wakati wa kusalimiana na Papa Francisko siku ya kutoa ushuhuda juu ya kifo cha mme wake Balozi Luca Attanasio aliyeuawa Goma DRC  (Vatican Media)

Zakia mjane wa Attanasio:Ninasali kwa ajili ya Papa awape faraja Watu wa Congo

Mke wa Balozi wa Italia aliyeuawa mwezi Februari mwaka 2021 huko Gomma ametoa maoni kuhusu ziara ya Papa kwenda DRC." Ni ujumbe wa matumaini ya thati ya watu wanaoteseka".Vile vile alielezea mpango wa chama“Mama Sofia”kwa ajili ya kusaidia wanawake na watoto akifikiria ambavyo naye anatunza watoto wake watatu baada ya kifo cha mmewe.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Ziara ya Kitume ya  Papa Francisko  katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni ujumbe mzuri. Ujumbe thabiti wa matumaini kwa watu wanaoteseka wanaohitaji ishara ya amani na msaada wa kiroho. Kwa moyo wangu wote, ninasali nikiwa  karibu na Papa na kutumaini kwamba  atapeleka utulivu katika mioyo ya watu  waweze kusahau silaha na vurugu.  Hayo ni maelezo ya Zakia Seddiki  mwenye sauti ya upole. Yeye bado ni kijana kwa njia fulani ambaye alionekana karibu kuwa hawezi kuzuia nguvu ya maneno yake na juu ya yote ya nafsi yake,  ambaye aliyejeruhiwa  katika maisha kufuatia na kifo cha Luca mme wake. Luca Attanasio aliokwa ni  balozi wa Italia aliyeuawa  huko Goma, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mnamo tarehe 22 Februari 2021, ambapo kwa maneno ya mke wake Zakia alisema kwamba anamhuhisi kuwa hapo , kwa njia tofauti. Amezungumza hayo kwa njia ya simu ya Vatican News.

Luka yuko kati yetu

Mwanamke wa asili ya  Morocco mwenye imani ya Kiislamu alikuwa ameweka maneno sawa na rangi nyeusi na nyeupe katika utangulizi wa kugusa moyo wa kitabu cha mwandishi wa habari Fabio Marchese Ragona Luca Attanasio. Historia ya  balozi wa amani. Barua ya upendo kwa ‘Tintin’ wake mtamu, mfano wa kijana ambaye alikuwa anawakilisha Italia nje ya nchi.  Baadaye Zakia alirudia mwaka jana tarehe 22 Juni 2021 katika Ukumbi wa Paulo VI uliokuwa umejaa watu wapatao 5,000 kwa ajili ya Mkutano wa Dunia wa Familia, ambapo alitoa ushuhuda wake kama mke na mama. Kwa hiyo akizungumza na Vatican News alisema kuwa “Hata leo, ingawa Luca hayuko nasi tena, upendo huo, kwa sababu ni mzuri na wa kweli, unaendelea. Ni upendo usiofifia, ambao haufi,” alisema hayo  mbele ya Papa Francisiko ambaye pia alipata fursa ya kukutana naye binafsi.

Zakia karibu na watoto wake

Bi Zakia alichangamka  jioni ya siku ile na kwa hiyo alisisimka  zaidi anapofikiri kwamba siku chache zijazo Papa Francisko atakwenda kutembelea ardhi ambayo yeye na Luca walikuwa wamejenga vitu vingi, waliota mipango na kuanzisha mahusiano ya kibinadamu.  Kwa hiyo alisema: “Tuliishi nchi hiyo kwa bidii. Alikuwa akisimama kidogo  wakati wa  kuzungumza na simu, huku akivuta pumzi, sauti yake ilisikika kwa nguvu wakati fulani, lakini ambayo haukusikika ya kutoa machozi.  Hakutaka kukazia fikira ya mambo yaliyopita, licha ya uchungu ambao bado unaowaka, lakini alipendelea kuzungumzia urithi wa mume wake ambao yeye mwenyewe alithibitisha kuuendeleza. Urithi mkuu, alisisitiza, ni juu ya binti zao wote watatu: Sofia, Lilia na Miral. Yeye anazidi kuwakuza shukrani pia kwa msaada wa mama yake Malika, ambaye yuko kando yake kila siku akimsindikiza. Aliwaambia watoto wake kwamba baba yao alipata ajali: “Ni ngumu sana, niliwapa toleo kwamba ilikuwa ajali pamoja na Vittorio (Iacovacci, mlinzi wake) na kwamba kwa bahati mbaya daktari hakuweza kuwaokoa kwa sababu madaktari si mara zote wanaweza kuokoa watu”.

Tumaini la ukweli

Kiukweli, kuna maswali mengi. Kwa hiyo ni matumini ya Zakia kwamba Luca anaweza kuwapatia nguvu ya kushughulikia jambo hilo. Hata hivyo, mapema au baadaye, wakati wa ukweli utafika alisema Bi Zakia  huku , akihakikishia imani kamili kwa taasisi na pia mbele ya Papa katika ardhi ya Congo ili iwe chombo cha faraja kwa watu wanaoteseka na uongofu kwa wale wanaoendelea kufanya biashara kwenye damu ya watu. “Ni ishara ya ujasiri ya Papa Francisko, pia kwa afya yake. Alitaka safari hiyo, na hivyo yeye anajua umuhimu wake, kwamba italeta nini kwa watu wa Congo”.

Barabara ya umwagaji damu

“Kubaki na sintofahamu za kutojali, vita, ni sawa na kuwa washirika wa wale ambao wamesababisha mateso na ukosefu huo wa haki. Binafsi ninataka kumshukuru Papa kwa ishara hii ya upendo na kwa uwezo wake wa kukufanya ujisikie kuwa karibu na wale wenye uhitaji na Wakongo wana uhitaji kwelikweli” alisisitiza mke wa balozi anaendelea. “Tatizo la Congo ni kubwa zaidi, kwa sababu kwa miaka mingi kumekuwa na barabara ya umwagaji damu ambayo kila siku kuna wajane, yatima,  na hofu inatawala. Kama Mustafa Milambo  aliyekuwa dereva ambaye pia aliuawa 2021)... naye anawakilisha kila Mkongo anayefanya kazi kwenye mashirika ya kimataifa, ambaye ana dhamana ya kusaidia familia yake, lakini pia hofu ya kuondoka na kutorudi. Tunatumaini kweli kwamba kutakuwa na fursa ya nchi hiyo kuota, kuona mambo chanya, kwa sababu siku moja nchi hiyo itaweza kujua amani. Tutaishi pamoja bila silaha”.

Mahusiano ya kibinadamu na kusaidia wanawake

Bi Zakia tayari amekwisha rudi nchini Congo kama mara 2-3 zaidi baada ya kifo cha mme wake Luca, na pia ili  kufunga makazi alikokuwa anaishi na kurejesha vitu vyao kibinafsi, vile vile kuwasalimu wanawake na watoto ambao uhusiano wa kibinadamu ulikuwa umejengeka kwa miaka hii.  Pia alirejea kusimamia chama cha Mama Sofia, kilichoanzishwa  huko Congo na sasa kipo pia nchini Italia. Kupitia hilo, inasaidia na kusaidia wanawake na watoto wa nchi ambazo hazijaendelea. Ni moja ya mambo halisi ambayo, kulingana na mwanamke, mume anapaswa kukumbukwa: Mawazo yake ya amani, haki, mshikamano kati ya watu. Hata wasichana wetu wanahitaji kuendelea katika njia ambayo baba yao alikusudia. Kwa hiyo Luca ametuachia sote, hasa vijana, matarajio ya ndoto, kufanya uchaguzi na kuwa sehemu ya taasisi, ya kutumikia Serikali ambayo ni kazi inayoweza kufanywa na ubinadamu”.

Kazi ya Mama Sofia

Mipango yote ya Mama Sofia katika sekta ya afya, elimu na upatikanaji wa maji ya kunywa iko hai kwa sasa. Kuanzia na kikundi kazi  cha kujitegemea kiitwacho   “Watoto wa Balozi” na shukrani kwa  mpango ambao kwa nchi 12 za Afrika zitaweza kutolowa kozi zenye cheti kwa lugha ya kiitalioano na ufadhili mwingi wa kushiriki katika kozi za vyuo vikuu mtandaoni. “Yote haya ni njia ya kuwasilisha ujumbe madhubuti wa amani. Kila kitu kinaendelea na kwa kuwa Luca yupo tofauti, alikuwa msaidizi wa kwanza kama mume na mwanadiplomasia”. Bila shaka, pamoja na mipango ya muda mrefu, kuna maombi ya dharura. Na katika nchi tata na maskini sana kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo wao ni wa kudumu. “Tusonge mbele… Hebu tujaribu kukuza amani, haki, mshikamano kupitia shughuli za kiutamaduni na kijamii. Kilichotokea kwa familia yangu kinanipa nguvu zaidi ya kuwasaidia wanyonge, nikiishi katika mkasa huu ninahisi kuwa karibu na watu wanaoteseka. Ndiyo maana siwezi kuacha”

Kamwe sihisi kuwa peke yangu

Katika maohojiano hayo Bi Zkia alihakikisha kwamba katika kazi hiyo hajisikii kuwa peke yake: “Tunachoweza kufanya ni shukrani kwa watu wengi ambao wanahisi na kuelewa mateso ya wanawake na watoto, linapokuja suala la haki za kimsingi. Kuna watu wengi ambao wanajaribu kusaidia na kuanza kuunda upya ulimwengu, kama vile nilivyoota juu yake na Luca. Hii ni nguvu ya ziada ya kutokata tamaana. Na  sijisikihi peke yangu.”

Bi Zakia mwanamke mjane wa Balozi Luca aliyeuawa huko Goma nchini DRC
30 January 2023, 10:18