"Ukweli na upendo:moyo wa imani kikristo"
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Kimechapishwa kitabu chanye kichwa: “Ukweli na upendo:moyo wa imani Kikristo" ambacho kinataka kufafanua zaidi urithi mzima wa upapa wa Benedikto XVI unaweza kujumlishwa katika mchanganyiko huu. Kama inavyojitokeza wazi kutoka katika kitabu hicho, ambacho kinakusanya mafundisho muhimu zaidi ya umahiri wake uliowekwa nuru, kwa dhati alifanya kila awezalo ili kuonesha kwamba maana ya kweli ya maisha iko katika kutafuta ukweli na katika zawadi ya binafsi katika upendo. Ili kufikia lengo hilo, hata hivyo, uthibitisho wa kusadikishwa na thabiti wa ukuu wa Mungu ni muhimu, mojawapo ya mada ambayo Hayati Papa Mstaafu Benedikto XVI amesisitiza zaidi.
Kwa hiyo, katika muktadha wa uinjilishaji mpya, dhamira yake msingi ilikuwa ni kufanya ukuu huu ugunduliwe kwa upya, hasa katika nchi zenye mizizi ya kale ya Kikristo, ambako umepotea kwa sababu ya mawazo ya kiulimwengu, kwa kupenda mali na kutamani. Katika kipindi chote cha upapa wake, kama mtaalimungu na mchungaji, Papa Mstaafu Benedikto XVI alikuwa msafiri mnyenyekevu, na katika safari hiyo ya pamoja kuelekea imani yenye ufahamu zaidi na iliyokomaa, ambayo hakuridhishwi tu na kile alichopata, lakini pia ambaye kila mara alitafuta mwanga mpya, furaha ya kukutana na Bwana mfufuka.
Hayati Papa Mstaafu aliandika: “Ni unyenyekevu tu unaweza kupata ukweli na ukweli ndio msingi wa upendo ambao hatimaye kila kitu kinatoka humo”. Papa Benedikto XVI, aliyeitwa Joseph Ratzinger alizaliwa huko Marktl am Inn, Jimbo kuu la Passau Ujerumani mnamo tarehe 16 Aprili 1927. Mnamo tarehe 29 Juni 1951 alipewa Daraja Takatifu ya Upadre pamoja na kaka yake mkubwa Georg na Julai 8 akaadhimisha misa yake ya kwanza. Baada ya kufundisha taalimungu kwa miaka ishirini na mitano katika vyuo vikuu vingi vya Ujerumani na kuanzisha jarida la kimataifa la taalimungu ya Umoja pamoja na Hans Urs von Balthasar, Henri de Lubac na wataalimungu wengine, mnamo tarehe 25 Machi 1977 aliteuliwa kuwa askofu mkuu wa Munich na Freising. Mnamo tarehe 27 Juni mwaka huo huo, aliteuliwa kuwa Kardinali na Papa Paulo VI. Mnamo tarehe 25 Novemba 1981, Mtakatifu Yohane Paulo II II alimteua kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. Na mnamo tarehe 19 Aprili 2005 alichaguliwa kuwa Papa na akachukua nafasi ya Mtakatifu Yohane Paulo II, ambaye alikufa mnamo tarehe 2 Aprili 2,005 , na ndipo akachagua jina jipya la Benedikto XVI.
Kwa hakika ilikuwa ni jambo la kushangaza ulimwengu mzima ambapo mnamo tarehe 11 Februari 2013 alipotangaza kujiuzulu! Kwani watu wengi na kwa karne nyingi hawakuzoea kusika Papa anajiuzulua japokuwa ilikuwa imeshatokea. Baada ya kuchaguliwa kwa Papa Francisko kama Papa mtawala mnamo tarehe 13 Machi 2013, Hayati Papa Mstaafu Benedikto XVI, alichagua kubaki katika monasteri ya “Mater Ecclesiae”katikaa Bustani mjini Vatican, ambako alikufa kwa amani mnamo tarehe 31 Desemba 2022 majaira ya asubuhi. Amezikwa kwa heshima zote za kipapa mnamo tarehe 5 Januari 2023 katika groto za Chini ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, mara baada ya misa ya mazishi iliyoongozwa na Papa Mtawala Francisko katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican kwa kuudhuliwa na waamini kutoka pande zote za dunia, viongozi wa kidini na kisiasa lakini pia na hata baadhi ya wafalme wa mataifa.