Ukraine,Krajewski:lori jingine la msaada limekwenda Zaporizhzhia
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Kitovu cha mshikamano ni nafasi za parokia ya Mtakatifu Sofia, Kanisa la Kigiriki-Katoliki jijini Roma ambapo wanaume wapatao ishirini, lakini pia waseminari na watu wengine wanaojitolea, wengi wao wakiwa Waukraine, waliaanza kupakia lori kila kona. Hilo Gari kubwa, la taifa wa Slovakia, ambalo liliondoka kuelekea eneo la Zaporizhzhia, moja ya vitovu vya vita nchini Ukraine, lililopigwa kwa miezi kadhaa na mabomu ya Urussi.
Habari hiyo ilitolewa na Kadinali Konrad Krajewski, ambaye siku chache kabla ya Noeli alikuwa ameendesha gari tena kupeleka jenereta arobaini na sehemu kubwa ya Masweta maalumu ya joto zilizokusanywa na Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo kupitia jukwaa la kuunga mkono. Na utiririshaji wa michango haujakoma, huku zaidi ya euro 300,000 zikiongeza zile ambazo zimewezesha kuongeza idadi ya jenereta na mavazi ya joto kutumwa huko Ulaya mashariki. Kwa mujibu wa Mwakilishi wa Kipapa alisisitiza kuwa nyenzo zote mpya zitapelekwa kwa wale watu wengi sana ambao wanaishi katika mazingira ya kinyama katika ukatili uliosababishwa na wakatili katika kipindi cha halijoto, hata kwa sasa katika baridi kali.
Mshikamano miongoni mwa wananchi
Kardinali akizungumza na vyombo vya habari Vatican alisema kuwa kiukweli umekuwa ni mlolongo wa wema wa watu wanaosaidia wananchi wenzao, wanaotaka kuwasaidia wale wanaoteseka. Mnamo tarehe 19 Desemba iliyopita, Kadinali huyo aliwasili Lviv na gari kubwa ambalo angeweza kuendesha na baada ya kusambaza misaada katika maeneo mbalimbali katika mji mkuu wa Kyiv, alihamia Kyiv kupelekea sehemu ya misaada na pia kusherehekea Noeli akiambatanisha pia na ukaribu na baraka za Baba Mtakatifu Francisko. Ilikuwa ni Noeli ya wakati wa vita, iliyotengenezwa kwa barafu na mwanga hafifu kutokana na mgao wa umeme uliopunguzwa na mwanga unaowashwa na jenereta. Kardinali Krajewski aliporejea wakati ule alisema kuwa ni kama utume kutimilika, lakini sasa baada ya siku chache pia amebainisha kuwa utume bado unaendelea kufanywa kwa upya!