Tafuta

2023.01.01 Mwili wa Papa Benedikto XVI ukiwa umelazwa kwenye kikanisa cha nyumba ya Mater Ecclesiae. 2023.01.01 Mwili wa Papa Benedikto XVI ukiwa umelazwa kwenye kikanisa cha nyumba ya Mater Ecclesiae.  (Vatican Media)

Uhusiano wa Ratzinger na Mt.Augustino:Mwongozo wa maisha,mtaalimungu&mchungaji

Papa mstaafu alikutana na Baba wa Kanisa wakati wakati masomo yake ya falsafa na taalimungu na alivutiwa naye.Tasnifu yake ya taalimungu imepata mwamko wa Waraka wa “Deus caritas est”.Papa Benedikto XVI alichagua ishara ya Agostino katika nembo ya Upapa na katika Kanisa la Mater Ecclesiae,kuna sanamu ya Askofu wa Hippo.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Papa Benedikto XVI na Mtakatifu Augostino. Wazo na taalimungu ya mrithi wa 264 wa Petro umejaa mafundisho na maandishi ya Baba wa Kanisa, lakini Joseph Ratzinger tayari akiwa kama mwanafunzi alihisi juu ya uhusiano na utu wa askofu wa Hippo. Alikuza  kwa namna ya pekee ya ibada ya kujitolea na shukrani kwa mtu huyo ambaye alihisi kuwa karibu naye sana katika sehemu ambayo alikuwa amepitia katika maisha yake kama mtaalimungu, kuhani na mchungaji. Alisema hayo mara kadhaa katika kipindi chake cha Upapa. Katika moja ya katekesi yake ya mwisho kati ya tano alizojikita nazo  kati ya Januari na Februari 2008, katika mzunguko wakati  katekesi za kila Jumatano alizungumzia juu ya Mababa wa Kanisa, mbele ya kaburi la Mtakatifu Augotino huko Pavia, mnamo Aprili mwaka huo huo, na kabla ya hapo kwa wanafunzi wa Seminari Kuu ya Roma mnamo tarehe 17 Februari 2007. Katika kipindi cha masomo yake ya kwanza ya falsafa na taalimungu katika nusu ya pili ya miaka ya 1940, alivutiwa sana na sura ya Mtakatifu Augustino na kwa safari yake ya ndani yenye shida iliyochukuliwa kuamini na kuelewa na wakati huo huo kuelewa na kuamini, kwa ufupi, kufanya mazungumzo ya imani na sababu zake. Mazungumzo ambayo Ratzinger aliendeleza na kukuza katika maisha yake yote.

Akiwaeleza waseminari  Papa Benedikito alisema: “Kwangu mimi Mtakatifu Agostino  ana ubinadamu mkuu uliovutia zaidi ya yote kwa sababu Yeye hakuwa na nafasi ya kujitambulisha na Kanisa kwa sababu alikuwa katekumeni tangu mwanzo, lakini ambapo badala yake alipambana kiroho ili kupata hatua kwa hatua Neno la Mungu”, hadi kufikia kusema ndio kwa Kanisa lake”. Na ni, hasa, historia ya kibinafsi ya mwanafalsafa wa Tagaste ambayo iliamgusa Ratzinger, ile njia ya kibinadamu, ambapo alisema kuwa hata leo tunaweza kuona jinsi tunavyoanza kuwasiliana na Mungu, jinsi upinzani wote wa asili yetu unapaswa kuwa, kwa kuchukuliwa kwa uzito na kisha lazima pia waelekezwe kufika kwenye ndiyo kuu kwa Bwana. Kwa njia hiyo taalimungu yake ya kibinafsi ilimvutia na, iliyokuzwa zaidi ya yote katika mahubiri yake.

Tukirudi nyuma, katika kazi ya Ratzinger kama msomi, mtaalimungu na mchungaji na katika maisha yake ya kibinafsi, sura ya askofu wa Hippo iko kila wakati. Ni pamoja na tasnifu juu ya uhusiano kati ya watu na Mungu katika Mafundisho ya Kanisa katika Agostino (People and House of God in the Doctrine of the Church of Saint Augustine) ambapo  mnamo mwaka 1953 Joseph Ratzinger  ambaye alikuwa tayari kuhani na kipaji cha kitaaluma, kuanzia kile ambacho Mwalimu wa Kanisa aliandika katika “Tafakari juu ya Zaburi 149” ana shahada ya taalimungu kutoka Chuo Kikuu cha Munich. Thesisi au Tasnifu hiyo ilichapishwa na katika utangulizi wa toleo la Kiitaliano la mnamo 1978, Ratzinger alielezea matokeo makuu ya utafiti wake, akibainisha kwamba “Usomaji upya wa Kikristo wa Agano la Kale na maisha ya kisakramenti yanayozingatia Ekaristi ni mambo mawili makuu katika Agano la Kale na maono ya Augostino ya Kanisa.”

Lakini kuna muktadha mwingine wa maisha ya Mtakatifu Augustino ambapo Benedikto XVI alitaka kusisitiza wakati wa ziara yake katika Seminari Kuu ya Roma wakati wa sikukuu ya Mama yetu wa Tumaini kuhusu  shauku yake ya kuishi, maisha ya kutafakari tu, na hivyo aliandika vitabu vingine vya falsafa…, lakini Bwana hakumtaka, alimfanya kuhani na askofu na kwa hivyo maisha yake yote, ya kazi yake, yalikuzwa kwa kiasi kikubwa katika mazungumzo na watu rahisi sana. Kwa upande mmoja, kila mara ilimbidi kutafuta maana ya Maandiko binafsi na, kwa upande mwingine, kutilia maanani uwezo wa watu hawa, muktadha wao muhimu, na kufika kwenye uhalisia na wakati huo huo Ukristo wa kina sana. Ilikuwa ni kitu kile kile ambacho Papa Ratzinger alitaka,  kustaafu kutoka katika maisha ya umma ili kujitolea kutafakari na kusali. Akiwa Mwenyekiti wa zamani wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa tangu 1981, alirudia mara kadhaa kumuomba hata  kung’atuka  kwa Yohane  Paulo II ambaye hakukubali.

Papa aliyechaguliwa tarehe 16 Aprili 2005, miezi michache baadaye, katika Siku ya ya Kuzaliwa kwa Bwana   Papa Benedikto XVI aliweza kukabidhi kwa Kanisa Waraka wake wa kitume wa  kwanza, Deus caritas est, ambao ulijikita katika  upendo wa Kikristo. Bado hata katika hilo ni Mtakatifu Augustino aliyemtia moyo. Shauku yake ya “kuzungumza juu ya upendo ambao Mungu hutujaza nao na ambao ni lazima tuwasiliane na wengine”, unafafanua katika mjadala uliogawanywa katika sehemu mbili kuu “zilizounganishwa kwa kina”. Ya kwanza yenye asili ya kubahatisha zaidi, ambayo alitaka kufafanua, mwanzoni mwa Upapa wake, takwimu muhimu juu ya upendo ambao Mungu, kwa njia ya ajabu na isiyo ya kawaida, anampatia mwanadamu, pamoja na kifungo cha ndani cha upendo huo. Upendo na ukweli wa upendo wa kibinadamu; sehemu ya pili yenye tabia thabiti zaidi, ambayo inahusu mazoezi ya kikanisa ya amri ya upendo kwa jirani”. Katika aya iliyotangulia hitimisho, Papa Benedikto katika waraka wake alitaka kuhakiki kwamba mchanganyiko wa dhana ya upendo, nuru pekee mbayo daima huangazia ulimwengu wa giza upya na kutupati ujasiri wa kuishi na kutenda. Upendo unawezekana na tunaweza kuufanya kwa sababu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu. Upendo unaoishi na kwa njia hii kuruhusu nuru ya Mungu iingie ulimwenguni."

Mnamo tarehe 22 Aprili 2007, alipokuwa aziara huko  Pavia, Papa Benedikto XVI alifafanua zaidi jinsi alivyokuwa karibu na Mtakatifu Augustino. Kwa hisia kali, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu  Pietro huko Ciel d'Oro, ambapo mabaki ya Mwalimu wa neema yanahifadhiwa, alifunua wazi kwamba ilikuwa nia yake kumweheshimu: “Kuonesha heshima ya Wakatoliki wote. Mmoja wa Mababa wake wakuu, iwe kwa ibada yangu  binafsi na shukrani kwa yule aliyeshiriki sehemu kubwa katika maisha yangu kama mtaalimungu na mchungaji, lakini ningesema kwanza kabisa kama mwanadamu na kuhani.” Na mbele ya kaburi la askofu wa Hippo, Papa Ratzinger pia alitaka kukabidhi kwa  Kanisa na kwa ulimwengu wote “Waraka wake wa kwanza  “akiwa na deni kubwa kwa wazo la Mtakatifu Augustino, ambaye alikuwa upendo na Upendo wa Mungu, na aliimba juu yake, akitafakari juu yake, alihubiri katika maandishi yake yote, na zaidi ya yote alishuhudia katika huduma yake ya kichungaji.”

Na pia alithibitisha  kwamba “ubinadamu wa kisasa unahitaji ujumbe huu muhimu, aliyefanyika mwili katika Kristo Yesu: Mungu ni upendo na kwamba kila kitu lazima kianze kutoka hapo na kila kitu lazima kielekee hapo: kila tendo la kichungaji, kila shughuli za kitaalimungu  na kwamba karimu zote hupoteza maana na thamani yao bila upendo, shukrani ambayo badala yake kila mtu anachangia katika kuujenga Mwili wa Fumbo wa Kristo. Papa Benedikito XVI aliongeza kuwa ujumbe “ambao Mtakatifu Augustino bado anaurudia kusema kwa Kanisa zima leo hii ni kwamba Upendo ni roho ya maisha ya Kanisa na matendo yake ya kichungaji”. Na haipaswi kusahau kwamba kwa moto wake wa Kipapa, Papa Benedikto XVI alichagua, kati ya alama nyingine, Ganda la Konokono, pia yenye maana ya Augustino. Hiyo kwa hakika, inamkumbuka maadiko fulani ambayo mhusika wake mkuu ni mwanafalsafa wa Tagaste.

Inasemekana kuwa Agostino, alipomwona mtoto kwenye ufuo wa bahari akiendelea kuchota maji baharini kwa ganda na kisha kuyamwaga kwenye shimo lililochimbwa kwenye mchanga, aliuliza ufafanuzi. Kijana akajibu anataka kuweka maji yote ya bahari kwenye shimo hilo. “Augustino alielewa juu ya juhudi zake ni za bure na zisizo na maana za kujaribu kutafuta  ukomo wa Mungu katika akili yenye mipaka ya mwanadamu. Na maelezo yameandikwa kwenye ukurasa ambao tovuti ya Vatican.va imefafanua zaidi juu ya  nembo Upapa wa  Benedikto XVI. Historia hiyo ina ishara dhahiri ya kiroho, kwa kutoa mwaliko wa kumjua Mungu, ingawa kwa unyenyekevu wa uwezo duni wa kibinadamu, kwa kuzingatia kutokamilika kwa mafundisho ya kitaalimungu.

Inashangaza kwamba katika Kikanisa cha Monasteri ya Mater Ecclesiae, katika bustani ya Vatican, ambapo mwili wa Benedikto XVI ulikuwa umelazwa na  kuruhusu kutolewa heshima kwa marafiki zake wa karibu, makadinali, maaskofu, walei, marafiki, washirika wa zamani, wanafunzi , familia, watawa wa kike na kiume, pia kulikuwa na sanamu ya Mtakatifu Augustino. Iliwezekana kuonekana mbele ya Altare. Ni simulacrum ya kale ya mbao ambayo inaonesha ishara za wakati; askofu wa Hippo anawakilishwa na mavazi ya kikuhani. Hakuna shaka kwamba yeye ni baba mkuu wa Kanisa, karibu naye ni mtoto ameshika ganda. Hata hivyo walio mstari wa mbele wa fundisho la Agostini ambalo Papa Benedikto XVI alipendea kuliweka katika Nembo yake na ganda, na ambalo luoko katika nembo ya zamani katika Monasteri ya Schotten, huko Ratisbon, ambapo Josepg Ratzinger alihisi kushukamana sana kiroho na nazidi ni ishara ya muhujaji. Na ni hsa mahali ambapo mhujaji wa dunia wa Benedikto XVI alihitimisha, Mtakatifu Agostino utafikiri shuhuda kwa kule ambacho Joseph Ratzinger alizawadia ulimwengu.

Uhusiano wa Benedikto XVI na Mt. Agostino
03 January 2023, 15:07