Tafuta

2023.01.21 Papa amekutana na Wajumbe wa Umoja wa Kitaifa wa walipata ulemavu wakati wa huduma ya kitaifa. 2023.01.21 Papa amekutana na Wajumbe wa Umoja wa Kitaifa wa walipata ulemavu wakati wa huduma ya kitaifa.   (Vatican Media)

Papa:vita ni jinamizi na epuka vurugu yoyote,hata uchongezi unaua

Baba amekutana na Wanachama wa Muungano wa Kitaifa Italia waliopata ulemavu wakiwa katika Huduma.Ni shirika la kuwalinda wale ambao wanateseka kutokana na ukatwaji wa viungo na ulemavu kutokana na utumishi wa kijeshi na kiraia.Kwao amesema wana moyo wa nguvu ya amani katika jamii,kusaidia kutatua migogoro kwa amani na kutoa tahadhari kwa wasiolindwa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 21 Januari 2023, amekutana mjini Vatican na wanachama wa Muungano wa Kitaifa wa waliopata ulemavu wakiwa katika Huduma, ambalo ni shirika la kuwalinda wale ambao wanateseka kutokana na ukatwaji wa viungo na ulemavu huo wakati wa  utumishi wa kijeshi na kiraia. Katika hotuba yake amebainisha kuhusu hali ya kutisha ya matukio ya sasa na kujitolea kwa maisha ya kila siku. Papa Francisko amesema: “Ndiyo, kuna maombi, chombo chenye nguvu, lakini tunakabiliwa na vita ambayo inaonekana kama jinamizi lisiloweza kushindwa. Je ni  nini kingine tunaweza kufanya? Tunaweza kujaribu, katika maisha ya kila siku, kukabiliana na migogoro kwa kuepuka vurugu na ukandamizaji wote, hata kwa maneno."

Inahitahijika maombi sana

Katika hotuba yake  ni kwa hao wanachama wa Muungano wa Kitaifa wa Waliokatwa kwa ajili ya Huduma na ambalo ni shirika lisilo la kiserikali jijini Romlakini pia limeea Italia nzima linajikitakuwalinda na kuwatetea wale ambao wallikatwa moja au zaidi ya viungo vyao na na kuwa udhaifu wakiwa katika huduma na wajibu wao,  kwenye  utumishi wa kijeshi na raia. Kwa maana hiyo hawa ni wanachama wanajeshi, maafisa wa polisi, wafadhili, maafisa wa polisi wa magereza, askari wa misitu, wazima moto na wengine ambao wanachama ambao wako katika aina hiyo ya ulinzi wa kiraia katika Nchi. Walikuwa Jumla ya watu 200 katika ukumbi wa Clementina mjini Vatican,  ambao Papa Francisko aliwashukuru awali ya yote kwa zawadi ya msalaba wenye sura ya Mchungaji Mwema, iliyoundwa maalum kwa ajili ya tukio hilo, lakini zaidi ya yote kwa msaada wao katika sala.  Papa amesema "Kiukweli, ninahitaji, kwani kazi hii sio rahisi. Asante kwa maombi yenu. Hii ndio zawadi bora zaidi ambayo mnaweza kunipatia.”

Kuwa wajenzi wa amani

Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza juu ya ahadi ya chama kwa ajili ya amani, kwamba anajua jinsi ambavyo kwa baadhi yao wana sababu ya kutokuwa na halali inahusishwa hasa na utume wa  amani, au na utimilifu wa huduma kwa utaratibu wa umma na uhalali. Hili kwa hakika linaboresha urithi wa maadili wa Muungano, lakini pia dhamira ya kuwa wapatanishi inatumika kwa kila mtu, bila kujali historia ya kila mtu.

Uchongezi unaua

Katika ulimwengu huu uliojeruhiwa na migogoro, kwa hiyo Papa Fransisko ametoa mwaliko wa kujenga amani kuanzia ishara ndogo za kila siku. Kama ile ya kuepuka vurugu, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa matusi. Papa amesema; “Na si rahisi! Kwa sababu wakati fulani neno linatosha tu kumuumiza au kumuua kaka au dada. Hebu tufikirie umbea, ambao ni kawaida sana, hapa tulipo, kati yetu... Badala yake hatupaswi kufanya hivyo" na kwamba ana uhakika "labda wao hawafanyi japokuwa ni  sehemu zingine ... uvumi ambao ni mkate wa kila siku. Na unaumiza sana, na unaharibu".

Kutoa hisia za kijamii kwa wale ambao wameishi uzoefu mbaya

Umoja wa Kitaifa wa Watu Waliokatwa viungi  kwa kwa sababu ya  Huduma unaweza na lazima uwe nguvu ya amani katika jamii, kusaidia kutatua migogoro kwa amani, kutafuta manufaa ya wote na kuvutia wale ambao hawajalindwa, alihimisa Papa. Wao pamoja na ukweli mwingine kama huo, wanaweza kutoa hisia za kijamii kwa kile, ambacho wao kibinafsi, kimekuwa uzoefu mbaya, kizuizi kilichowatesa katika hali ambazo ni tofauti kwa kila mmoja. Kwa Papa pande wa amesema , hiki ni kipengele cha thamani kubwa ya kimaadili na kiroho. Kila mtu anaalikwa kuondokana na tabia ya kujifungia mwenyewe, katika hali yake mwenyewe, kufungua mkutano, kushirikiana na mshikamano. Na hii inaweza kuleta mabadiliko makubwa, unajua vizuri.

Nguvu ya  upendo

Papa Francisko, amesisitiza kuwa ni kweli, kikomo, uzito wa kubeba unabakia sawa, haupotei, hata hivyo unapokea maana tofauti, maana chanya: mbele ya hali yao, badala kujishusha inakuwa ishara ya juu  zaidi. Na hili linaweza kufanyika kwa pamoja, kwa sababu tunasaidiana. Zaidi ya yote, inawezekana kufanya hivyo pamoja na Yesu Kristo, ambaye kwa uwezo wa upendo wa Mungu aligeuza uovu kuwa wema, si kwa udhahiri, kwa nadharia, bali ndani yake mwenyewe, katika uzoefu wake binafsi, katika maisha yake, na mwili wake. Nguvu hiyo hiyo ndiyo matakwa ambayo Baba Mtakatifu amewatakia kila mmoja wa washiriki wa Umoja huo na kwamba Bwana awape nguvu ya kusaidia watu wengi kuweka ishara ya juu zaidi katika hali yao ngumu.

Papa na wahanga wa kijeshi
21 January 2023, 15:55