Papa Mstaafu Benedikto amegusa maisha ya watu wengi:‘Baba na kiongozi’
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Ilikuwa tayari katika mapambazuko ya kwanza ya Jumatatu tarehe 2 Januari 2023 waamini wengi sana waliwasili katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, mjini Vatican huku wakisubiri ufunguzi saa 3.00 kamili wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro ili kutoa heshima zao za mwisho kwa Baba Mtakatifu Mstaafu. Walei, mapadre, watawa kike na kiume, vijana wengi kutoka sehemu mbali mbali za dunia ambao wamemtambua Papa Benedikto XVI kuwa baba na kiongozi. Katika uwanja kuna watawa wengi na wengine wa kigeni, lakini pia wanaokaa katika taasisi mbali mbali za Roma; familia nyingi pia kutoka sehemu mbali mbali wanaendelea kufika. Lakini alfari walikuwa wa kwanza kwenye mstari, tayari kwenye uwanja kuanzia saa 11.30 alfajiri na mapema, aidha kikundi cha wanafunzi wa Taalimungu wa Kihindi waliomtaja Papa Mstaafu Benedikto kama ‘taa ya Kanisa’.
Kwa upande wa mwamini mmoja wa Roma akihojiwa na mwandikishi wa habari alisema jinsi ambavyo Papa Mstaafu alivyo kuwa mwalimu na mchaungaji, na hivyo ni vema sana kumtambua kutoa heshima ya mwisho. “Alitufundisha jinsi ya kuamini na jinsi gani upendo wa Mungu ulivyo kwa watoto wake”, kwa mujibu wa maelezo ya mwanamke mmoja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Wengi wa waamini wamemkumbuka Papa mstaafu juu ya jukumu lake kama msomi na mtaalimungu. “Benedikto ni baba, awali ya yote, ni jambo dogo kusema alikuwa mtu mwenye akili na utamaduni tu”, alieleza Padre Andrea, wa parokia moja ya mji mkuu wa Roma. Kwa maana hiyo “Alikuwa mtu wa Mungu na alitufundisha kiukweli kufikiri kama Wakristo. Ni mtu wa Mungu mwenye hekima na mtu hawezi kukosa kwenda kumuaga”.
Hata hivyo kulikuwa na maoni mengine yanahosiana na maisha binafsi ya watu Papa Mstaafu ambayo yanagusa sana watu wengi. Kuna mwingine alisema, kwake yeye ni mtu muhimu kwa sababu anakumbuka siku aliyojuzulu ilikuwa sambamba na siku ya kifo cha baba yake na mama mkwe wake. Kwa hiyo katika yeye amesema sasa anamkosa mtu pole kama walivyokuwa ndugu zake, lakini amesema anamshukuru kwa kuwa alikuwa muhimu kwake kwa kumuimarisha kulifuata Kanisa. Na mtu mwingine pia amesema Papa mstaafu alikuwa mkuu, wa imani na daima alipenda wazo lake na katika maneno yake.
Kulikuwa na shukrani kubwa kutoka kwa watawa waliohudhuria hapo ambao wamekiri kupata msukumo wa uhakika katika wito wao kutoka kwa Papa Benedikto XVI. Kwa mfano Sr. Maria Caritas, aliyefika Roma kutoka Nebraska, nchini Marekani, alichagua jina lake wakati wa kufunga nadhiri akiongozwa na waraka wa Deus caritas est. Naye Padre Luca, kutoka Milano alisema: “Nilikuwa katika seminari alipochaguliwa kwa hivyo kumbukumbu yangu iko hai kabisa. Nimebaki na hisia za baba, mwalimu mkuu wa huruma isiyo na kikomo”. Na mwingine mtawa kutoka Brazil anayeishi Palermo amesema: “Tupo hapa kwa sababu yeye ni sehemu ya familia yetu. Nilimwona huko Marekani, Brazil, kisha Roma na kwa urahisi wake alikoleza wito wangu sana” .