Tafuta

2023.01.21  Papa Francisko amekutana na Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniana  "de Propaganda Fide" 2023.01.21 Papa Francisko amekutana na Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniana "de Propaganda Fide"  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa:wamisionari si kwa sababu ya mavazi bali urahisi na uaminifu!

Akizungumza na jumuiya ya Chuo Kikuu cha Kipapa la Urbaniana inayoundwa na wanafunzi na mapadre wanaopangiwa katika maeneo ya utume,amewaalika wanafanane na Yesu,wa kuaminika kwa maelewano yaliyojiri ndani yake kati ya kile alichokitangaza na kile alichofanya,kutoka nje ya nafsi yake kukutana na wengine na kufungua majadiliano.Ulimwengu na Kanisa vinahitaji mashuhuda wa udugu na amani.

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

Papa Francisko Jumamosi tarehe 21 Januari 2023, amekutana na Jumuiya nzima ya wanafunzi, walimu na wahudumu wa Chuo Kikuu cha Kipapa  la Urubaniana na amewakaribisha kwa shangwe huku akimshukuru Gambera kwa maneno yake na kuwasalimu wakufunzi na wanafunzi wote. Wakiwa wanafunzi wa Chuo cha Urbano,  wao ni  sehemu ya mkondo hai wa mapokeo tajiri na ya kale ambayo yalianza mnamo mwaka 1627, mwaka ambao Papa Urbano VIII aliamua kuanzisha seminari jijini Roma kwa ajili ya mafunzo ya makasisi kwa kile kinachoitwa  maeneo ya utume. Ilikuwa ari angavu muhimu, ambayo bado leo hii ina uhalali wake na ambayo wao wanaitwa kuipokea na kuitafsiri kwa njia ya ubunifu, kujiruhusu kuulizwa maswali na mahitaji na maswali mengi ya nyakati tunamoishi. Hakika, Kanisa zima leo hii limeitwa katika uongofu wa kichungaji na kimisionari" (Evangelii gaudium, 25), pia katika malezi ya mapadre wajao, na katika mtazamo huu unaweza kuwa msukumo na msaada kwa wengine wengi. Baba Mtakatifu amesema  kwamba mwaka huu, maadhimisho ya miaka mia nne tangu kuanza kwa Baraza la Propaganda Fide, katika mchakato wa safari yao unatafakari mada ya uhusiano hai na wa kibinafsi na Yesu kama chanzo cha kiroho cha kila utume  ukiongozwa na kauli mbiu: “ili wote wawe wamoja, kutumwa kuhubiri”. Kwa hivyo Papa amependa kutafakari kwa ufupi juu ya mada hiyo.

Wanafunzi wa Urbaniana na Papa
Wanafunzi wa Urbaniana na Papa

Tunaweza kujiuliza:ni sifa zipi muhimu zaidi za kutunza na kuimarisha wakati wa malezi ya awali, ili kuwa kweli wanafunzi-wamisionari karibu na Mungu na ndugu zake? ameuliza Papa.  Kipengele cha kwanza ambacho aliwependa kuweka wazini ujasiri wa uhalisi, ujasiri wa kuwa wa kweli. Kiukweli, ukaribu wetu pamoja na Mungu na kaka na dada zetu unatambuliwa na kuimarishwa kadiri tunavyokuwa na ujasiri wa kuvua barakoa, labda tuonekane kuwa wakamilifu, wasio na dosari na wenye heshima, au bora zaidi. Barakoa hazihitajiki, Papa amekazia mara mbili  kwa: “ndugu wapendwa, hazihitajiki! Wacha tujitambulishe kwa wengine bila barakoa, kwa jinsi sisi tulivyo na mipaka yetu na migongano, tukishinda hofu ya kuhukumiwa kwa sababu hatuendani na mfano bora, ambao mara nyingi huwa katika akili zetu tu”. “Hebu tukuze uwazi na unyenyekevu wa moyo, ambao hutupatia mtazamo mmoja juu ya uaminifu wetu,  udhaifu wa ndani na umaskini (Tafakari, Malaika wa bwana 23 Oktoba 2022). Tukumbuke kwamba sisi ni wamisionari wanaoaminika si kwa sababu ya mavazi tunayovaa au mitazamo ya nje, bali kwa sababu ya mtindo wa urahisi na uaminifu.

Papa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kipapa Urbanianana
Papa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kipapa Urbanianana

Huo ndio uwazi”, amekazia Papa Francisko. Kwa maana hiyo amesema uaminifu uliotambuliwa ndani ya Yesu na watu waliokutana naye (rej. Mk 1:22) ulitokana na maelewano ambayo yalionekana kwake kati ya kile alichotangaza na kile alichofanya. "Ni maelewano na  mshikamano". Kwa hiyo Papa amewaomba wasiogope kujionesha jinsi walivyo, hasa kwa wale kaka ambao Kanisa huweweka kando yao kama walezu. Wakati mwingine vishawishi vya urasmi vinaweza kuwapo au mvuto wa majukumu kana kwamba hii inaweza kukuhakikishia utambuzi kamili. Lakini amesema wasidanganyike na suluhishi hizo ambazo ni rahisi lakini ni za uwongo. Mtakatifu  John Henry Newman, mwanafunzi wa zamani wa chuo hicho akizungumzia uhalisi alionya dhidi ya tabia ya wale ambao wangependa kutenda kwa heshima na badala yake waliacha kuwa wao wenyewe. Hadhi lazima iwepo kutoka kwao wenyewe. Papa amependa kuwakumbusha kuhusu Mfarisayo, ambaye aliomba “mbele yake mwenyewe” na mtoza ushuru ambaye hata hakuwa na ujasiri wa kutazama juu, lakini alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule” (Lk 18:14).

Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniana wamekutana na Papa
Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniana wamekutana na Papa

Sifa ya pili ambayo Papa amependa kuikumbusha ni uwezo wa kutoka nje ya nafsi yao wenyewe. Maisha ya imani ni msafara"unaoendelea, kutoka katika mipango yetu ya kiakili, kutoka katika kizuizi cha hofu zetu, kutoka katika uhakika mdogo unaowahakikishia. "Vinginevyo tunahatarisha kumwabudu Mungu ambaye ni makadirio mahitaji yetu tu,  na kwa hivyo muungu na bila hata kukutana na watu wengine wa kweli. Badala yake, inatusaidia sisi kukubali hatari ya kutoka kwetu, kama walivyofanya Ibrahimu, Musa na wavuvi wa Galilaya walioitwa kumfuata Bwana (rej. Mk 1:16-20)" Papa ameshauri. Na wao wanayo fursa ya kuifanya hivyo sasa katika maisha ya jumuiya, hasa katika jumuiya ya malezi iliyo tajiri na tofauti kama yao, yenye tamaduni nyingi, lugha na hisia. Baba Mtakatifu amesema kuwa hiyo ni zawadi kubwa ambayo wanaweza kuimarishwa kiasi kwamba kila mmoja anaweza kuondoka kwenye ua lake ili kujifungulia kwa wengine, kwa ulimwengu wao na utamaduni wao. Kwa sababu hiyo, amewahimiza kuishi changamoto ya udugu bila woga, hata inapohitaji bidii na kujitoa.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Urbaniana
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Urbaniana

Ulimwengu wetu na pia hata Kanisa linahitaji mashuhuda wa udugu:, nahivyo ni maombi ya Papa kwamba na wao wanaweza kuwa hivyo hivyo mara kwa mara wakati wanarudi katika majimbo na nchi zao, ambazo mara nyingi hugunduliwa zina migawanyiko na migogoro. Na pia hata kuwa mashuda wa furaha kwa sababu  ni “ Furaha ya Injili inayojaza maisha ya jumuiya ya wanafunzi (Evangelii gaudium, 21); furaha ya kimisionari ambayo daima ina mienendo ya kutoka nje na ya zawadi. Kwa hiyo ni  furaha na zawadi”. Hatimaye, Papa amependa kusisitiza sifa moja muhimu ya kuwa mfuasi-mmisionari: ambapo inahitaji uwazi kwa ajili ya mazungumzo. Kwanza kabisa kufanya mazungumzo na Mungu, katika maombi, ambayo pia ni msafara kutoka katika nafsi yetu ili kumkaribisha, anaposema ndani yetu na kusikiliza sauti zetu. Na baadaye  kwa ajili ya mazungumzo ya kidugu, na  uwazi kwa wengine. Mtakatifu Yohane Paulo II alitufundisha kwamba mazungumzo lazima yawe mtindo ufaao wa mmisionari (Taz. Redemptoris missio, 55-56).

Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Kipapa ikimsikiliza Papa
Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Kipapa ikimsikiliza Papa

Baba Mtakatifu Francisko amesema kwamba "Yesu alituonesha sisi hayo kwa kujifanya mwanadamu, akakumbatia janga, maswali na matarajio ya wanadamu wanaoteseka katika kutafuta amani.  Kwa hiyo: “ Ndugu wapendwa, dunia inahitaji mazungumzo, inahitaji amani. Na inawahitaji wanaume na wanawake wenye kuishuhudia”. Baba Mtakatifu amewaomba wajiweke katika shule ya wale wafiadini wa mazungumzo ambao hata katika baadhi ya nchi zo wamesafiri kwa ujasiri barabara hiyo ili kuwa wajenzi wa amani. Wasiogope kuifuata hadi mwisho, wakienda kinyume na wimbi ili kumshirikisha Yesu, wakiwasilisha imani ambayo amewapatia (taz.Christus vivit, 176).  Kwa kuhitimisha amesema kwa maombezi ya Bikira Maria Mama yetu na wanafunzi wengi watakatifu na wenyeheri wa zamani wawasindikize  katika safari hiyo. Amewabariki kwa  moyo na amewaomba wasisahau  kusali kwa ajili yake.

Papa na Chuo Kikuu Urbaniana
21 January 2023, 14:33