Papa amemteua Padre Samuel Nkuah-Boateng kuwa Askofu wa jimbo Wiawso
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Alhamisi 26 Januari 20223 Baba Francisko amekubali maombi ya kung’atuka kutoka shughuli za kichungaji yalitolewa na skofu Joseph Francis Kweku Essien wa Jimbo la Wiawso, nchini Ghana,na wakati huo huo akamteua Padre Samuel Nkuah-Boateng, kuwa Askofu wa jimbo hilo na ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni msimamizi wa Kanisa Kuu la Wiawso. Padre Samuel Nkuah-Boateng alizaliwa tarehe 6 Mei 1968 huko Sefwi Bosomoiso. Baada ya majiundo ya seminari ndogo ya Mtakatifu Teresa huko Elmina, Jimbo Kuu la Cape Coast na Seminari Kuu ya Kanda ya Mtakatifu Pietro huko Cape Coast, aliendelea na mfunzo ya Sosholojia na Mafunzo ya Kidini katika Chuo Kikuu cha Ghana. Alipewa daraja la ukuhani mnamo tarehe 28 Julai 2001 kwa ajili ya jimbo la Wiawso.
Mhesh. Padre Samule alishikilia nyadhifa na kufanya masomo zaidi: Paroko wa parokia ya Mkingiwa dhambi ya asili, huko Enchi (2001-2003); katibu wa askofu wa Wiawso (2003-2008); Gambera wa Mtakatifu Maria huko Dwinase (2003-2009); Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Augustino Sefwi Boako (2009-2011); mkurugenzi wa Kituo cha Kichungaji na Malezi (2009-2018); msimamizi wa Kanisa kuu la Wiawso (2011-2018); rais wa chama cha mapadre wa jimbo (2012-2020); Masomo ya Uzamili katika Huduma ya Kichungaji na Elimu ya Dini katika Chuo Kikuu Katoliki, Ghana (2015-2017); Shahada za Uzamili katika Falsafa (2018-2020); tangu 2009, mwanachama wa Baraza la washauri na Baraza la Makleri; tangu 2020, Mkurugenzi wa Kituo cha Kichungaji na Malezi, Mratibu wa Tume ya Haki na Amani ya Jimbo na Msimamizi wa Kanisa Kuu la Wiawso.