Tafuta

2023.01.19:Kitabu chenye kichwa "Dio è sempre nuovo" yaani "Mungu daima ni mpya" kinahusu mafundisho makubwa ya Hayati Papa Mstaafu Benedikto XVI kuhusu imani ya kikristo. 2023.01.19:Kitabu chenye kichwa "Dio è sempre nuovo" yaani "Mungu daima ni mpya" kinahusu mafundisho makubwa ya Hayati Papa Mstaafu Benedikto XVI kuhusu imani ya kikristo. 

‘Mungu daima ni mpya’.Kina cha mawazo ya Joseph Ratzinger ni msaada kwetu!

“Mungu daima ni mpya”,ni kichwa cha Kitabu ambacho kinapendekeza antholojia kubwa ikizungukia mada msingi za imani ya kikristo katika maneno ya Hayati Papa Mstaafu Benedikito XVI.Utangulizi wa kitabu hicho ni wa Baba Mtakatifu Francisko ambaye anabanisha kwamba ni kuzama katika mawazo ya kiroho ya Joseph Ratzinger ambaye alifanya taalimungu kwa magoti.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Dibaji ya Papa Francisko katika kitabu chenye kichwa “Mungu daima ni mpya” kilicho haririwa na Luca Caruso, ambacho kimechapishwa kwenye  maduka ya vitabu mnamo Alhamisi tarehe  19 Januari 2023 kinatoa antholojia kubwa kuzungukia mada kuu za imani ya Kikristo katika maneno ya Hayati Papa Mstaafu Benedikto XVI. Papa Francisko, ambaye ametia saini ya utangulizi huo, ameelezea andiko hilo kama aina ya mchanganyiko wa kiroho wa maandishi ya Papa Benedikto XVI, kwa maana hiyo amebainisha kwamba: “hapa kunaangaza uwezo wake wa kuonesha upya undani wa imani ya Kikristo”.

Mawazo ya Mtaalimungu na mchungaji Papa 

Kitabu hicho kinamzamisha msomaji katika mawazo ya mtaalimungu na mchungaji Papa ambaye, mwanzoni mwa upapa wake, alijiwasilisha kwa ulimwengu mnamo tarehe 19 Aprili 2005, kama mfanyakazi mnyenyekevu katika shamba la mizabibu la Bwana na ambaye, akijiachia kabisa kwa Mungu, siku zote alisitawisha uhitaji wa kweli kwa kukazia uhusiano mkubwa kati ya imani na sababu. Kupitia sura tisa za kitabu kuhusu Mungu na Yesu, juu ya imani, upendo, sala, vijana na familia, matumaini, utakatifu, ukweli na uhuru na furaha, Papa  Benedikto XVI anachora uzuri wa Ukristo kwa mawazo safi na mwenye bidii ambaye anahoji uhusiano wake na Mungu tukio la upendo ambalo huangazia usiku wa giza zaidi.

Mungu lazima atafutwe na kusikilizwa

Baba Mtakatifu Francisko anaandika kwamba Mungu lazima atafutwe na kusikilizwa, kama alivyoeleza Papa Benedikto wa kumi na sita katika kitabu hicho, ambacho ni kwa jamii zetu. Hili linaonekana kwake kuwa hitaji la kwanza, anakiri  Papa kwamba , Mungu awepo tena katika maisha yetu, kwamba tusiishi kana kwamba tunajitawala, na  tumepewa mamlaka ya kubuni uhuru na nini maana maisha”. “Mungu anakipenda kiumbe chake, mwanadamu; anampenda hata katika anguko lake na hamwachi peke yake. Anapenda hadi mwisho.” Papa Francisko ameandika katika utangulizi kwamba  “Mawazo ya kinana ya Joseph Ratzinger, ambayo yalitegemea Maandiko Matakatifu na Mababa wa Kanisa, bado yana msaada kwetu leo na anamtakia kila msomaji kupata katika kurasa hizo, zilizopitishwa na sauti ya shauku na upole wa mwalimu wa imani na matumaini, neema ya kukutana na Yesu mpya na yenye kuleta uzima.

 

20 January 2023, 09:17