Tafuta

Papa anawalika viongozi wa Curia Romana na Wakuu wa Mabaraza ya Kipapa kujikita katika sala za kibinafasi kuanzia tarehe 26 Februari hadi 3 Machi 2023 kwa maandalizi ya Kwarezima. Papa anawalika viongozi wa Curia Romana na Wakuu wa Mabaraza ya Kipapa kujikita katika sala za kibinafasi kuanzia tarehe 26 Februari hadi 3 Machi 2023 kwa maandalizi ya Kwarezima.  (Vatican Media)

Mafungo ya Kiroho,Papa anaalika Curia Romana kuishi kwa namna ya kibinafsi

Hata mwaka huu uteuzi wa kiutamaduni wa Kwaresima hautafanyika katika Nyumba ya Divin Maestro huko Ariccia.Badala yake Papa Francisko anawaomba washirika kujikita wao binafsi katika maombi kuanzia tarehe 26 Februari hadi Machi 3 na kusimamisha kazi.Wakati huo huo,shughuli za kipapa pia zitasimama ikiwemo Katekesi yake Jumatano Mosi Machi 2023.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Kama ilivyokuwa mwaka 2022, pia kwa kipindi cha Kwaresima mwaka huu Papa Francis amewaomba Makardinali wanaoishi Roma, wakuu wa Mabaraza ya Kipapa na wakuu wa Curia Romana “kupitia kipindi cha Mafungo  ya Kiroho kwa njia ya kibinafsi, kusimamisha kazi na kujiumba katika sala kuanzia alasiri ya Dominika  26 Februari hadi alasiri ya Ijumaa 3 Machi 2023”,  katika juma la kwanza la Kwaresima kipindi cha maandalizi ya Pasaka. Ni Taarifa iliyotoka katika Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, ambayo pia inaarifu kwamba shughuli zote za  Papa zitasitishwa katika juma hilo, ikiwa ni pamoja na Katekesi yake ya  siku ya Jumatano tarehe 1 Machi 2023.

Tangu mwanzo wa upapa wake, Papa Francisko alichagua Nyumba ya Divin Maestro inayoendeshwa na Watawa wa Paulini huko Ariccia kama mahali pa kurejea pamoja kwenye Mafungo ya kiroho na Curia Romana. Janga la UVIKO -19 liliweka ugumu wa uteuzi wa Kwaresima katika miaka miwili iliyopita. Pia mwaka 2022 kwa sababu ya kuendelea kwa dharura hiyo hiyo ambapo haikuwezekana kufanya Mafungo huko. Wakati wa sala ya Malaika wa Bwana mnamo tarehe 6 Machi Papa alikuwa amewaomba  waamini kuwasindikiza kiroho Wajumbe wote wa Curia Romana katika siku ambazo  alizifafanua kwamba "wanabeba sala zao kwa mahitaji yote ya Kanisa na ya familia ya kibinadamu".

Mafungo Binafsi ya kiroho 26 Feb hadi 3 Machi 2023
20 January 2023, 15:41