Tafuta

2023.01.02 Moja ya Kumbu kumbu zake Kardinali Krajewski. 2023.01.02 Moja ya Kumbu kumbu zake Kardinali Krajewski. 

Krajewski:Benedikto alikuwa na busara,mkarimu&alitusikiliza

Mkuu wa Sadaka ya Kipapa anamkumbuka Papa Mstaafu Benedikto XVI wakati alipokuwa sehemu ya waandaaji wa Sherehe za Kipapa katika miaka ya upapa wake,kwa mujibu wake alisema kuwa "Ni Mtaalimungu mkuu na mwenye ubinadamu sana".

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Ilikuwa ni mnamo tarehe 19 Aprili 2005, wakati dunia nzima ilikuwa inatazamia kupokea  Baraka na  kukutana na Papa mpya. Moshi mweupe kutoka katika kikanisa cha Sistine ulitangaza uchaguzi wa makadinali ambao, katika kura ya nne, walimchagua mrithi wa Papa Yohane  Paulo II. Picha baadaye zilionesha madirisha ya vioo vya rangi yakifunguliwa na Kadinali Jorge Medina Estévez akitamka jina la Joseph Ratzinger, Papa Benedikto XVI. Kwenye Balkoni  alionekana mmoja wa washereheshaji wa kipapa Kardinali wa baadaye Konrad Krajewski mikononi mwake akiwa na msalaba ametangulia na nyumba kufuata Papa mpya!

Siku ya Kuchaguliwa kwa Papa Benedikto XVI mnamo tarehe 19 Aprili 2005
Siku ya Kuchaguliwa kwa Papa Benedikto XVI mnamo tarehe 19 Aprili 2005

Katika mahojiano hayo Kardinali Krajewski ameeleza kuwa “ilikuwa wakati hisia kali sana katika maisha yangu , kwani nilikuwa katika nyumba ya Papa wakati, Papa Yohane Paulo II alipofariki, moja ya nyakati ngumu na kina. Kardinali Krajewski alikumbusha  juu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Papa mpya  hasa kujikabidhi chini ya mikono ya makadinali, maandalizi ya mazishi ya Papa ambaye alimthamini sana kwa juhudi zake na kujitolea kwake katika kuandaa Misa iliyoadhimishwa huko Łódz, mji alikozaliwa Kardinali, wakati wa ziara ya tatu ya Papa Yohane Paulo II nchini  Poland mnamo mwaka 1987. Wakati huo Krajewski alikuwa ni mseminari tu.

Siku ambayo alichaguliwa Papa Benedikto XVI mnamo 19.04 2005
Siku ambayo alichaguliwa Papa Benedikto XVI mnamo 19.04 2005

Kwa moyo uliojaribiwa lakini kwa kumpoteza Papa mpendwa, alisema kuwa alijiweka chini ya Monsinyo Piero Marini, Mshereheshaji mkuu wa maadhimisho ya kiliturujia ya kipapa wa wakati ule. “Wakati Kadinali Ratzinger alipochaguliwa, pale katika Kikanisa cha Sistine, Monsinyo Marini alimwambia kwamba alipaswa kubeba msalaba wa maandamano mbele ya Baba Mtakatifu. 'Wanapofungua mapazia alipaswa atoke yeye kwanza na baadaye kufuatia  Papa pamoja na mshereheshaji. Kardinali Krajewski alitabasamu akifikiria wakati huo kwa sababu alikumbuka hisia za kuona Uwanja wa Mtakatifu Petro ukiwa umefurika watu. “Baba Mtakatifu kisha akahutubia maneno tunayojua kwa kila mtu. Nilifuata miaka 8 ya upapa wake kama msimamizi wa sherehe. Nilifanya safari nyingi, sherehe zote huko Roma, nchini Italia”.

Ziara ya Papa Benedikito XVI huko Aquila Italia 28 .04.2009
Ziara ya Papa Benedikito XVI huko Aquila Italia 28 .04.2009

Kuna mambo kadhaa yanayohusu nafsi ya Papa Mstaafu ambayo yamebaki kuchapishwa ndani ya moyo wa  Kardinali Krajewski. “ Kile ninachokumbuka  ni fadhili zake kubwa za ukarimu na urahisi wake. Tulikuwa vijana, nilikuwa mdogo kwa umri lakini Baba Mtakatifu hakuwahi kutuita ki urahisi tu bali kwa heshima na  alikuwa mkarimu sana. Alikuwa amependezwa na jina langu la Konrad ambalo ni la Kijerumani zaidi kuliko la Kipoland, kwa hiyo mama yangu alipofariki aliniuliza ilikuwaje, alikuwa na umri gani. Alikuwa rahisi sana, na ukaribu wa kifamilia, maridadi sana." Nimebeba sura hii ya upapa wake.” Hata hivyo ni tabia ambazo wengi, katika siku hizi za maombolezo, wamethibitisha.  “Alikuwa mtaalimungu mashuhuri, profesa, tofauti kimtindo na Yohane  Paulo II,  lakini mwenye kuwa na  moyo mkunjufu, aliyekuwa  wazi kwa wote, aliyekuwa makini sana hata kwetu, wasimamizi wake wa kawaida wa maadhimisho ya misa”, alisisitiza tena.

Umati ukitazama moshi mweupe ulioashiria uchaguzi  wa kumpata Papa Mpya mnamo 19.4.2005
Umati ukitazama moshi mweupe ulioashiria uchaguzi wa kumpata Papa Mpya mnamo 19.4.2005

Msimamizi wa Sadaka ya kitume aidha amekumbuka hali ya siku hizo, hata maumivu kwa ajili ya Papa Wojtyla, kwamba “moyo ulivunjika, lakini pia Papa mpya ambaye alikuwa karibu kuandika kurasa nyingine katika historia ya Kanisa”. Na “sasa ninaomboleza tena huku nikimshukuru Bwana kwa Upapa huu mkuu kwa sababu tumebahatika kweli kuwa na Mapapa hawa wa mwisho ambao ni watakatifu wa kweli, wanaotuongoza kwa uwazi na zaidi ya yote kwa utakatifu wa maisha yao. Ninaomba sana kwa ajili ya Benedikto na kwa ajili ya Kanisa”. Kardinali amehitimisha.

03 Januari 2023, 14:50