Kardinali Stella yuko Cuba kuadhimisha 25 tangu ziara ya Papa Wojtyla
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Historia ilidumu kwa siku 5 na kubaki Historia. Tarehe 21 Januari 1998, Mtakatifu Yohane Paulo II alitua Havana, katika kisiwa cha mapinduzi ya Fidel Castro ambapo Papa aliyekuwa ameubeba ukuta wa Berlin alitaka kuleta hata mapinduzi ya Injili. Kadinali Beniamino Stella amekumbusha hayo wakati wa kufanya kumbu kumbu ya miaka 25 ya tukio hilo na ambaye yuko Cuba kwa Juma moja kwa ajili ya kumbukumbu ambayo wakati ule ilimuona kama mhusika mkuu, yaani alikuwa ni Balozi waVatican nchini humo na kuwa karibu na Papa Wojtyla wakati wa kutua kwake.
Imani katika viwanja
Katika Misa iliyoadhimishwa mnamo tarehe 24 Januari katika Kanisa kuu la Havana, Kadinali alisisitiza urithi wa kifungu hicho hasa kwamba kwa kutazama nyuma, ambapo kimsingi ni sura ya imani, alisema tkwamba wanatambua uwepo wa Mtakatifu Yohane Paulo II kama wakati wa neema na baraka kwa taifa hilo, kwa wana na binti zake wote. Wacuba, waliweza kutangaza imani hadharani mitaani na viwanjani, na kuwaruhusu wengi kugundua tena mizizi yao ya Kikristo na kugundua upya Kanisa kama ukweli ambao ulikuwa sehemu ya maisha ya kitaifa, katika huduma ya wote bila kutenga yeyote.
Muujiza wa mikono mitupu
Baada ya adhimisho la kwanza la Ekaristi, Kardinali Stella aliyekaribishwa baada ya kuwasili kwake na Rais Miguel Díaz Canel alianza ziara ya utaratibu wa jumuiya za kikanisa. Mbali na mikutano mbalimbali, Mwenyekiti Mstaafu wa Baraza la Kipapa la Makleri aliyebaki Cuba tangu mwaka 1992 hadi 1999, aliongoza Ibada ya Misa Takatifu kwa siku katika maeneo takatifu na makanisa mbalimbali kisiwani humo, akitoka jimbo moja kwenda jimbo jingine. Kwa hiyo 29 Januari ilikuwa ni zamu ya Kanisa kuu la Matanzas, ambalo limefanyiwa ukarabati. Akikazia juu ya Heri, mada kuu ya Injili ya Dominika, Kadinali alikazia thamani ya hotuba ya Yesu, mchanganyiko wa unyenyekevu na upendo.
“Ninajua kwamba mnaishi humu kama Kanisa maskini, dogo na dhaifu, lakini mimi mwenyewe nilipokuwa balozi wa kitume, mara nyingi nilimsikia rafiki yangu Monsinyo Adolfo Rodriguez akisema kwamba Kanisa la Cuba haliwezi kulalamika juu ya Bwana wake na kulalamika juu ya Kanisa, ukweli kwamba haukumpatia chochote, kwa sababu Mungu alikuwa amemjalia yale ambayo Bernanos alisema: muujiza wa mikono mitupu, ambayo ni mikono yenye uwezo wa kutoa hata kile wasichokuwa nacho.” Muujiza, alihitimisha, ulioshuhudia wakati wa miaka ya janga na pia, alikumbuka, katika moto uliozuka mwezi Agosti iliyopita nje kidogo ya jiji kati ya tanki kubwa za ghala la mafuta. Liturujia ya Ekaristi hiyo kwa maana hiyo ilitolewa kwa waathrika wa janga hilo na wale wa Uviko.