Tafuta

2023.01.08 Kaburi la Papa Benedikito XVI. 2023.01.08 Kaburi la Papa Benedikito XVI. 

Kard.De Donatis:Unyenyekevu na utumishi ni utambulisho wa Papa Benedikto XVI

“Inatosha kufikiria uhusiano fulani aliokuwa nao Roma,mapadre na watu wa Casalbertone,katika parokia ambayo alikuwa amepewa kama Kardinali. alikweenda kutoa kipaimara lakini pia hata kula chakula cha jioni na makuhani.Ni maneno ya Kardinali De Donatis katika Kanisa ya kumwombea Hayati Papa Mstaafu Benedikto XVI.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kardinali Angelo de Dodatis, Makamu wa Papa wa Jimbo la Roma aliadhimisha misa Takatifu kwa ajili ya kukumbuka kifo cha Papa Mstaafu Benedikto XVI  na kumwombea mapumziko ya amani katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane, Laterano Roma, jioni tarehe 12 Januari 2023. Mahubiri yake yaliongozwa na sentensi ya neno la Mungu: “Ingekuwa heri  leo msikilize sauti yake  na msifanye migumu mioyo yenu”. Hiyo leo hii ni ambayo wamekutana kumshukuru Mungu kwa ushuhuda wa maisha  na utunzaji wa kichungaji wa Benedikto XVI kwa upande wa Jimbo la  Roma. Neno lilikuwa linatoka katika ukurasa wa Injili ya Marko  ambalo ni moja ya muujiza wa kwanza wa Yesu kumponya kijana. “Ninataka, utakaswe! Kwa hiyo papa mstaafu alitoa maoni yake juu ya kifungu hiki: “Katika ishara na maneno ya Kristo kuna historia nzima ya wokovu, kuna kuwilishwa mapenzi ya Mungu ya kutuponya, kututakasa na uovu unaotuharibu na kuharibu mahusiano yetu.

Papa Benedikito XVI anabaki katika moyo wa Kanisa na upendo wa Kanisa
Papa Benedikito XVI anabaki katika moyo wa Kanisa na upendo wa Kanisa

Katika mawasiliano hayo kati ya mkono wa Yesu na mwenye ukoma, kila kizuizi kimevunjwa kati ya Mungu na uchafu wa mwanadamu, kati ya Patakatifu na kinyume chake, ili kuonesha kwamba upendo wa Mungu una nguvu kuliko uovu wowote, hata ule unaoambukiza na wa kutisha.Yesu alijitwika udhaifu wetu juu yake mwenyewe. , akawa “mkoma” ili sisi tupate kutakaswa. Sote tunahitaji kuponywa namna hii, kuguswa na mkono wa Bwana. Utu wetu wote unaomba wokovu, hata wakati njia za historia, katika ulimwengu na katika maisha ya Kanisa, zinaonekana kuangaziwa na giza na majaribu tu. Injili ya Marko, ambayo itatusindikiza katika majuma haya ya kwanza ya wakati wa  kipindi cha kawaida cha Mwaka, Kardinali Di Donatis alisema , ni injili ya mfuasi, ambayo inatafuta kumwongoza mwanadamu kwenye ufahamu wa fumbo la Yesu, akimtambua kama Kristo.

Kanisa la Armenia lilisali kwa ajili ya Roho ipumzike vema ya Papa Benedikito VI
Kanisa la Armenia lilisali kwa ajili ya Roho ipumzike vema ya Papa Benedikito VI

Polepole mwandishi anamfunulia msomaji  kuwa Bwana ni nani hasa: si mtu wa miujiza, si mponyaji wa kawaida, lakini yeye ni Mwokozi, na Mwana wa Mungu. “Papa Benedikto XVI pia alituongoza kwa mkono, akitufundisha kumjua Bwana na kumkazia macho daima, Yesu wa Nazareti, Kristo anayeshiriki ubinadamu wetu, anakufa na kufufuka tena kwa ajili yetu. Tunaweza kusema kwamba mchanganyiko wa maisha yake yote, uzoefu wa kujifunza na kufundisha ulikuwa mtu pekee wa Mwana wa Mungu, akitukumbusha mara kwa mara kwamba bila yeye hakuna maana ya kuwa Mkristo. Na ilikuwa ya kusisimua sana kujua kwamba maneno yake ya mwisho yalikuwa: “Yesu, ninakupenda”, alisisitiza Kardinali Di Donatis.

Papa Benedikto XVI alikuwa mtaalimungu  mkuu kwa sababu alikuwa mpenzi mkuu wa Mungu, na alirudia mara nyingi kwamba Kanisa halikui kwa kugeuza imani bali kwa kuvutiwa.  Kwa maana hiyo “Katika siku hizi sisi sote tumetokea kuchukua baadhi ya maandiko yake, kupitia baadhi ya picha, kurudisha mioyoni mwetu baadhi ya matukio aliyoshiriki katika miaka ya upapa wake. Papa Benedikto  XVI alijitokeza katika  ulimwengu kwa unyenyekevu na heshima, kwa dhamira na kusikiliza, pia akitoa ishara mpya kwa Kanisa la Roma kama, kwa mfano, ushiriki wake wa kila mwaka katika uzinduzi wa mkutano wa jimbo, kwa mafunzo yake ya kina na wakati huo huo ya wazi na ya nguvu”.

Picha ya Papa Benedikito XVI siku alipochaugulia na kusalimia waamini kwa mara ya kwanza
Picha ya Papa Benedikito XVI siku alipochaugulia na kusalimia waamini kwa mara ya kwanza

Katika miaka  95 ya maisha yake, Papa Mstaafu Benedikto XVI aliishi miaka arobaini katika jiji la Roma ambalo kwa hiyo alikuwa ameshikamana nalo sana. Kwa kufafanua zaidi Kardinali di Donats aliomba wafikirie uhusiano fulani aliokuwa nao na mapadre na watu wa Casalbertone, katika parokia ambayo alikuwa amepewa kama Kardinali. Mara kadhaa alikwenda katika kanisa la Maria Konsolata kwa ajili misa za  Kipaimara lakini hata  kiurahisi kula  chakula cha jioni pamoja na makuhani wa Kanisa hilo. Mnamo tarehe 7 Mei 2005, alipoingia kwa mara ya kwanza kama Papa Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane, Lateramo, ili  kuweza kuchukua umiliki wa kiti chake kama mkuu wa Kanisa , alianza tena dhana ya kuwa mtumishi dhaifu wa Mungu na kusema  “Yeye anayeshikilia huduma ya Petro lazima awe na ufahamu wa kuwa mtu dhaifu na dhaifu, anayehitaji utakaso na uongofu daima”. Na alihitimisha mahubiri yake kwa kurejea kwa nguvu  juu ya Ekaristi. Alisema kwamba “Katika Fumbo hili upendo wa Kristo daima unaonekana kati yetu. Hapa, anajitoa kwa upya daima. Hapa, anaacha moyo wake upigwe kwa upya daima.

Shukrani kwa Ekaristi,  Kanisa daima linazaliwa  kwa upya! Kanisa si jingine ila mtandao  huo wa jumuiya ya  Ekaristi, ambamo sisi sote tunakuwa mwili mmoja na kuukumbatia ulimwengu mzima. Kusimamia katika mafundisho na kuongoza kwa upendo, mwishowe, lazima iwe kitu kimoja yaani  mafundisho yote ya Kanisa, hatimaye  yanaongoza katika upendo. Katika hilo, Kardinali di Donatiz alipenda kutoa mwaliko huo kwamba uwe wazi zaidi wako siku hiyo, hata kwa wakati ufaao zaidi. Hata kama kwa sasa tunapitiwa na kipindi cha majaribu , lazima tuamini kwamba shukrani kwa Ekaristi Kanisa limezaliwa kwa upya  mara ya pili. Huruma ya Yesu haijasimama, Bwana hajatusahau, Yeye ni “Mungu aliye karibu”, mkono wake umenyooshwa kuelekea ukoma wetu.  Papa Mstaafu Benedikto XVI alisema waziwazi wakati wa kuadhimisha miaka hamsini ya Mtaguso kwamba: “Tumeona kwamba udhaifu wa kibinadamu upo pia katika Kanisa, kwamba mtumbwa wa Kanisa unasafiri hata kwa upepo tofauti  na wakati mwingine tukiwa tumefikiri kwamba  “Bwana amelala na ametusahau” ... lakini pia tulipata uzoefu mpya wa uwepo wa Bwana, wa wema wake, na wa nguvu zake.

Misa ya Mazishi yake mnamo tarehe 5 Janauari 2023
Misa ya Mazishi yake mnamo tarehe 5 Janauari 2023

Kwa maana hiyo “Moto wa Roho Mtakatifu, moto wa Kristo si moto unaorarua, uangamizao bali ni moto wa kimya kimya, ni moto mdogo wa wema, wema na ukweli, ambao unabadilisha, kutoa mwanga na joto  la Bwana na sip wetu, lakini tunapofuata kwa upendo Mapenzi Yake na sio yetu,  tunakuwa na amani na kwa maana hiyo Papa benedikot XVI hakutaka kuacha kufundisha na akafanya; hivyo  hakutaka kuacha jimbo lake pendwa ya Munich na alifanya hivyo; aidha alitaka kwenda nyumbani kuwa pamoja na kaka yake na kumaliza masomo yake baada ya miaka 24 ya utumishi wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa …  na hakufanya hivyo; hadi  mnamo tarehe 11 Februari  2013, miaka kumi iliyopita wakati, katika wakati wa kustajabisha na usio wa kawaida, usiotabirika na wa kushangaza, alioneshania ya  kujiuzulu kwake kutoka katika kiti cha Upapa  na  jinsi alivyokuwa nataka mema ya Kanisa, akionesha  ushuhuda wake kwa Papa wetu Francisko kwa hekima isiyoweza kusemekana.

Papa Francisko akimuaga Papa Mstaafu kwa mara ya mwisho
Papa Francisko akimuaga Papa Mstaafu kwa mara ya mwisho

Karidnali Angeli di Donatis akirudi katika Injili iliyosomwa, alisema anaamini “Bwana anataka kuamsha, katika mioyo yetu yote, shauku ya  utakaso wa kweli, ambao huturudisha kwenye furaha na neema ya kukutana naye, na kuturudisha katika shauku ya kutangaza Injili hiyo”.  Akihitimisha  Kardinali de Donatis alipenda kutumia maneno ya Papa Francisko kuhusu maoni ya kifungu cha Injili ilyosomwa kwamba  “Na sasa, hebu tuwe na muda wa kimya, na kila mmoja wetu anaweza kufikiria katika moyo wake,  kuangalia ndani yake  mwenyewe. Na kila mmoja, kwa ukimya, lakini kwa sauti ya moyo anaweza kumwambia Yesu: “Ukitaka, waweza kunitakasa”. Na kwa kimya , kwa mwaliko wa Papa Francisko, tunaweza kuhisi ukaribu wa  Papa Benedikto  XVI ambaye ilithibitisha kwamba “Bwana na anayekubali shauku yetu kuwa “Nataka, takasika”.

Mahaburi ya Kardinali De Donatis katika misa katika Kanisa Kuu Laterano
13 January 2023, 17:09