Kard.Parolin:mafia ni chaguo la utumwa,turudi kuishi ndani ya sheria
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Ikiwa kukamatwa kwa Messina Denaro ni mafanikio ya serikali, inabakia kuwa jambo msingi, katika utekelezaji wa haki, wa kumweka mtu katikati, kama alivyofanya Mwenyeheri Rosario Livatino, hakimu wa kwanza ambaye Kanisa lilimwinua kwa heshima katika altare. Kwa ajili ya haki ambayo ni ukombozi na itaweza kuwaokoa wale wote ambao wameingia katika uwanja wa uhalifu. Hivyo ndivyo Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, alisema wakati waandishi wa habari wakimuuliza maoni yake juu ya kukamatwa kwa bosi huyo wa mafia (Kikundi cha kihalifu nchini Italia) baada ya miaka thelathini ya kujificha, ambapo mahojiano hayo yalifanyika kabla ya warsha iliyoandaliwa mchana tarehe 18 Januari 2023 katika Seneti, Roma Italia kuhusiana na habari za Mwenyeheri Rosario Livatino. Hafla, iliyoandaliwa na Kituo cha Utafiti cha Rosario Livatino, ambacho kilifunguliwa kwa ishara muhimu ya kuleta masalio ya jaji huyo ambalo ni shati la umwagaji damu alilovaa wakati wa mauaji yake mnamo tarehe 21 Septemba 1990 kwenye maktaba ya Jumba Kuu la Serikali ya Italia.
Kukamatwa kwa Msessina Denaro
Kwa hakika kukamatwa kwa Messina Denaro kunaweza kujumuishwa kama mafanikio ya serikali. Kulikuwa na juhudi kubwa ya nguvu za utaratibu. Tunaweza tu kufurahishwa na hitimisho hili. Kwa mujibu wa Katibu wa Vatican, alisema hii ni hatua ya kuwasili ambayo inaashiria mwisho wa msimu huo wote ambao tayari ulikuwapo. Ni matumaini yake kwamba wote wanaweza kurudi katika uhalali huo. Kuhusiana na kilichotokea Jumatatu 16 Januari 2023 huko Palermo cha kukamata muhalifu wa kimafia kinarejesha, zaidi ya yote kwa watu wa Sicilia, hisia kwamba "lazima tuishi pamoja kulingana na maadili, ambayo inawezekana hatimya kuacha uchaguzi wa uasi, uchaguzi wa mafia, ambao ni chaguo la utumwa kwa wale wanaoupitia na kwa watu wengine ambao ni wathirika. Kwa maana hiyo tunahitaji kujiondoa katika hilo", alisisitiza.
Rosario Livatino, Mkristo imara
Kuhusu Mwenyeheri Livatino, Kardinali Parolin alisema alikuwa ni mtu wa ajabu na kwamba katika warsha hiyo anakuza ujuzi wake na kwamba “Alikuwa Mkristo katika sehemu moja, ambaye aliweza kuishi imani yake kwa ukamilifu katika kutumia hasa taaluma nyeti kama ile ya mahakama, inayopatana na tafsiri yake na matumizi ya haki kwa kanuni za Kikristo.” Sadaka yake, pia kwa kuzingatia kile kilichotokea Jumatatu huko Palermo, haikuwa bure na hivyo “Nyakati za Bwana ni tofauti na nyakati zetu na hakuna uhakika kwamba matokeo yatakuja mara moja, lakini kwa hakika kila ishara ya ukarimu, kila tendo la upendo, kila toleo la maisha ya mtu, kila sadaka inayotolewa kwa jina la Bwana daima ina thawabu na huzaa matunda.”
Hakimu aliyechanganya haki na upendo
Mwenyeheri Livatino ameweza kuchanganya haki na upendo na huo ni ujumbe muhimu kwa mahakimu wa leo pia. Zaidi ya mambo hayo yote ambayo haki inakuwa ya ukombozi, inamweka mtu katikati na ni juhudi zinazofanywa pia na Serikali na jamii, ili kuweza kuwaokoa wale wote waliojiweka katika uwanja wa uhalifu na ubadilifu. Katika kutambulisha kazi ya mkutano huo, Kadinali baadaye alisisitiza jinsi sura nzuri ya mwenyeheri, ambaye alikufa shahidi wakati bado hajafikisha miaka 38, inastahili kupendekezwa zaidi ya yote kwa vijana. Mchakato wa kutangazwa mwenyeheri ulithibitisha kwamba mafia ya Agrigento walitaka auawe ili kukabiliana na kazi yake ya haki iliyozama katika Injili. Katibu wa Vatican alieleza kuwa Hakimu Mkristo Livatino ameonesha, kwamba imani inaweza kuwa roho na mwongozo katika kusimamia haki. Hakimu kijana alikumbusha kuwa kuchagua, ni moja ya mambo magumu zaidi kwa hakimu, lakini katika hilo, ikiwa ni mwamini, anaweza kupata msaada katika kukutana na Mungu katika sala na kusoma Injili. Kwa maana hiyo anatupatia fumbo la mahakama ambalo katika utekelezaji sahihi wa maamuzi yake, linakuwa nyongeza ya shughuli ya Mungu.
Chuki ya wamafia kwa maisha yake ya imani na sala
Na wamafia pia walichukia, maisha ya imani na sala ya Rosario Livatino, wakimwita “santocchio” e “bigotto”. Mtu ambaye akiwa anawahukumu, alikuwa akiomba kwa ajili ya roho za wafu kutokana na vita vya mafia. Wamafia ambao, ikiwa wanaonesha kujitolea kwa watakatifu na Maria, wanakana Ukristo kwa matendo yao na wanaishi aina ya upagani wa kujitolea kwa mungu wa fedha. Mwenyeheri sikuzote alijua jinsi ya kutumia wema wa msamaha. Hakumsahau jirani yake mwenye uhitaji, hata kama amefungwa. Akimtazama Kristo, alikumbuka kwamba kutanguliza upendo, hata kabla ya haki. Kwa hili aliteseka sana katika matamshi ya jinai dhidi ya washtakiwa. Kama Kristo Msalabani, aliwauliza watesaji wake “Nimewakosea nini?”. Na kifo chake cha kusikitisha kinakuwa uongofu kwa baadhi ya wakuu wake na wauaji”. Walimuua “Mkristo wa kweli na mwamuzi mlei, ambaye sasa yuko hai ndani yetu na kusema nasi kwa mfano wake”, alihitisha Kardinali Parolin.