Hayati Papa Benedikto VI:Harakati za kikanisa na jumuiya mpya ni zawadi
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Katika kufanya kumbu kumbu ya Hayati Papa Mstaafu Benedikto XVI, Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, wanatoa shukrani kwa Bwana kwa zawadi ya Mtumishi wake mwaminifu wa Injili na wa Kanisa, kama hata alivyomfafanua Papa Francisko hasa kwa sababu ya Mafundisho yake Makuu na kwa ajili ya ushuhuda wake wa imani ya maisha ya kikristo. Baraza hilo linafanya hivyo kwa kupendekeza baadhi ya hotuba zake/ mahubiri yake yanayohusiana na Harakati za Kikanisa na Jumuiya mpya, siku za Vijana duniani (WYD na Familia. Leo hii tunaona mojawapo ya hotuba aliyotoa kwa ajili ya Harakati za Kinanisa na jumuiya mpya. Katika moja ya hotuba yake Hayati Papa mstaafu Benedikito XVI kwa maaskofu washiriki wa Semina moja ya mafunzo iliyoandaliwa na Baraza la Kipapa la Familia la wakati ule mnamo tarehe 17 Mei 2008, alisema kuwa: “Harakati za Kikanisa na jumuiya mpya ni moja ya uvumbuzi mpya muhimu unaoibuliwa na Roho Mtakatifu ndani ya Kanisa kwa ajili ya utekelezaji wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican. Walienea baada ya mtaguso, hasa katika miaka iliyofuata mara moja, katika kipindi kilichojaa jitihada za kusisimua, lakini pia kilichokuwa na majaribu magumu. Papa Paulo VI na Yohane Paulo II walijua jinsi ya kukaribisha na kutambua, kuhimiza na kuhamasisha kusikotarajiwa wa ukweli mpya wa walei ambao, kwa namna mbalimbali na za kushangaza, ulirejesha uhai, imani na matumaini kwa Kanisa zima.
Ushuhuda wa furaha busa na hemia ya kuwa Wakristo
Hata hivyo, Papa alibainisha kuwa kwa hakika, walitoa ushuhuda wa furaha, busara na uzuri wa kuwa Wakristo, wakijionesha kuwa na shukrani kwa kuwa washiriki wa fumbo la ushirika ambalo ni Kanisa. Kwa maana hiyo alisema jinsi ambavyo walishuhudia kuamshwa tena kwa msukumo wenye nguvu wa kimisionari, uliochochewa na hamu ya kuwasiliana na mang’amuzi yote ya thamani ya kukutana na Kristo, kwa kutambuliwa na kuishi kama jibu pekee la kutosha kwa kiu ya kina cha ukweli na furaha ya moyo wa mwanadamu. Je, tunawezaje kushindwa kutambua, wakati huo huo, kwamba jambo jipya kama hilo bado linangoja kueleweka vya kutosha katika mwanga wa mpango wa Mungu na utume wa Kanisa katika mazingira ya wakati wetu? Kwa sababu hiyo basi kumekuwa na uingiliaji mwingi wa miito na maelekezo kutoka kwa Mapapa, ambao walianzisha mazungumzo na ushirikiano wa kina zaidi katika ngazi ya Makanisa mengi. Ubaguzi mwingi, upinzani na mivutano zilishindwa. Kazi muhimu ya kuendeleza ushirika uliokomaa zaidi wa vipengele vyote vya kikanisa inabaki kutimizwa, ili karama zote, kwa kuheshimu umaalum wake, ziweze kuchangia kikamilifu na kwa uhuru katika kuujenga Mwili mmoja wa Kristo.
Upendo mwingi lazima uhamasishwe,busara na uvumilivu
Kwenda kukutana na Harakati na jumuiya mpya kwa upendo mkubwa hutusukuma kujua uhalisi wao vya kutosha, bila mionekano ya kijuu juu au hukumu za kupunguza. Pia inatusaidia kuelewa kwamba Harakati za kikanisa na jumuiya mpya si tatizo au hatari ya ziada, ambayo inaongeza majukumu yetu ambayo tayari ni mazito. Hapana! Wao ni zawadi kutoka kwa Bwana, rasilimali ya thamani ya kuimarisha jumuiya nzima ya Kikristo kwa karama zao. Kwa hiyo, makaribisho ya imani yanayowapa nafasi na kuthamini michango yao katika maisha ya Makanisa mahalia hayapaswi kukosekana. Ugumu au kutoelewana juu ya masuala fulani hairuhusu kufungwa. Upendo mwingi unapaswa kuhamasishwa, busara na uvumilivu. Papa Mstaafu alisema wao kama wachungaji wanaombwa kusindikiza kwa ukaribu, pamoja na maombi ya kina ya kibaba, kwa njia ya maelewano na busara, Harakati na jumuiya mpya, ili kwa ukarimu waweze kuweka katika huduma ya manufaa ya wote, kwa utaratibu na matunda, karama nyingi ambapo wao ni wabebaji na kwamba wamefikia kujua na kuthamini: ari ya kimisionari, michakato ya safari ya ufanisi katika malezi ya Kikristo, ushuhuda wa uaminifu na utii kwa Kanisa, usikivu kwa mahitaji ya maskini, na utajiri wa miito.
Udhati wa karama mpya na utayari wa kunyenyekea
Papa Mstaafu Benedikto XVI alikuwa amesisitiza kuwa “Udhati wa karama mpya unahakikishwa na utayari wao wa kunyenyekea chini ya utambuzi wa mamlaka ya kikanisa. Harakati nyingi za kikanisa na jumuiya mpya tayari zimetambuliwa na Vatican na kwa hiyo lazima zihesabiwe kuwa zawadi kutoka kwa Mungu kwa Kanisa zima. Wengine, ambao bado wako katika hatua ya uchanga, wanahitaji ufuatiliaji wa hali ya juu na makini zaidi wa Wachungaji wa Makanisa mahalia. Yeyote anayeitwa katika huduma ya utambuzi na mwongozo asidai kuwa anatawala juu ya karama, bali ajihadhari na hatari ya kuzisonga roho (rej. 1 Thes. 5:19-21), akipinga kishawishi cha kuweka kiwango kile ambacho Roho Mtakatifu anacho tayari kuwa na sura nyingi ili kuchangia katika ujenzi na upanuzi wa Mwili mmoja wa Kristo, ambao Roho.
Harakati za kikanisa na Jumuiya mpya zisindikizwe
Hayati Papa Mstaafu Benedikito VI aidha alikuwa amesema kwamba Askofu kwa kuwekwa wakfu na kusaidiwa na Roho wa Mungu ndani ya Kristo, na Mkuu wa Kanisa, atapaswa kuchunguza karama na kuzijaribu, ili kutambua na kuthamini lililo jema, la kweli, linalochangia kuongezeka kwa utakatifu wa Mungu, watu binafsi na Jumuiya. Ikiwa uingiliaji kati wa marekebisho utahitajika, wao pia wanaweza kuwa maonesho ya upendo mwingi. Harakati na jumuiya mpya wanajivunia uhuru wao wa kujumuika, uaminifu kwa karama yao, lakini pia wamedhihirisha kwamba wanafahamu vyema kwamba uaminifu na uhuru unahakikishwa, na kwa hakika hauzuiliwi na umoja wa kikanisa, ambao Maaskofu wanayo na wao ni wahudumu, walezi na viongozi ambao wameungana Mrithi wa Petro.