Tafuta

Walemavu#TheChurchIsOurHome:Inuka&tembea!

'Rise up and walk!'Inuka na tembea! Ni mada ya video ya II ya watu wenye ulemavu na Sinodi.Ni kichocheo cha kutojiruhusu kufungwa na hali ya mtu na kujitwika jukumu la kutangaza Injili na kugeuza uhalisi ili iweze kuendelea kuuelekea Ufalme wa Mungu”. Video ya I ilikuwa desemba 6:‘Uwajibikaji pamoja na ujumuishwaji’.Nyingine zitakuwa Januari 12&26,2023.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha limechapisha tarehe 15 Desemba 2022 video ya Pili kuhusu Watu walemavu ‘#The ChurchIsOurHome’. Mpango ambao unataka kuakisi ushirikishwaji wa Walemavu katika mchakato wa safari ya Sinodi. Papa Francisko katika Mkutano tarehe 12 Desemba alisema kuwa “kwa kawaida kuna kufikiria ulemavu katika wazo la hitaji, la kusaidiwa na wakati mwingine, shukurani kwa Mungu kuna wazo fulani la kuonea  hata huruma kidogo. Lakini sio hivyo, kwani Papa hawatazami hivyo; Kanisa haliwatazami hivyo. Mtazamo wa kikristo kuhusu ulemavu, siyo zaidi na waa haipaswi kuwa ile ya kuonea huruma , na kama ile ya kutegemwa usaidizi. Lakini kwa utambuzi kuwa udhaifu, ukichukuliwa kwa uwajibikaji na mshikamano, ni rasiliamli kwa kiungo chote cha kijamii na kwa ajili ya jumuiya ya kikanisa.”

Injili inatoa nguvu isio tarajiwa

Kwa njia hiyo katika video ya Pili katika safu ya #TheChurchIsOurHome, yaani Kanisa ni Nyumbani kwetu’ ambayo imechapishwa tarehe 15 Novemba 2022, washiriki katikia eneo hili maalum la kisikilizakisinodi, wanaeleza ni jinsi gani ya kushiriki katika jumuiya ya kikanisa na kukutana na Injili ambayo inatoa nguvu isiyotarajiwa!

Inuka na tembea ni kichocheo cha kutojiruhusu kufungwa kushuhudia Injili

Kwa mujibu wa Enrique Alarcón Garcia, ambaye anazunguka kwa kutumia kiti cha magurudumu, anabainisha kuwa "maneno ya Yesu anayomweleza aliyepooza kuwa 'Inuka na tembea', ni kichocheo cha kutojiruhusu katu kufungwa na hali ya mtu na kujitwika jukumu la kutangaza Injili na kugeuza uhalisi ili iweze kuendelea kuuelekea Ufalme wa Mungu". Mchakato wa Safari ya Sinodi pamoja na mienendo shirikishi, kwa maana hiyo unafungua fursa ya ushiriki kamili wa watu wenye ulemavu katika maisha ya Kanisa na kuwawezesha kuelewa kikamilifu na kuishi wito wao mahususi.

 

Ikumbukwe kuwa Video hizi zinachapishwa katika majukwaa ya: Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, Sekretarieti kuu ya Sinodi na Vatican News. Huu ni mpango wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha,  kwa kutaka kusimulia mchango wa waamini walemavu katika Sinodi juu ya kuwa pamoja kwa kuongozwa na mada ya: ‘Uwajibikaji pamoja na ujumuishwaji ambayo ilichapishwa video hiyo tarehe 6 Desemba na nyingine mbili ya mfululizo huu zitachapishwa tarehe 12 na 26 Januari 2023.

Video ya II kuhusu Walemavu na mchakato wa Sinodi
15 December 2022, 14:59