2022.12.19 Mkutano vijana katoliki washeherekea Noeli kupitia mtandao wa kijamii. 2022.12.19 Mkutano vijana katoliki washeherekea Noeli kupitia mtandao wa kijamii. 

Wafuasi katoliki washeherekea Noeli kwenye 'bara la Kidijitali'

Hatua ya pili ya safari ya wainjilishaji vijana kwa njia ya mtandao kutoka nchi mbalimbali baada ya kumalizika kwa Sinodi ya kidijitali wamekutana kusheherekea Noeli kwa njia ya mtandao.Hatua ya kwanza ilikuwa maombi ya utume wa kimisionari Oktoba.Kati ya watoa mada, Askofu Mkuu Fischella pia Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Dk.Ruffini.

Na Angella Rwezaula,- Vatican.

Katika maandalizi ya Noeli, imefanyika mkutano tarehe 19 Desemba 2022 na wainjilishaji Katoliki  wa kidijitali ulioandaliwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano kati ya watoa mada alikuwa na Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la  Mawasiliano, Dk Paolo Ruffini, Askofu Mkuu Rino Fischella wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji na Monsinyo Lucio Adrián Ruiz, Katibu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano. Kwa upande wa Askofu Mkuu amejikita kutafakari juu ya somo lilisomwa la wito wa Nabii Yeremia. Ni andiko  muhimu sana ambalo linaruhusu kupokea wakati huo huo habari mpya kwa sehemu mbili. Kwa upande mmoja, ni nani nabii, na kwa upande mwingine, tunawezaje sisi kuwa manabii wa upendo wa ushuhuda upendo wa Mungu, katika kipindi hiki cha utamaduni wa kidijitali. Nabii si mtu wa mbwembwe. Mara nyingi katika lugha zetu tunatumia neno ili kuelekezea mambo ya wakati ujao. Sio hivyo.

Sherehe ya Noeli  kwa wafuasi katoliki wainjilishaji katika mtandao "Bara la kidijitali
Sherehe ya Noeli kwa wafuasi katoliki wainjilishaji katika mtandao "Bara la kidijitali

Unabii una maana ya kusema kwanza kuelezea mapema wakati ujao. Hakika baadhi ya vipindi vinaweza kupelekea hata ukubwa huo, lakini kwa maana nyingine sio msingi wa shughuli za kinabii. Kama ilivyosikia somo, Askofu Mkuu alisema nabii kinyume chake ni mtu ambaye ana shughuli ya kutunza na kuhuisha uhai wa Neno la Bwana. Si kwa bahati mbaya kwamba katika sanaa wachoraji fulani walitaka kumwakilisha nabii huyo kama mtu mwenye masikio makubwa, yasiyolingana na mwili wote. Maana ambayo msaanii alitaka kuchangia inaonekana wazi, kwani msanii wakati mwingine hana kazi kubwa ya kusikiliza. Na hili liweze kutokea kunahitaji ukimya ambao unaruhusu kupokea sauti ya Mungu ambayo mara nyingi inamezwa.

Sherehe ya Noeli  kwa wafuasi katoliki wainjilishaji katika mtandao "Bara la kidijitali
Sherehe ya Noeli kwa wafuasi katoliki wainjilishaji katika mtandao "Bara la kidijitali

Askofu Mkuu aidha alisema lakini kama tujuavyo, katika maisha, ya nabii mwingine, Elia Mungu anazungumza katika ukimya kwamba wakati mnong’ono mwanana wa upepo uliposikika”( 1 Wafalme 19, 12 ), Nabii alifunika uso wake kwa sababu alielewa kwamba yuko mbele za Mungu.” Mungu hakuwa ndani ya moto, hata katika upepo au katika tetemeko la ardhi, lakini katika ukimya. Nabii, kwa hiyo, kwa kulinganisha ni mtu wa kukaa kimya kwa sababu amechagua kusikiliza ili kuweza kulihusisha Neno la Mungu kwa upatanisho. Kila anayepokea wito daima ni katika ukimya kwa sababu ni Mungu anamkabidhi utume. Ssisi sote tunahusishwa katika uzoefu sana wa imani. Mara nyingi inawezekana kuwapo na kishawishi cha kuzuia kusikiliza Mungu na kutafuta sababu za kutokuwa tayari: kujifanya kuwa vijana ili kutoweza kuwa wawajibikaji, kutaka kuwa na ulazima wa kusubiri wakati mwingine ambao tunafikiri ni muafaka… kama Yeremia hasa sisi tunashawishika kusema: “sijuhi kuzungumza, … mimi ni kijana.” Na kumbe si hivyo tunaweza kujibu wito wa Mungu.

Askofu Mkuu Fisichella amesema, tunatambua kuwa Yeye anamtolea kila mmoja wetu zana za kuweza kujibu utume ambao anakabidhiwa. Kuna neno msingi katika maisha ya imani ambalo linaeleza vyema hali hiyo yaani neema. Hiyo inaonesha maisha ya Roho Mtakatifu ambayo hutolewa kwetu ili kuweza kutimiza kazi tuliyokabidhiwa. Hatuwezi kuogopa Mungu akiingia katika maisha yetu. Kwa kutoa mfano kuelewa jambo hilo Askofu Mkuu alisema “Hebu tufikirie ukweli mmoja: ikiwa hakuna umeme au betri imeisha charge huwezi kuunganishwa. Ikiwa hakuna mtandao wa mapokezi huwezi kupiga simu ... Ni kama hiyo katika maisha ambayo huzuia Mungu kuingia kwa sababu huwezi kuwasiliana. Huwezi kuhusiana na mtu yeyote…

Sherehe ya Noeli  kwa wafuasi katoliki wainjilishaji katika mtandao "Bara la kidijitali
Sherehe ya Noeli kwa wafuasi katoliki wainjilishaji katika mtandao "Bara la kidijitali

Askofu Mkuu Fisichella amebainisha kwa wote marafiki wa kidijitali waliokuwa wanafutilia kwamba, imani sio maneno. Kuamini si sawa na kujinyima kitu… kinyume chake ni kuitikia mwito ambao Yesu anamwalika kila mmoja kumfuata ili wote wawe wanafunzi wake wa umisionari ambapo unawezesha ndani kugundua tena maana ya kweli ya maisha.  Kwa njia hiyo wote hao hawapaswi kuogopa kuufungua kwa kuuweka wazi mlango wa mioyo yao  kwa upana ili kuukaribisha upendo ambao Bwana ameuleta, wala kuzuia akili zao kuzifungulia zaidi fumbo hilo la upendo tunalolikaribisha ndani  yak ila mmoja. “Tunahitaji jambo moja tu: kupendwa kuwepo kweli; kupenda kuishi kwa utulivu na uaminifu. Hii ndiyo imani yetu na hii inamaanisha kuwa manabii katika wakati wetu”, alihitimisha.

Dk.Ruffini kwa wainjilishaji wa kidijitali Mawasiliano ni muhimu:Mungu-Yesu-Roho na binadamu
Dk.Ruffini kwa wainjilishaji wa kidijitali Mawasiliano ni muhimu:Mungu-Yesu-Roho na binadamu

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, Dk Paulo Ruffini ameanza na maneno ya ushairi kwa kuwatakia kila mmoja Noeli inayokuja, katika wakati mweusi na wakati wa kuchanganyikiwa. Kipindi kinachangamotisha kama watoa habari kukumbusha kuwa Noeli tayari imefika. Ni katika kipindi ambacho sio cha kwetu, lakini kama ilivyo kuwa hapo awali na kama leo hii kimebadilisha na mabadiliko ya kihistoria. Na kinatualika tusiogope. Kwa sababu Mungu alijifanya mtu kweli na hivyo hata mtoto mdhaifu kwa muonekana, aliwadharau wenye kiburi katika mioyo yao na kuwaangusha wenye nguvu kutoka viti vyao na kuwainua wanyenyekevu; aliwafariji; amewashibisha wenye njaa vitu vizuri, aliwafukuza matajiri mikono mitupu. Alipitia machungu, mateso na mahangaiko ya kila mwanadamu. Na kwa kushinda kifo, akajitwika maovu ya ulimwengu, alirudisha maana kwa yale yote ambayo yalikuwa yamepotea, na kuokoa uhusiano wa kiumbe-muumba.

Sherehe ya Noeli  kwa wafuasi katoliki wainjilishaji katika mtandao "Bara la kidijitali
Sherehe ya Noeli kwa wafuasi katoliki wainjilishaji katika mtandao "Bara la kidijitali

Dk. Ruffini aidha alisema kwamba: “ Hata sisi leo hii kama ilivyo hata ninyi, heri kwa sababu tuliamini pasipo kuona, kama wachungaji, tunaweza kushuhudia mkutano huu unaotutaka tushirikishwe katika ngazi ya kimataifa, kupitia ulimwengu mkuu wa wavuti.” Kwa njia hiyo alisema “ kushirikisha ni ufunguo wa neno, kushirikishi wema, uzuri, kushirikisha matarajio ya wokovu. Kushirikisha tukio linalotupitia,na kwa sababu hiyo linapenyeza giza; linayeyusha hatari ya ibada ya sanamu ya kujitosheleza, hujenga umoja kwa njia ya mawasiliano. Hiyo ni zawadi ya ushuhuda wetu. Changamoto moja tuliyo nayo mbele kwa hakika ni hii hapa. Umoja ni neno la kikristo kwa ajili ya kutangaza Noeli ambayo ilikuja na ambayo inakuja. Ni kutangaza uhakika wa mwangaza zaidi ya giza. Ya ufufuko zaidi ya kifo”.

Sherehe ya Noeli  kwa wafuasi katoliki wainjilishaji katika mtandao "Bara la kidijitali
Sherehe ya Noeli kwa wafuasi katoliki wainjilishaji katika mtandao "Bara la kidijitali

Akinukuu kifungu cha maneno ya Kardinali Martini kuhusu mtazamo wa mwisho wa maisha ya Yesu, Dk. Ruffini alisema: “Katika kaburi la Yesu, usiku wa Pasaka, ishara kali zaidi ya mawasiliano katika historia nzima ya wanadamu hufanyika. Roho Mtakatifu, kwa kumpa uzima Yesu mfufuka, anawasiliana na mwili wake nguvu yenyewe ya Mungu. Kwa kuwasiliana mwenyewe na Yesu, Roho hujitambulisha  yenyewe kwa wanadamu wote na kufungua njia ya mawasiliano yote ya kweli. Ni sahihi kwa sababu inahusisha karama ya nafsi, hivyo kushinda utata wa mawasiliano ya kibinadamu ambayo mtu hajui ni kwa kiwango gani vinahusika jambo na kitu  Mawasiliano kwa hiyo kwanza kabisa yatakuwa kile ambacho Baba alichofanya yeye mwenyewe kwa Yesu, na baadaye  kile ambacho Mungu anafanya kwa kila mwanamume na mwanamke, pia kwa kile tunachofanyiana sisi kwa sisi katika  kielelezo cha mawasiliano haya ya kimungu.

Sherehe ya Noeli  kwa wafuasi katoliki wainjilishaji katika mtandao "Bara la kidijitali
Sherehe ya Noeli kwa wafuasi katoliki wainjilishaji katika mtandao "Bara la kidijitali

Kwa hiyo Roho Mtakatifu, ambaye tunapokea shukrani kwa kifo na ufufuko wa Yesu na ambaye hutufanya tuishi kwa kumwiga Yesu mwenyewe, anaongoza roho ya mawasiliano ndani yetu. Anaweka ndani yetu sifa, kama vile kujitolea na kupendana,  sifa ambazo hutukumbusha zile za Neno  lililofanyika Mwili. ….. Kwa hiyo hata mawasiliano katika Kanisa … ni kubadilishana mioyo katika neema ya Roho Mtakatifu. Kwa hiyo sifa zake ni kuaminiana, kutangaza , kuelewana na mwingine na kuwa na  huruma”. Dk. Rufini kwa kuongeza amesema tazama  ndio changamoto yetu. Na kwa pamoja tunaweza kujenga mawasiliano tofauti. Kwa unyenyekevu, bila majivuno, bila kujipendelea; kwa ufahamu ya  kuwa sisi ni watumishi wasio na faida, ni vyombo vya utume unaotuvusha. Tunaweza kuunda mtandao wa ushuhuda kwa kutambya tofauti kati ya Roho ambaye anatuunganisha(Kati yetu na Mungu, kama wajumbe wa mmoja na wengine) na teknolojia ambazo (zikiachwa zenyewe, kwa kukosa pumzi ya kimungu inayohuisha roho zetu) hazitambui  upendo ambao kila kitu kipo. Na hatimaye amewatakia Nole njiema na kwamba “Udogo wa Mungu ambaye anakuwa mtoto, dhaifu, asiye na kinga, utufundishe kuamini lakini si katika kujiamini sana badala yake ndani yake, na uzuri wa kuwa wajumbe wa  kila mmoja, mashuhuda wa njia tofauti ya kuishi maisha yetu katika wakati.”

Sherehe ya Noeli kwa 'Bara la Kidijitali"
20 December 2022, 16:57