Uzinduzi wa Toleo la V la maonesho ya mapango 100 jijini Vatican
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Toleo la tano la kimataifa zaidi ya mapango 100 mjini Vatican linarudi tena,ambalo ni maonesho yanayokusanya kazi zilizofanywa na wasanii wengi ulimwenguni kote ambao mara nyingi wanaelezea ubunifu wao katika kuwakilisha wa tukio la Kuzaliwa kwa Bwana. Kwa njia hiyo tarehe 8 Desemba 2022 uzinduzi huo utafanyika chini ya nguzo za Bernini, zinazozungukia Uwanja wa Mtakatifu Petro. Kazi hiyo ya kisanii inayojumuisha mapango mbali mbali ambapo inawakaribisha kwa mara nyingine tena wageni kushangaa mbele mila na tamaduni za kutengeneza mapango ya kuzaliwa kwa Yesu. Mwaka huu yatakuwa mapango 120 kutoka nchi mbali mbali za Ulaya kama vile Ukraine, Hungeria, Malta, Slovenia, Slovacchia, Croazia, na katika ulimwengu kama vile Taiwan, Venezuela na Guatemala. Nchi nyingi hizi zinawakilishwa tayari na Mabalozi wa nchi zao katika Ubalozi jiji la Vatican ambao wamepewa jukumu la kuhamasisha matukio ya nchi zao binafsi.
Maonesho hayo yatabaki kwa wiki tano, kuanzia tarehe 8 Desemba 2022 hadi Diminika tarehe 8 Januari 2023, kuanzia saa 4.00 hadi saa 1.30 usiku kila siku. Kiingilio ni bure na hakuhitaji kuomba mapema. Tarehe 24 Desemba na 31 Desemba 2022 Maonesho yatafungwa mapema saa 11 kamili jioni. Maonesho hayo yatazinduliwa saa 10.00 kamili na Askofu Mkuu Rino Fisichella, pamoja na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, kitengo ambacho kinahusika na masuala msingi ya uinjilishaji ulimwenguni. Atakuwapo pia mwakilishi wa Ubalozi wa Ukraine kutoka Ubalozi katika Vatican na wajumbe mbali mbali wa jumuiya hiyo ambao watashangaza tukio hilo kwa kutumbuiza nyimbo za siku kuu ya kuzaliwa kwa Bwana kutoka Ukraine. Bendi ya muziki pia kutoka kikundi cha Ulinzi wa mji wa vatican kitasindikiza tukio hilo kwa baadhi ya nyimbo rasmi.