Tafuta

Papa na baraza la Makardinali 5 na 6 Desemba 2022. Papa na baraza la Makardinali 5 na 6 Desemba 2022. 

Ulinzi wa Watoto na Cop27 ni kati ya mada za Mkutano wa Baraza la Makardinali

Katika nyumba ya Mtakatifu Marta,kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya Habari ya Kiti Kitakatifu,kazi ya Baraza ilifanyika katika siku za hivi karibuni,tarehe 5 na 6 Desemba,mbele ya Papa.Kulikuwa na muda wa kutafakari juu ya awamu ya pili ya mchakato wa Sinodi kibara.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko alishiriki katika mkutano wa Baraza la Makardinali, katika Nyumba ya Mtakatifu Marta, tarehe 5 na 6 Desemba. Katika siku ya kwanza, suala la mkutano  COP27 nchini Misri lilikuwa katikati ya mkutano huo, ambapo walianza na kusikiliza ripoti  kutoka kwa Makadinali Parolin na Ambongo Besungu. Siku hiyo hiyo, Makardinali pia walishiriki katika adhimisho la Ekaristi Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu petro kwa ajili ya mazishi ya  Kardinali Richard Kuuia Baawobr wa Ghana.

Siku ya Jumanne tarehe 6 Desemba, pamoja na Papa, Makardinali waliweza kutafakari juu ya awamu ya pili ya  mchakato wa Sinodi katika mabara inayoendelea, yenye mada 'Kwa ajili ya Kanisa la Sinodi: Ushirika, Ushiriki na Utume'. Katika ripoti ya Kardinali Mario, Grech na matunda ya mchakato wa sinodi ya kidijitali ilifafanua kuwa kuna ushirikiano na Baraza la kipapa la Mawasiliano. Mwishoni, Kardinali O'Malley alielezea juhudi za hivi karibuni za Tume ya Ulinzi wa Watoto katika huduma ya Mabaraza ya Maaskofu na Curia Romana  na, alasiri, Kardinali Gracias aliripoti juu ya Mkutano wa Shirikisho la Maaskofu wa Asia katika  Mkutano , ulofanyika Bangkok  mwezi Oktoba  uliopita.

Mkutano huo ulikuwa fursa ya kusasisha baadhi ya mambo ya sasa katika maeneo mbalimbali ya kijiografia na kurejea tathmini ya jumla ya maendeleo ya Bodi katika miaka ya hivi karibuni. Walioshiriki katika mkutano huo, ambao uteuzi wao ujao umepangwa kufanyika mwezi wa Aprili 2023, walikuwa Makadinali Pietro Parolin, Giuseppe Bertello, Óscar A. Rodríguez Maradiaga, Reinhard Marx, Seán Patrick O'Malley, Oswald Gracias na Fridolin Ambongo Besungu, kama pamoja na Katibu wa Baraza, Monsinyo Marco Mellino.

08 December 2022, 16:59