2022..12.19 Kardinali Krajewski yuko Ukraine. 2022..12.19 Kardinali Krajewski yuko Ukraine. 

Ukraine,masweta ya joto:lengo limefikiwa lakini makusanyiko yanaendelea

Zaidi ya euro 111,000 zimekusanywa hadi sasa kupitia jukwaa la Eppela,ili kuruhusu michango ya pesa kutumika kwa ununuzi wa sweta za joto,mafuta ya genereta na kutumwa katika nchi iliyokumbwa na vita.Kardinali Krajewski,yuko sasa katika utume mpya kwa niaba ya Papa na lori,tayari amewasilisha sehemu ya vifaa vilivyokusanywa.

Na Angella Rwezaula;- Vatican

Zaidi ya euro 111,000 zimekusanywa hadi sasa kupitia jukwaa la Eppela, lililozinduliwa hivi karibuni ili kuruhusu michango ya pesa kutumika kwa ununuzi wa nguo  za joto na ziweze kutumwa katika nchi iliyokumbwa na vita, Ukraine. Kardinali Konrad Krajewski, ambaye aliondoka kwa utume mpya wa Kipapa na lori, tayari amewasilisha sehemu ya nyenzo zilizokusanywa pamoja na jenereta zilizotolewa na kununuliwa kwa idadi ya watu. Na siku chache zilizopita wito ulikuwa umefika kuhusu  majira ya baridi karibu kila kona, kwa idadi ya watu wa Ukraine, iliyojaribiwa sana na vita, ambayo itajikuta inakabiliwa na baridi  kali, masweta maalum ya  joto yanahitajika. Aliyeomba msaada alikuwa Kardinali Konrad Krajewski, Msimamizi ya Sadaka ya Kipapa, ambaye aliondoka kwenda Ukraine Jumamosi iliyopita katika utume mpya, ambaye katika taarifa yake alizindua uchangishaji kupitia jukwaa la mtandao  ili kuweza kununua sweta zinazofaa kwa msimu wa baridi ili kutumwa Ukraine.

Kardinali Krajewski ameanza kusambaza generata nchini Ukraine
Kardinali Krajewski ameanza kusambaza generata nchini Ukraine

Katika wito wao walikuwa wamesema wanahitai euro elfu 100.  Na kwa bahati nzuri usiku wa manane tarehe 19 Desemba, 2022 lengo hili lilifikiwa na sasa limepita na kufikia zaidi ya euro 111,000. Kardinali, aliyetumwa na Papa kuwapelekea watu wa Ukraine pamoja na uwepo wake, pamoja na faraja katika imani, matunda ya mshikamano yaliyooneshwa na watu wengi katika wiki za hivi karibuni  ambavyo ni jenereta za umeme, mavazi ya joto  na tayari vimefikia Lviv na sehemu nyingine ziliokusudiwa. Miongoni mwa vituo vyake pia Zaporizhzhia, Odessa na Kyiv. Shukrani kutoka kwa Mkuu wa sadaka ya kitume kwa wale  wote waliochana na wanaotaka kuchangia na kwa kuwa bado kuna dharura ya baridi inaendelea na upendo unaweza kusaidia kutoa angalau misaada kwamba makusanyo yataendelea hadi  tarehe 6 Januari 2023.

Kardinali Krajewski aliondoka na loro la vifaa vya kusaidia nchini Ukraine
Kardinali Krajewski aliondoka na loro la vifaa vya kusaidia nchini Ukraine

Kwa mujibu wa  Kardinali Krajewski alisisitiza katika taarifa kwa vyombo vya habari, “Makusanyo ya  ziada yataenda kabisa kwa ununuzi wa mava na  mafuta kwa wakazi wa Ukraine. Noeli ya Kikristo ya kweli, hivyo ikiwa mtu anakaribisha hitaji la mwingine, kukumbatia mateso na kuchukua hata hatua kidogo kuyapunguza”. Kwa moyo huu, ofisi ya misaada ya Papa ilikuwa imezindua uchangishaji wa pesa wiki iliyopita. Siku chache mapema kulikuwa na ombi la kutuma au kuleta mavazi ya wanaume, wanawake na watoto Vatican.


Kardinali anawashukuru  kwamba “Moyo wa Waitaliano ni mzuri, ulio wazi,  aliongeza huku akirudia kutoa wito wake wa ununuzi wa masweta, na mafuta na kuzingatia ukarimu wa wengi kwa watu wa Kiukreni. Kardinali Krajewski alikuwa pia amehakikisha kwamba yeye mwenyewe angepeleka nyenzo zilizokusanywa nchini. Na kiukweli Kardinali tayari ameshafikisha sehemu ya mzigo wa lori alilotoka  nalo Vatican. Lakini unahitaji kuwa tayari kwa hitaji lolote jipya kwa sababu msimu wa baridi ni mrefu na baridi. Ndiyo maana uchangishaji unaendelea hadi tarehe 6 Januari. Mpango huo ulifuatia ombi la Papa, lililozinduliwa Jumatano iliyopita mwishoni mwa katekesi yake  "ili Noeli iwe ya  unyenyekevu zaidi, kuokoa kitu kwa watu wa Ukraine wanaohitaji". “Wanaoteseka sana, watu wanahisi baridi na wengi wanakufa kwa sababu hakuna madaktari na wauguzi. Noeli ndiyo, lakini na Waukraine wawe moyoni," alisema Papa.

Bonyeza: https://e.va/magliettetermicheucraina kwa ajili ya uwezekano wa kutoa chochote ili kununua masweta maalum ya joto kwa watu wa Ukraine.

21 December 2022, 16:39