Ufadhili wa masomo Kard.Foley: 7 Machi 2023 ni mwisho wa kuwasilisha!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kuna ufadhili wa Masomo kutoka Mfuko wa Kardinali Foley (Cardinal Foley Scholarship Fund, CFSF) kwa ajili ya mafunzo na mahitaji yote yanayohitajika kwa mwanafunzi atakayekuwa amekubaliwa kutoka nchi za kusini mwa dunia kwa ajili ya programu za masters na uzamili katika tasnia ya mawasiliano. Lengo ni kupanua msingi wa mapadre wenye sifa na uwezo, watawa na walei ili kuendeleza huduma ya mawasiliano katika makanisa mahalia. Pia mfuko huo unakusudia kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa Afrika, Asia na Amerika Kusini kwa kutoa mafunzo kwa wawasilianaji wa Kanisa wa siku zijazo katika vyuo vya mafunzo mahalia, vitivo vya mawasiliano (na taalimungu) na seminari kuu.
Kwa njia hiyo uwakilishi wa maombi ya ufadhili wa mafunzo utafungwa tarehe 7 Machi 2023 kwa ajili ya ufadhili huo kwa mwaka wa masomo 2023/2024. Mfuko wa udhamini unaratibiwa na kusimamiwa na CAMECO. Kamati ya uchunguzi, ambayo inatoa nafasi za masomo, kwa sasa inaundwa na wawakilishi Baraza la Kipapa la Mawasiliano, Aachen Mission, Institute of Missiology, USCCB Catholic Communication Campaign na Adveniat.
Wadhaminiwa wote hata hivyo hawawezi kuwasilisha maombi yao kwa kujitegemea, lakini lazima waungwe mkono na mamlaka ya Kanisa au mkuu wa Shirika la Kitawa ambaye anamsimamia mwombaji. Kuanzia 2012 hadi leo, mfuko huo umewezesha wanafunzi 81 ambao wamepata ufadhili wa masomo. Mfuko huo umepewa jina la Kardinali John Patrick Foley, aliyekuwa rais wa zamani wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, kwa heshima ya kujitoa kwake kuendelea kujenga uwezo wa Kanisa katika ushiriki wake wa kimawasiliano. Maelezo zaidi yanapatikana kwenye tovuti rasmi ya Cameco ambapo unaweza kupata hata fomu muhimu ya ya kujaza au kutuma scholarship@cameco.org
Je unawezaje kutuma ombi na ni nani anafaa ufadhili wa masomo?
Mapadre, mashemasi, watawa, wa kudumu na walei, wanaume na wanawake, wakisaidiwa na askofu wao na/au wakuu wao wa mashirika, na wenye uwezo uliothibitishwa (pamoja na uzoefu wa vitendo) na nia ya kufanya kazi katika tasnia ya mawasiliano. Maombi yanahitajika kuwasilishwa na mamlaka ya Kanisa husika. Kumbuka kuwa maombi yanayotumwa na wagombea wenyewe hayawezi kuzingatiwa, lazima kufuata vigezo vilivyowekwa.
Ikumbukwe kuwa Mfuko wa Udhamini wa Kadinali Foley,(CFSF) unasaidia gharama za elimu na maisha za wanafunzi kutoka Kusini mwa dunia katika programu za Master na Uzamili katika tasnia ya mawasiliano. Mfuko huo umepewa jina la kumbukumbu ya Kardinali John Patrick Foley, aliyekuwa rais wa zamani wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, kwa heshima yake ahadi ya kudumu katika kujenga uwezo wa Kanisa katika ushiriki wake wa mawasiliano. Mfuko wa udhamini unashughulikia hitaji la malezi ya kutosha ya kitaaluma kwa wale ambao watawajibika kwa ajili ya maendeleo ya baadaye ya utume wa Kanisa mahalia katika uwanja wa mawasiliano.