Toa zawadi ya sweta maalum ya joto kwa watu Ukraine katika mpango:‘crowdfunding
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Kuanzia tarehe 16 Desemba 2022, limefunguliwa jukwaa la ufadhili liitwalo ‘crowdfunding Eppela’ na kwa kubonyeza tu kwa nia ya kusaidia inawezekana, kutoa hata kiasi kidogo ili kununua masweta mazito maalumu ya joto kwa ajili ya watu wa Ukraine. Katika katekesi yake siku ya Jumatano, Baba Mtakatifu Francisko alipendekeza kwamba inawezekana kufanya “Noeli yenye gharama chache ya unyenyekevu zaidi, huku akihimiza kutuma chochote kile kilichookolewa ili kupunguza mateso ya wengi wanaosumbuliwa na baridi, njaa, ukosefu wa huduma. Na kwamba Noeli na moyo wa Ukraine.
Siku chache zilizopita, Baraza la Kipapa la Upendo lilikuwa tayari limezindua mkusanyo wa kutuma au kuleta mavazi yaliyoombwa Vatican. “Mwitikio wa watu ulikuwa wa ukarimu sana kwa sababu mioyo ya Waitaliano ni mizuri, iliyo wazi na ambapo, tayari wamejibu kwa shauku kwa ajili ya matatizo ya wale wanaoteseka kwa abbu ya vita alielezea Kardinali Konrad Krajewski, Mkuu Sadaka ya Kitume ya Papa. Kwa maana hiyo Kardinali Krajewski alihakikishia lengo lake wenye viwanda vingi, vilivyowasiliana hapo awali na ambavyo tayari vimetoa masweta ya joto lakini pia kuwezesha ununuzi kwa bei ya uzalishaji au utambuzi.
Mara tu nyenzo zitakapokusanywa na kupakiwa kwenye lori, pamoja na jenereta za nishati zilizonunuliwa, Kardinali Konrad Krajewski, mwenyewe atapeleka kila kitu huko Ukraine. Hata hivyo kuèpeleka vifaa hivyo sio mwisho bali ni muhimu kuendelea na kujitoa , kwa sababu baridi ni ndefu na ngumu, ambapo kweli ni muhimu kuwa tayari kwa mahitaji yoyote mapya. Ameomba watoe zawadi hiyo ya Noeli na ni mwaliko ambao, kama Papa Francisko alivyokuwa amsema katika mahubiri yake kwenye Misa katika Nyumba ya Mtakatifu Marta mnamo tarehe 26 Novemba 2018, kuwa :“ukarimu ni jambo la kila siku, ni ukarimu wa mambo madogo.” Kwa maana hiyo Ukibonyeza hapa inawezekana kutoa zawadi ya sweta la joto katika mpango huo:
https://www.eppela.com/projects/9302