Tafuta

Vatican kuendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na Slovenia kwa ajili ya ustawi, maendeleo ya watu wa mungu Vatican kuendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na Slovenia kwa ajili ya ustawi, maendeleo ya watu wa mungu 

Slovenia na Vatican Kuimarisha Zaidi Uhusiano wa Kidiplomasia Kwa Ajili ya Mafao ya Wengi

Baba Mtakatifu pamoja na mgeni wake, katika mazungumzo yao, wote wawili wameridhika na uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili na kwamba wametia nia ya kuendelea kuboresha uhusiano huu katika maeneo muhimu zaidi. Viongozi hawa wawili wameridhishwa na mchango wa Kanisa Katoliki katika ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini Slovenia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 17 Desemba 2022 amekutana na kuzungumza na Bwana Robert Golob, Waziri mkuu wa Slovenia ambaye baadaye amebahatika kukutana na kuzungumza pia na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje, Ushirikiano na Mashirika ya Kimataifa. Baba Mtakatifu pamoja na mgeni wake, katika mazungumzo yao, wote wawili wameridhika na uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili na kwamba wametia nia ya kuendelea kuboresha uhusiano huu katika maeneo muhimu zaidi.

Vatican na Slovakia kuendeleza zaidi uhusiano wa kidiplomasia
Vatican na Slovakia kuendeleza zaidi uhusiano wa kidiplomasia

Viongozi hawa wawili wameridhishwa na mchango wa Kanisa Katoliki katika ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini Slovenia. Baba Mtakatifu Francisko na Waziri mkuu wa Slovenia, katika mazungumzo yao, wamegusia tema mbalimbali katika medani za Kimataifa kwa kujikita zaidi kuhusiana na: Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, EU, Nchi zilizoko Magharibi mwa Balkan, hali ya vita nchini Ukraine na madhara yake katika Ukanda wa Nchi za Ulaya. Baadaye walibadilishana zawadi mbalimbali kama ukumbusho wa siku hii muhimu kati ya Baba Mtakatifu Francisko na Bwana Robert Golob, Waziri mkuu wa Slovenia.

Slovenia
20 December 2022, 16:06