Tafuta

Kozi ya mafunzo kuhusu Sidoni Januari 2023 Kozi ya mafunzo kuhusu Sidoni Januari 2023 

Sinodi:Uandikishaji wa kozi ya mafunzo kwa lugha tofauti kuhusu Sinodi umefunguliwa

Mnamo Januari 2023 itafanyika kozi ya mafunzo kwa lugha mbambali kuhusu Sinodi,iliyoandaliwa na Kituo cha Evangelii Gaudium cha Taasisi ya Chuo Kikuu Sophia.Kozi hiyo hiyo inakusudia kutoa maandalizi ya kitaalimungu na kichungaji kwa upana na lengo la kuweza kutoa kwa jumuiya ya kikristo mtindo wa mazoezi ya kijumuiya katika kufikiria na kutenda kikristo.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Somo la kwanza la utangulizi limekabidhiwa kwa Kardinali Mario Grech, Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu litalofanyika mnamo tarehe 17 Januari 2023 ijayo, ambalo ni sehemu ya Kozi kwa  lugha mbali mbali kuhusu Sinodi iliyoandaliwa na Kituo cha Evangelii Gaudium cha Taasisi ya Chuo Kikuu Sophia. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kuhusiana na kozi hiyo,  Ofisi Kuu ya Sinodi ya maaskofu iliyoandaliwa kwa ushirikiano na Sekretarieti kuu ya Sinodi, kutakuwa na hatua 4. Kati ya hizo 3 zitakuwa za kitaaluma na mkutano wa  mwisho kwa wanaoishi Roma.

Je ni mantiki gani zitatolewa?

Mantiki zitakazozingatiwa zinahusiana na mchakato wa Sinodi ambapo itakuwa n:  Nini maana ya Sinodi? Hii ya mwisho inaendana na kile kilichofafanauliwa na Mafundisho ya Kanisa na sheria ya Kanoni? Je inawezekana kuiishi katika Kanisa? Kutokana na kwamba wahusika ni watu wote wa Mungu (kuanzia na maaskofu, wahudumu wa kichungaji, mapadre, na watawa wote kike na kiume, waseminari na walei wote), kozi hiyo inakusudia kutoa maandalizi ya kitaalimungu na kichungaji kwa upana mkubwa na lengo la kuweza kutoa kwa jumuiya ya kikristo mtindo mmoja wa mazoezi ya kijumuiya ya kufikiria na kutenda kikristo.

Namna ya kufanya kozi hiyo

Kozi hiyo kwa mujibu wa taarifa ni kwamba itafanyika kupitia jukwaa la Zoom. Na inawezekana kujiandikisha kwa kozi nzima au kwa hatua moja moja kati ya mafungu hayo manne. Mafunzo hayo yatafanyika kwa lugha ya kiitaliano, ikiwa pamoja na tafsiri ya moja kwa moja kwa lugha ya kihispania, kireno na kiingereza. Kozi hiyo inawatazama hata wajumbe wote wa jumuiya sawa kama vila ( Parokia, vyama vya kitume  na marafiki) ambao wanaweza kufanya uzoefu wa moja kwa moja wa mitindo ya kusikiliza, ya kujadiliana na kufanya maamuzi kwa msingi wa Kanisa la kisinodi.

Kwa maelezo zaidi na kujiandikisha tembelea tovuti ifuatayo: ceg@sophiauniversity.org 

au https://www.sophiauniversity.org/it/centro-evangelii-gaudium

20 December 2022, 15:56