Tafuta

Papa Mstaaafu amerudi Nyumbani kwa Mungu Baba Mwenyezi. Papa Mstaaafu amerudi Nyumbani kwa Mungu Baba Mwenyezi. 

Ufunguo wa upapa wake ni “Mungu ni upendo”

Benedikto XVI mbele ya kashifa ya kikuhani kikanisa,aliendelea kutoa mwito wa uongofu,kutubu,unyenyekevu na kupendekeza picha ya Kanisa huru dhidi ya mali na siasa kwa ajili ya kuwa na ufunguzi wazi ulimwenguni.

ANDREA TORNIELLI

Ilikuwa ni mnamo mwaka 1417 kwamba kifo cha Papa mstaafu kisingekuwa na maana ya mwisho wa upapa. Kifo cha Benedict XVI, aliyekuwa anaitwa Joseph Ratzinger, kimetokea leo mjini Vatican, karibu miaka kumi baada ya tangazo lake la mshangao mnamo tarehe 11 Februari 2013, kwa kusomwa kwa taarifa fupi ya Kilatino mbele ya makadinali walioshangaa. Kamwe katika milenia mbili ya historia ya Kanisa Papa hakuwahi kuondoka kwenye kiti chake kwa sababu ya kujiona hafai kustahimili uzito wa upapa. Baada ya yote, katika jibu alilopewa mwandishi wa habari Peter Seewald, katika mahojiano ya kitabu kiitwacho “Nuru ya Ulimwengu” yaliyochapishwa miaka mitatu mapema, alikuwa kwa namna fulani amesema: “Wakati Papa anafikia ufahamu wazi wa kutokuwa na nguvu tena kimwili, kiakili na kiroho kutekeleza jukumu alilokabidhiwa, basi ana haki na katika baadhi ya mazingira pia ana wajibu wa kujiuzulu”. Ingawa katika maelezo yote ya utawala wake ilitarajiwa kwa heshima hadi mwisho wa maisha yake, ikiwa ni mfano wa kihistoria wa umuhimu mkubwa, ingekuwa kweli ukarimu kumkumbuka kwa namna ya pekee  Papa Mstaafu  Benedict XVI .

Taalimungu kijana katika Mtaguso

Mtoto wa Askari aliyezaliwa mnamo 1927, katika familia rahisi na ya Kikatoliki sana huko Bavaria, Joseph Ratzinger alikuwa mhusika mkuu wa Kanisa katika karne iliyopita. Alipewa daraja la Ukuhani pamoja na kaka yake Georg mwaka 1951, akawa daktari wa taalimungu miaka miwili baadaye na mwaka 1957 alipata sifa ya ualimu kama profesa wa taalimungu ya kweli. Alifundisha huko Freising, Bonn, Münster, Tübingen na hatimaye Regensburg. Pamoja naye anatoweka mmoja wa Papa aliyeshiriki binafsi katika kazi ya Mtaguso wa Pili wa Vatican. Akiwa mtaalimungu kijana sana na ambaye tayari alikuwa ameheshimika, Ratzinger alikuwa amefuatilia kwa karibu kikao hicho kama mtaalamu wa Kardinali Frings wa Cologne, karibu na mrengo wa kuleta mageuzi. Yeye ni kati ya wale wanaokosoa vikali mipango ya maandalizi iliyoandaliwa na Curia Romana, kisha ikafagiliwa mbali na uamuzi wa maaskofu. Kwa mtaalimungu kijana Ratzinger, katika maandiko yake:  “lazima  kutoa majibu katika maswali ya haraka zaidi na yanapaswa kufanya hivyo, iwezekanavyo, si kwa kuhukumu na kulaani, lakini kwa kutumia lugha mama”. Ratzinger anapongeza mageuzi yajayo ya kiliturujia na sababu za kutoweza kwake kubadilika. Anasema kwamba ili kugundua upya asili ya kweli ya liturujia ilikuwa ni lazima “kuongeza nguvu ukuta wa Kilatino”.

Mlinzi wa imani pamoja na Wojtyla

Lakini baadaye Benedikto XVI pia ni shahidi wa moja kwa moja wa mgogoro wa baada ya Mtaguso kwenye maandamano katika vyuo vikuu na vyuo vya kitaalimungu. Alishuhudia kuhojiwa kwa ukweli muhimu wa imani na majaribio yasiyo mazuri katika nyanja ya kiliturujia. Mapema mnamo 1966, mwaka mmoja baada ya kumalizika kwa Mtaguso alisema alivyoona maendeleo ya “Ukristo kwa gharama iliyopunguzwa”. Paulo VI mnamo  mwaka 1977 alimteua kuwa askofu mkuu wa Munich akiwa na umri wa miaka hamsini tu na wiki chache baadaye akamchagua kuwa Kardinali. Mnamo Novemba 1981, Yohane Paulo II alimkabidhi uongozi wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. Ni mwanzo wa ushirikiano mkubwa kati ya Papa wa Poland na Mtaalimungu wa Bavaria, ulimalizika tu kwa  kifo cha Wojtyla, ambaye hadi mwisho alikataa kujiuzulu bila kutaka kujinyima mwenyewe. Hii ndiyo miaka ambayo Ofisi Takatifu ya zamani iliweka nukta kwenye  katika mafunzo  mengi: hasa kwa kupunguza kasi ya Taalimungu  ya Ukombozi inayotumia uchanganuzi wa Umaksi na kuchukua msimamo mbele ya kuibuka kwa matatizo makubwa ya kimaadili. Kazi muhimu zaidi kwa hakika ni Katekisimu mpya ya Kanisa Katoliki, kazi iliyodumu kwa miaka sita, iliyopata mwanga mwaka 1992.

“Mfanyakazi Mnyenyekevu katika Shamba la Mizabibu”

Baada ya kifo cha Wojtyla, mkutano wa 2005 ulitoa wito wa kumrithi katika muda wa chini ya saa 24 mtu ambaye tayari ni mzee wa  umri wa miaka 78, aliyeheshimiwa na  ulimwenguni wote hata na wapinzani wake. Akiwa katika Balkoni ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Papa Benedikto wa kumi na sita alijionesha kama “mfanyikazi mnyenyekevu katika shamba la Bwana la  mizabibu ”. Kwa kutokuwa na kiumbelembele  alisema hana programu yoyote lakini alitaka “kusikiliza, pamoja na Kanisa zima, kwa neno na mapenzi ya Bwana”.

Huko Auschwitz na Regensburg

Hapo awali alikuwa na haya, lakini hakukata tamaa kusafiri, kwa mana hiyo haya hata upapa wake ulikuwa na ziara kama zile za  mtangulizi wake. Miongoni mwa nyakati za kugusa moyoni zaidi, ni ziara ya Auschwitz mnam Mei 2006, ambapo Papa wa Ujerumani alisema: “Mahali kama maneno haya yanashindikana, mwishowe kunaweza tu kubaki kimya cha kushangaza,  kimya ambacho ni kilio cha ndani kwa Mungu: Kwa nini uliweza kuvumilia haya yote?”. 2006 pia ni mwaka wa kesi ya Regensburg, wakati msemo wa kale kuhusu Mohammed ambapo Papa alinukuu bila kuupitisha katika chuo kikuu alichokuwa mwalimu msemo ukaja kuibua maandamano katika ulimwengu wa Kiislamu. Tangu wakati huo Papa alizidisha ishara za tahadhari kwa Waislamu. Benedikto wa kumi na sita alikabiliwa na safari ngumu, alikabiliana na mtafaruku wa huenezaji wa dini kwa jamii zisizo za Kikristo na upinzani ndani ya Kanisa. Alisheherekea siku yake ya kuzaliwa katika Ikulu ya Marekani (White House), pamoja na George Bush jr na siku chache baadaye, mnamo tarehe 20 Aprili 2008, alisali Ground Zero akiwakumbatia jamaa za aathrika wa Ugaidi wa mbamo tarehe 11 Septemba.

Waraka  juu ya upendo wa Mungu

Ingawa akiwa kama Mwenyekiti wa Zamani  Baraza la Kipapa la  Mafundisho Tanzu mara nyingi aliitwa “panzerkardinal”, kama Papa alizungumza mara kwa mara kuhusu “furaha ya kuwa Mkristo”, na akaweka wakfu waraka wake wa kwanza kwa Waraka wa “Deus caritas est” , yaani  upendo wa Mungu. “Mwanzoni mwa kuwa Mkristo hakuna uamuzi wa kimaadili au wazo kubwa, lakini kukutana na tukio, na Mtu”, aliandika. Alipata hata muda wa kuandika kitabu juu ya Yesu wa Nazareti, kitabu cha kipekee ambacho kilichapishwa katika vitabu vitatu. Miongoni mwa maamuzi ya kukumbukwa ni pamoja na Motu Proprio ambayo inatoa uhuru wa misale ya Kirumi kabla ya kutub na uanzishwaji wa uratibu ili kuruhusu jumuiya za Kianglikaia kurudi kwenye Umoja na Roma. Mnamo Januari 2009, Papa aliamua kuondoa kutengwa kwa maaskofu wanne waliowekwa wakfu isivyo halali na Monsinyo Marcel Lefebvre, akiwemo Richard Williamson, mkanushaji kwenye vyumba vya gesi. Mabishano yaliibuka katika ulimwengu wa Kiyahudi, Papa alichukua kalamu na karatasi na kuwaandikia maaskofu ulimwenguni kote akichukua jukumu lote.

Majibu ya kashfa

Miaka michache iliyopita imekuwa na mlipuko wa kashfa ya watoto na Vatileaks, uvujaji wa nyaraka zilizoibiwa kutoka katika dawati la papa na kuchapishwa katika kitabu. Benedikto wa kumi na sita amedhamiria na kuwa mgumu katika kukabiliana na tatizo la “uchafu” ndani ya Kanisa. Ameleta sheria kali sana dhidi ya unyanyasaji wa watoto, na kuwaomba Curia na maaskofu kubadili mawazo yao. Akweenda mbali zaidi na kusema kwamba mateso makubwa zaidi kwa Kanisa hayatokani na adui zake wa nje, bali kutoka na  dhambi zilizomo ndani yake. Mageuzi mengine muhimu ni yale ya kifedha: ni Papa Ratzinger ambaye alitanguliza kanuni za kupinga utakatishaji fedha haramu mjini Vatican.

“Kanisa lisilo na pesa na nguvu”

Mbele ya kashfa na taaluma ya kikanisa, Papa mzee wa Ujerumani aliendelea kutoa wito wa uongofu, toba na unyenyekevu. Wakati wa safari yake ya mwisho nchini Ujerumani, mnamo Septemba 2011, alialika Kanisa kuwa la kidunia kidogo: “Mifano ya kihistoria inaonesha kwamba ushuhuda wa kimisionari wa Kanisa”unajitokeza wazi zaidi. Likiwa huru kutoka katika mizigo na marupurupu ya kimwili na ya kisiasa, Kanisa linaweza kujitoa vyema zaidi na kwa njia ya Kikristo ya kweli kwa ulimwengu wote, linaweza kuwa wazi kwa ulimwengu kweli kweli…”.

31 Desemba 2022, 11:18