Tafuta

03-12-1963 Papa Paolo VI  na mababa wa Mtaguso 03-12-1963 Papa Paolo VI na mababa wa Mtaguso  

Miaka 59 ya Hati ya Sacrosanctum Concilium kuhusu Liturujia Takatifu

Mnamo tarehe 4 Desemba 1963,Mtakatifu Paulo VI alichapisha hati ya mtaguso kuhusu Liturujia Takatifu-Sacrosanctum Concilium.Katifa afla ya kumbukizi ya miaka 59,imeandaliwa Tafakari yenye mada:“Mitindo ya uwepo wa Kristo katika liturujia Sacrosanctum Concilium.'Mtaguso unaamini kushughulikia mageuzi na uhamasishaji wa liturujia'.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mtaguso mtakatifu unapendekeza kufanya maisha ya Kikristo kukua zaidi kila siku kati ya waamini; ili kukabiliana vyema na mahitaji ya wakati wetu zile taasisi ambazo zinaweza kubadilika; kupendelea kile kinachoweza kuchangia muungano wa waamini wote katika Kristo; ili kuimarisha kile kinachosaidia kumwita kila mtu kifuani mwa Kanisa. Kwa hiyo mtaguso unaamini kwamba lazima pia ushughulikie kwa namna ya pekee mageuzi na uhamasishaji wa liturujia. Hiki ni kifungu kilichoandikwa katika utangulizi wa katiba ya upyaisho juu ya Liturujia Takatifu - 'Sacrosanctum Concilium' iliyopitishwa kwa kura 2158 za ndio na 19 pekee za hapana na kuchapishwa na Papa Mtakatifu Paulo VI ,  mnamo tarehe 4 Desemba 1963. Na katika  fursa ya  kukumbu kumbu ya kufikisha miaka 59  tangu kuchapishwa kwa hati hiyo ya Mtaguso wa kitume kuhusu Liturujia Takatifu  itakayo adhimishwa tarehe 4 Desemba 2022, Taasisi ya Kipapa ya Liturujia kwa ushirikiano na Kituo cha Shughuli za  Liturujia, Kituo cha Kiliturujia cha Vincenti, Chama cha Maprofesa na Wasanii wa Liturujia, Shirika la  Watawa wa Wafuasi wa Mungu Mwalimu, pamoja na Ofisi ya  Kiliturujia ya Jimbo la Roma, wameandaa siku ya mafunzo yanayojikita na  mada: “Mitindo ya uwepo wa Kristo katika liturujia: Sacrosanctum Concilium”.

Mshauri wa Kituo cha Shughuli za matendo ya Liturujia(CAL),  Profesa Giuseppe Falanga, Mtaalimungu na mkufunzi wa Liturujia katika Chuo Kikuu cha Santa Croce jijini  Roma, ambaye aliandika na kuchapisha kitabu kiitwacho: ‘Schola Dominici Servitii.  Mchango wa Kituo cha matendo ya Kiliturujia (CAL) kwa harakati na upyaisho wa liturujia nchini Italia’ alihojiwa na mwandishi wa habari za Baraza la Maaskofu Italia ili kuelezea ni mitindo gani ya Kristo katika liturujia. Katika kujibu amerejea picha ya kiinjili ya Marta, ambaye katika fursa ya kutembelewa na Yesu baada ya kufiwa na kaka yao Lazaro, alikwenda kwa dada yake Maria na kumwambia: “tazama  Mwalimu yuko hapa anakuita”(Yh 11,28).

Kwa maana hiyo Profesa Falanga amesema katika liturujia ni kumbu kumbu ya kuonesha kwamba Mfufuka bado yupo hapa na anatuita kwa jina na kutualika kumjua katika Mwili ambao ni Neno na Mwili wake ambao ni Mkate, lakini bila kusahau mwili wake mwingine, ambao ni ule wa kikanisa, hasa katika ndugu wenye kuhitaji msaada. Kwa mujibu wa Profesa alisema kwamba hata tabia yetu lazima iwe ile ya Maria ambaye kwa kusikia hivyo aliamka haraka na kwenda kwake (Yh 11,29). Ni vizuri, katika hilo, Mtakatifu Ambrose alieleza vema anapoandika kuwa: “ Mimi ninakuona katika mafumbo, uwepo halisi hata katika ishara maskini tangu wakati ule ambao Bwana alipenda kusimika hema lake katikati yetu na kujifanya kupatikana kwa kila mtu ambaye anamtafuta kwa moyo wa dhati.”

Akijibu ni mapya gani yaliyoonekana katika Katiba ya kitume kuhusu: ‘Sacrosanctum Concilium’ yaani Liturujia takatifu alisema kwamba:  ya kwanza ni ukweli kwamba kulikuwa na katiba iliyowekwa kwa ajili ya liturujia takatifu, matunda ya kwanza ya Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican. Licha ya kubeba mambo mapya (fikiria, kwa mfano, maana ya ‘fumbo la Pasaka’ au thamani ya ‘kushiriki’ na dhana ya ‘sherehekea’), haukutaka “liturujia mpya”  kama wengine 'walivyo fafanua, lakini ukuaji mpya wa mti wa karne nyingi wa Kanisa aminifu kwa mapokeo. Kwa upande wa Profesa hisia ya jumla, inaonekana inaweza  kuwa chanya tu hata kama hali halisi ya binadamu daima ni kamilifu. Na liturujia ni 'opus Dei', yaani ‘Kazi ya Mungu’ katika maudhui yake ya wokovu lakini, katika sura zake za nje, ni 'opus hominis', yaani 'kazi ya mwanadamu'. Kwa hivyo, labda, bado ni mapema kufanya tathmini ya kazi iliyofanywa, na matunda yaliyokomaa ambayo yanaweza kuvunwa tu katika vizazi vichache.

Kwa mujibu wa muandishi akitaka kujua jinsi ambavyo katika katiba hiyo pia kuna aya ya matumizi ya Kilatino na lugha za kitaifa katika liturujia na kama imeleta mabadiliko , je ni yapi, Profesa amejibu kwamba: Ndio kwa sababu lengo lilikuwa kurudisha sherehe za kiliturujia kwenye 'usahili wa hali ya juu, ufupi na uwazi' uliozoeleka katika karne za kwanza. Ibada hizo zilikuwa zimeingizwa pole pole na kuelemewa na ishala na ishara daima zisizoeleweka zaidi. Hata matumizi ya lugha ya Kilatino, ambayo yalienea sana katika Kanisa na kuthaminiwa kama sehemu ya umoja na ushirika, kiukweli hayakuendana tena na wito wake, badala yake ilikuwa sababu ya kuvunjika na umbali kati ya ‘imani inayoadhimishwa’ na klero na 'imani ya kuiishi' kwa watu. Hata kiutamaduni, Kanisa lilibaki limesimama katika utaftaji wa lugha tasa, wakati lugha chafu (zinazoeleweka kwa idadi inayokua ya watu) zilivamia sio tu nyanja ya anayezungumza, bali pia lugha ya sayansi, sanaa, fasihi na teknolojia. Mababa wa Mtaguso, kwa hiyo, waliamua kukubali lugha za kitaifa (mahalia) ambazo, pamoja na ile ya Kilatino, zingependelea uelewekaji na ushiriki kwa wote.

Katika muktadha wa mafundisho yaliyomo katika liturujia, Profesa amebainisha kuwa Papa Mstaafu  Benedikto  XVI, katika Wosia wake wa Spe Salvi, yaani' Kuokolewa kwa matumaini, uliochapishwa mnamo tarehe  30 Novemba 2007, katika kifungu cha 2 chenye kichwa: Imani ni tumaini, Papaanaandika kwamba: 'Injili si mawasiliano tu ya mambo yanayoweza kujulikana (ya habari), bali ni mawasiliano ambayo huzalisha ukweli na kubadilisha maisha (ya utendaji).  Kwa njia hiyo, liturujia (sherehe ya imani yetu) ina thamani ya utendaji zaidi ya ile ya ufundishaji. Sio kucheza kwa maneno, lakini ni kusema kile kinachokamilishwa katika adhimisho la kiliturujia, ambapo tunaweza kusema kwamba kwetu sisi, kupitia lugha ya utendaji ya liturujia, sio tu 'tumeumbwa'(yaani, tumeinjilishwa), lakini zaidi ya yote, tumeundwa upya (yaani kufanywa kwa upya), 'kubadilishwa' kuwa Mwili wa Kristo ambao ni Kanisa, na hatimaye 'kufanana' na Kristo Bwana”.

Profesa baadaye amejibu jinsi  gani ya kuelimisha watu katika roho ya kiliturujia kwamba: kuelimisha kwa maoni yake, ni neno la utaratibu pia kwa liturujia kwa wakati huu. Kwa ajili hiyo Papa Francisko, mnamo tarehe 29 Juni 2022 amthibitisha kwamba  aliandika barua nzuri ya kitume, iitwayo: Desiderio desideravi, yaani, Nilitamani unataka unayohusu Mafunzo ya liturujia kwa Watu wa Mungu, ambamo ndani ya barua hiyo anamnukuu mara kadhaa  Romano Guardini.  Jambo muhimu kwa upande wa Papa ni kutaka kuelimisha kuelewa alama. Na njia ya kuifanya 'hakika ni kutunza sanaa ya kusherehekea', ambayo 'haiwezi kupunguzwa kwa uzingatiaji wa vifaa vya utengenezwaji na haiwezi hata kuzingatiwa kama ubunifu wa kufikirika, wakati mwingine wa bure, bila ubunifu wa sheria. Tamaduni yenyewe ni kawaida na kawaida sio mwisho wenyewe, lakini kila wakati katika huduma ya ukweli wa hali ya juu ambayo inataka kuhifadhi. (rej. kifungu 48).  Nia ya Papa Fransisko ni kuondokana na tabia za urasmi wa kiliturujia, lakini pia uzembe wa maadhimisho mengi na ili kugundua tena maana ya kina ya adhimisho la Ekaristi iliyoibuka kutoka katika Mtaguso. Papa hakutaka kutoa kanuni mpya, bali kusaidia kugundua umuhimu na uzuri wa maadhimisho ya kiliturujia katika maisha ya Kanisa na katika uinjilishaji, amehitimisha.

Liturujia Takatifu
01 December 2022, 15:53