Tafuta

2022.12.23 Kardinali Parolin alitembelea hospitali ya Bambino Gesù  kwa ajili ya Heri kwa watoto wadogo. 2022.12.23 Kardinali Parolin alitembelea hospitali ya Bambino Gesù kwa ajili ya Heri kwa watoto wadogo.  

Kard.Parolin kwa mgonjwa wa Gesù Bambino:uchungu wa watoto wadogo hauna majibu

Kama ilivyo kwa kila Noeli katibu wa Vatican hupeleka salamu na baraka za Papa Francisko kwa wagonjwa wa hospitali ya Vatican.Kwanza alitembelea kitengo cha ugonjwa wa kimetaboliki ambapo alikutana na Sophie na watoto wengine waliolazwa hospitalini,baadaye akafanya mazungumzo na madaktari na wafanyakazi kwa kuwatia moyo kuwa wajisikie washirika wa Papa katika upendo.

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

Katikati ya vita isiyo na matarajio ya suluhisho, mchango wa wahudumu wote  ni mdogo  na wenye thamani katika ujenzi wa amani, alisema Kardinali Parolin Katibu wa Vatican, ambaye kama kila Noeli kwa niaba ya Papa hufika kuwapelekea salamu na baraka katika hospitali ya Kipapa ya Bambino Gesù. Katika kuwazungukia wagonjwa hao wadogo wakiwa na wazazi wao, mnamo tarehe 23 Desemba 2022, Mwanamke mmoja alikamkaribia Kardinali Pietro Parolin kwa kuuliza swali akiwa amevalia barakoa, huku ananong'ona ambapo kila mzazi hapaswi kamwe kuuliza anapomwona mtoto wake katika kipindi cha  Noeli  hayupo nyumbani, akiwa na taa za kitandani amefungwa kwenye mipira na harufu za kujikinga. Swali lilikuwa: “Lakini, kwa maoni yako, yote haya yana maana? Kwa nini mtoto wangu anateseka?  Kwa upande wa Sophie ugonjwa wake ni nadra ya neva, ambapo mtoto amekuwa akiugua tangu kuzaliwa kwake. Hapakuwapo na hasira au ubishi katika maneno ya mwanamke huyo, ambaye alikuja Roma kutoka Benevento, Italia ili kumtunza binti yake, lakini utafutaji wa dhati wa maana ya historia  hii ambayo yeye na familia yake wamekuwa wakiishi kwa miaka ndio ilimfanya kuuliza swali  Kardinali akitegemea labda apate jibu.  Naye Katibu wa Vatican  alimkaribia na pia kupunguza sauti yake na kusema kwamba: “Uchungu usio na hatia hauwezi kueleweka. Hauhalalishwi sababu zake. Mambo haya hayatokei kwa bahati mbaya, kuna hisia… Tunajua kwamba kuna mtu mkubwa kuliko sisi.”

Mchango wa amani duniani ili iwe bora

Huu ni wakati wa ukaribu na wa hiari na mwanamke huyo kijana  ambaye aliweza kufanya atafakari sana wakati wa ziara yake  karibu kwa saa tatu ambazo Kardinali alikaa  Hospitali ya Watoto ya Bambino Gesù,  ili kupeleka, kama desturi, na utamaduni wa  salamu za Noeli kwa wagonjwa wadogo, lakini pia kwa madaktari, wauguzi na wafanyakazi wote.  Kwa mujibu Kardinali Parolin aliwambia kuwa wao ni washirika na Papa, katika shughuli za upendo mkuu akisisitiza kwamba kazi inayofanywa kwa watoto hao haiishii ndani ya kuta za hospitali, lakini ni hatua ndogo lakini thabiti ambayo inaelekeza amani ya kimataifa. “Leo hii sote tuna wasiwasi kuhusu kinachoendelea duniani, hatuoni uwezekano wa kupata suluhisho la vita hivi vinavyoendelea nchini Ukraine kwa mwaka mmoja sasa, lakini pia kwa migogoro mingine mingi duniani. Hali ni hatari sana”, Kadinali Parolin alisema. Kwa kuongezea alithibitisha kuwamba “Kwa hivyo mtu anaweza kusema ninaweza kufanya nini kubadilisha hali hiyo? Kwa upande wa jibu lake  anaamini kuwa tunachopaswa kufanya “ni wajibu wetu na kukifanya kwa uaminifu na ukarimu mkubwa kisha kila mmoja wetu atoe mchango wake mdogo lakini mkubwa katika kujenga ulimwengu  uweze kuwa bora”.

Ziara ya watoto

Kardinali Parolin alikuwa na uthibitisho wa mchango huu mdogo lakini mkubwa, unaofanywa kwa kujitolea kila siku, kwa kutembelea Kitengo cha Magonjwa ya mfumo wa chakula mwanzoni mwa ziara yake hapo Hospitalini huku akiandamana na Mwenyekiti wa Hospitali hiyo Bi Mariella Enoc, mkurugenzi wa matibabu Massimiliano Raponi na mkuu wa kitengo hicho  Profesa Carlo Dionisi Vici. Katika vyumba hivyo vilivyopambwa na taa za Noeli na eneo la Pango ndogo ya kuzaliwa kwa Bwana Kardinali alikutana na Cecilia, Sofien, Dariana Victoria, Yassmine na Sophie. “Wanasema watoto hawa ni kama Yesu msalabani anayeteseka. Sijui kama ni kweli, lakini inatufariji ...”, alifichua mama Concetta, akieleza kwamba anataka kutoka ndani ya Hospitali kabisa ikiwezekana tarehe 28 Desemba kwa sababu ya kutaka kuungana na mtoto wake mwingine mwenye umri wa  miaka 11 na mume ambaye pia anahitaji huduma maalum. Kwa maana hiyo aliuliza swali: “Tufanye nini katika haya, tafadhali? “Ndio, tujikabidhi kwa Bwana,” alijibu Kardinali Parolin, ambaye, baada ya kumshika  bega mtoto aliyelala, aliweka kadi ya Noeli kwenye mto wake na kusema “ ni zawadi kutoka kwa   Papa”.

Marafiki wa zamani

Katika kitanda kingine ni Yassmine: ‘Gelsomino’, aliyekuwa amevalia ushungi wa kiislamu ambaye mara moja alisema “wao wanatoka mbali”. Msichana mdogo, aliyezaliwa Italia, alikuwa mgonjwa tangu alipokuwa na umri wa siku 3. Aliingia kwa kasi katika hali ya kukosa fahamu, alikuwa kwenye vipimo vya damu. Katika mwaka mmoja na miezi 3 alifanyiwa upandikizaji wa ini. Anajitahidi kuongea na pia anaweza kwenda shule ya chekechea, wakati huo huo akikabiliana na matibabu kwa wiki nzima. Sasa ameunganishwa kwenye mirija na amekuwa na hitilafu katika siku chache zilizopita. Kwa hivyo alirudi katika hospitali hiyo ambayo inamwona kama rafiki wa zamani. Kama yeye, mtu anayemjua zamani ni Dariana Victoria, labda yeye kidogo historia pia ni ya  kuhuzunisha zaidi kati ya zile zinazoonekana hapo kwa Kardinali. Alikuwa mtoto wa kike. Karibia  umri wa miaka 5, anaathiriwa na ugonjwa wa kupungua, (Pearson's Syndrome).  Yeye anakula kwa kutumia mpira na wakati huo ana kisukari, walithibitisha madaktari. Akiwa na wazazi wake na ndugu zake, Victoria alikuja kutoka nchini Venezuela  kwa matibabu maalum. “Venezuela!” Kardinali Parolin alishangaa.  Ni kwa sababu Kardinali mara moja alikumbuka miaka ya uwakilishi  kama Balozi wa Vatican nchini Venezuela. “Wavenezuela wana mioyo mikuu alisema  Kardinali, akielekeza mikono yake mtoto huyo.

Hata mazungumzo  na mbwembwe hizi ndogo husaidia kuonesha ukaribu huo na Papa ambapo Kardinali Parolin aliubeba. Pamoja na wagonjwa, juu ya yote, lakini pia na mama wengi karibu na kitanda cha watoto wao. Kwa hiyo kuna pia Cecilia,  ambaye kila mara anacheza vichekesho. Au hata mama wa Sofien, Mwitaliano-Moroko, ambaye aliingia hospitali ya Vatican kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa siku 14. Kwa sasa ana umri wa miaka 14. Katika miaka minne atakuwa na miaka 18 na ataingia ulimwengu wa dawa za watu wazima. Kwa 'kesi' kama yake, hata hivyo, kuna ukosefu wa miundo yenye uwezo na vifaa vya kufuatilia aina hiyo ya ugonjwa, madaktari wengine wanalalamika kwamba “Tunahitaji dawa ya mpito na mifumo ya umma”, kwa kumwambia  katibu wa Vatican.

Kuponya, lakini juu ya yote kuponya

“Watoto wengine hawaponi kabisa, lakini bila shaka wanaponywa,” alisema daktari. Maneno hayo yalibakia kichwani mwa kadinali ambaye aliyarudia muda mfupi baadaye, wakati akikutana na madaktari wakuu na wafanyakazi wa hospitali waliounganishwa katika  kupeana matashi mema kwenye Banda la Salviati (kwa jina la familia ya mwanzilishi wa Hospitali ya Gesu Bambino): kufanya kila kitu kuponya lakini zaidi ya yote tiba, ambayo ina maana pia kusimama karibu nao. Madaktari wa Bambino Gesù wamekuwa wakifanya hivyo kwa zaidi ya miaka 150, alikumbusha Mariella Enoc: “Ni hospitali ya 'watoto maalum'. Tunahitaji kuwajua sio kwa namba na karatasi za usawa ambazo ni chanya lakini kwa ajili ya  utume tunaofanya, kwa wanadamu waliolazwa hospitalini hapa. Mara nyingi tunashughulikia mahitaji ambayo yanaonekana kuwa ya pemebeni lakini badala yake yanabadilisha maisha ya familia”.

Daima Kardinali Parolin aliwakumbusha kuwa wao ni washirika na Papa wakati akiwasifu madakatari wote  kuwa: “Hapa upendo wa Papa unatekelezwa kwa wagonjwa na zaidi ya wale wote ambao ni wahitaji zaidi na ambao tunajisikia hasa katika shida”. “Je huko wapi uovu wa watoto, uchungu wa watoto, uchungu usio na hatia?” Kardinali Parolin anauliza. “Hili kimekuwa ni swali ambalo ubinadamu umekuwa ukijiuliza tangu ulipoanza kutafakari kidogo. Na hatuwezi kutoa majibu... Inabakia kuwa fumbo kuu la maisha lakini hata hivyo, tunachoweza kufanya ni kusimama karibu  kama Msamaria katika mfano na kuponya. Kiukweli tujisikie kama washirika na Papa katika utume”. Na hata zaidi  kutokana na kwamba hata Papa anajua kuwa kuna watu  kwa niaba yake ambao  hujisikia kama washirika na Bwana katika kutunza wale wanaohitaji”.

24 December 2022, 22:00