Papa alikutana na mke na mtoto wa mfungwa wa vita huko Ukuraine
Na Angella Rwezaula;– Vatican.
Larissa na Sergheij walimpatia Baba Mtakatifu Francisko Kalenda moja ya 2023, Jumatano asubuhi tarehe 21 Desemba 2022, yenye picha za kutisha za uharibifu kutokana na vita nchini Ukraine. Mama na mtoto wake, ambao walikaa kwa muda na Papa katika Ukumbi wa Paulo VI, baada ya katekesi yake, hawa ni mwanamke na mtoto wake, ambapo baba wa mtoto ni mfungwa wa vita nchini Ukraine. Papa alitumia muda kufununua picha hizo za kutisha, moja baada ya nyingine. Ni picha za uharibifu na za kuhuzunisha zikitoa ushuhuda kamili wa mkasa wa wakazi wa Mariupol, jiji lililo haribiwa kishahidi Kusini-mashariki mwa nchi, kwa miezi kadhaa huku likizingirwa na jeshi la Urussi.
Kalenda yenye neno Azovstal
Ikiwa imepambwa kwa neno la ‘Azovstal’ katika kumbukumbu ya upinzani wa Kiukreni ndani ya kiwanda cha kutengeneza chuma, kalenda hiyo pia inawakilisha ishara ya matumaini kwamba 2023, inaweza kuwa mwaka wa amani kwa ajili ya Ukraine. Larissa pia alimkabidhi Papa orodha ya majina ya wafungwa wa Kiukreni, kwa matumaini kwamba inawezaekana kuwezesha kuachiliwa kwao, au angalau kuboreshwa kwa hali zao kizuizini. Hata hivyo idadi kamili ya wafungwa wa vita wa Kiukreni haijulikani, lakini kati yao ni mume wa Larissa, baba yake Sergheii. Pamoja na kalenda hiyo pia kuna picha ya Maria katika shajara yenye ramani ya Ulaya na glovu za ndondi za baba, pia walimpatia Papa Francisko kitambaa cha kiutamaduni kilichopambwa, kama ishara ya kutaka kutunza wengine.
Pambo la mabua ya ngano
Aliye wasindikiza Larissa na Sergheii alikuwa mke wa balozi wa Ukraine anayewakilisha nchi yao mji wa Vatican, Bi Diana Yurash, ambaye alimpatia Papa Francisko zawadi ya pambo la kawaida la Noeli lililotengenezwa kwa mabua ya ngano. Haya “Ni mabua ya mwisho yaliyokusanywa kwenye mashamba ambako sasa kuna mabomu na mabomu ya ardhini,” kwa maelezo ya Irina Skab, msaidizi katika Ubalozi huo.
Sala ya Papa Francisko kwa ajili ya amani
Ndugu wasilikilizaji wa Radio Vatican tutakumbuka vema kwamba tarehe 8 Desemba wakati wa Siku kuu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili, kwa mara nyingine tena, baada ya vizuzi vya uviko -19, Papa aliweza kutimiza tukio la kiutamaduni, kwenda kwenye uwanja wa Hispania, Roma mahali ambapo akiwa chini ya Sanamu iliyoko kwenye kinara kirefu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili alisali sala ya kina. Wakati anasalia, kwa kufikiria machungu yanayoendelea kuwakumba watu, na mateso alitokwa hata machozi na kwikwi. Leo hii basi nasi kwa pamoja turudie kuisikiliza sala hiyo ya Papa isemayo:
Mama Yetu Mkingiwa, leo watu wa Roma wanakusanyika kwako. Maua yaliyowekwa kwenye miguu yako na hali halisi ya uzalendo inayoeleza upendo na ibada kwako ambaye unakesha kwa ajili yetu sote. Wewe unaona na kupokea hata maua yasiyoonekana ambayo ni maombi mengi, maombi mengi ya kimya, ambayo wakati mwingine yamesongwa, yamefichika lakini si kwako, ambaye ni Mama. Baada ya kuja miaka miwili kukuheshimu tu katika mapambazuka ya siku, leo hii nimerudi kwako pamoja na watu wa Kanisa hili na Mji huu. Ninakuletea shukrani zangu na maombi ya wana wako wote, wa karibu na mbali. Wewe huko mbinguni ambako Mungu alikupokea, unatazama mambo ya dunia vema kuliko sisi; lakini kama Mama sikiliza maombi yetu, ili uyawakilishe kwa Mwanao, katika moyo wake uliojaa huruma. Awali ya yote ninakuletea upendo wa kimwana wa wanawake na wanwaume wengi, na sio tu wakristo, ambao wanamwilishwa kwako utambuzi mkubwa sana, kwa ajili ya uzuri wako wote wa neema na unyenyekevu: kwa sababu katikati ya mawingu meusi, wewe ni ishara ya tumaini na ya faraja.
Ninakuleta tabasamu za watoto, ambao wanajifunza jina lake mbele ya picha yako, wakiwa kwenye mikono ya mama yao na bibi zao, na wanaanza kujua kwamba wanaye hata Mama wa Mbinguni. Na ikitokea kwamba katika maisha zile tabasamu zinaacha nafasi ya machozi, ni jinsi gani ilivyo muhimu kukutambua wewe na kuwa na zawadi ya umama wako! Ninakuleta shukrani za wazee na watu wazima: neema ambayo inafanya kitu kimoja kwa maisha yao, kiungo cha kumbu kumbu, cha furaha na uchungu, cha matarajio ambayo wao wanatambua vizuri ya kwamba wamefikia kutokana na msaada wako, kwa kushikiliwa mkono kwa mkono wako.
Ninakuletea mahangaiko ya familia, ya mababa na mama ambao mara nyingi inakuwa ngumu kuweka mzani sawa wa nyumba, na kukabiliana siku kwa siku changamoto ndogo na kubwa ili kwenda mbele. Kwa namna ya pekee ninakukabidhi wenzi vijana kwa sabababu ya kukutazama wewe na Mtakatifu Yosefu, wanaweza kwenda kukabiliana na maisha kwa ujasiri, kwa kuamini katika Mungu mpaji. Ninakukabidhi ndoto na wasi wasi za vijana, waliowazi katika wakati ujao lakini wakisimamishwa na utamaduni tajiri ya mambo na maskini wa thamani, wakijazwa pomoni na habari na kushuka kwa elimu, wenye kushawishiwa katika kudanganya na wasio na huruma katika kukatisha tamaa. Ninakukabidhi hasa vijana ambao wamehisi zaidi janga la uviko, ili pole ple waweze kuinuka na kuanza kufungua mabawa yao na kupata thamni ya kweli ya juu.
Bikira Mkingiwa, nilitaka leo hii nikuletee shukrani kwa watu wa Ukraine kwa sababu ya amani ambapo kwa kipindi kirefu tunaomba kwa Bwana. Kinyume chake bado tena ninawakilisha maombi ya watoto, wazee, mababa , mama na vijana ambao wanateseka katika ardhi ile. Lakini kiukweli sisi tunaelewa kwamba wewe huko na wao wanaoteseka wote, hivyo kama ulivyokukuwa karibu na mtoto wako msalabani. Asante Mama Yetu! Kwa kukutazama wewe, usiye na dhambi, tunaweza kuendelea kuamini na kutumaini kuwa chuki inashindwa na upendo, ukweli unashinda uongo, msamaha hushinda mkosaji, na amani inashinda vita. Na iwe hivyo.