Kard.Krajewski:Ugumu wa kuvuka mpaka&Noeli pamoja na waukraine
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Hatimaye baada ya siku tatu Msimamizi wa Sadaka ya Kitume ya Papa alisimama Lviv nchini Ukraine kwa mujibu wa maelezo ya Kardinali Konrad Krajewsk mwenyewe, akizungumza kutoka mji wa Magharibi mwa Ukraine alikofikia baada ya kusafiri kutoka Poland na mzigo wa jenereta na masweta maalum ya joto ambapo vyote hivyo vilivyotolewa kwa ajili ya wakazi wanaoteseka sana kwa zaidi ya miezi tisa ya migogoro wa kivita na Urussi. Kwa upande wake Kardinali alisisitiza ilivyokuwa ngumu sana kuvuka mpaka, akibainisha kwamba hata alilazimika kupanga foleni kwa kilomita 25 mpakani.
Katika kuwakilisha ujumbe wa mshikamano na watu wa Ukraine Kardinali Konrad Krajewski, Msimamizi wa Sadaka ya Kipapa ilibidi akabiliane na foleni ndefu kwenye mipaka, na baridi ya msimu wa baridi na giza la kulazimishwa kwa sababu ya kukatika kwa umeme nchini kote huko. Na baada ya kusimama huko Lviv, wanaendelea kuelekea mji mkuu wa Kyiv, ambapo atakuwa huko katika siku kuu ya Noeli.
Kardinali amebainisha alivyosimama na kukutana na maskini, kutoa baraka za Baba Mtakatifu, na kutuma salamu za heri. Kama Mwenyekiti wa Huduma ya Upendo, Kardinali Krajewski ataendelea kuonesha upendo huo katika vitendo, kuusambaza kwa bidii. Na alisema kuwa anakwenda Kyiv kuwa huko katika siku kuu ya Noeli. Watu wengi hawana mwanga na joto. Uaminifu wake kwa dhamira ya kutowaacha watu peke yao ni ya juu zaidi. Maelfu na maelfu ya nguo zinazosaidia kuishi katika wakati huu mgumu sana zimekusanywa na alitaka kuwa mdhamini, kwamba kila kitu walichokuwa wamekusanya nchini Italia kitahamishwa mara moja.
Shukrani kwa njia za kikanisa, masweta yalifika mahali yalipohitajika bila matatizo makubwa. Jenereta zilikwenda katika maeneo ya Odessa, Zaporizhzhia, Kharkiv. Wakati unaofaa unaotii mtindo wa kibinafsi na bidii, lakini unaopata kichocheo chake kikuu kwa usahihi katika Injili, kama Kadinali mwenyewe anavyosema: “Injili inazungumza ya leo huu kwamba telemka kutoka kwenye mti na uende nyumbani, sio wiki, lakini leo hii. Kwa hiyo nilikuwa nikitafuta hii leo ya Injili nchini Ukraine”.
Ndugu Alois huko Kyiv na Leopoli,kukutana na vijana na wahusika wa makanisa
Ndugu Alois Mkuu wa Jumuiya ya Taize amekwenda naye Kyiv na Leopoli, ili kukutana na vijana na wahusika wa Makanisa. Kwa mujibu wa Habari za Kanisa Katoliki Italia (SIR) limebainisha amefika kuonesha mshikamano wao katika jaribio hilo la kutisha. Ndugu Alois kwa siku tano, atatembelea viongozi wa Kanisa na kukutana na vijana katika miji ya Kiev na Lviv, ambako atasali nao katika Siku Kuu ya Neoli kwa mujibu wa kalenda ya Gregorian.
Vijana 300 watashiriki mkutano huko Rostock
Kwa mujibu wa Jumuiya ya Taizé ilitangaza kuwa “Katika miaka ya hivi karibunivijana wengi wametoka Ukraine kuja Taizé na kwenye mikutano ya Ulaya. Takriban vijana 300 kati yao watakuwepo kwenye mkutano wa vijana huko Rostock, unaoanadaliwa kila mwishoni mwa mwaka kwa sehemu mbali mbali za Ulaya, lakini wengi wap hawataweza kufika kwa sababu ya vita. Kwa maana hiyo Ndugu Alois amesema ametaka kwenda kukutana nao ili kueleza mshikamano wao katika adha hii mbaya sana.