Tafuta

2022.12.08 Kardinali Konrad Krajewski - Mkuu wa Sadaka ya Kipapa ametembelea Ischia, Italia. 2022.12.08 Kardinali Konrad Krajewski - Mkuu wa Sadaka ya Kipapa ametembelea Ischia, Italia. 

Kard.Krajewski huko Ischia:ukaribu na faraja kwa wenye uchungu!

Mwakilishi wa Papa wa Baraza la Kipapa la Upendo ametembelea familia zilizokumbwa na mkasa wa maporokomo mnamo tarehe 26 Novemba 2022 na kusababisha vifo vya watu 12 huko kisiwani Ischia Italia.Kwa mujibu wake amesema wote wamepokea faraja ya Papa ambaye aliwatumia rozari iliyobarikiwa naye.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Maumivu hayawezi kuondolewa lakini yanaweza kuvumiliwa pamoja. Kardinali Konrad Krajewski, aliyetumwa na Papa  kwenda Ischia baada ya maporomoko ya ardhi yaliyogharimu maisha ya watu 12, ametoa wazo hilo baada ya kutembelea baadhi ya familia zilizofiwa na ndugu zao. Kwa sauti yake ya utulivu, anajua jinsi ambavyo amepeleka faraja ya Papa Francesco, kwa wafiwa na kwamba kwamba amesikiliza machungu ya wale waliopoteza wapendwa wao na hasa wajukuu zao. Akielezea juu ya tukio hilo, Kardinali amesema kwa kufanya ziara hiyo katika siku kuu ya Mkingiwa dhambi ya Asili kuna maana fulani. Katika nyuso za bibi, shangazi na wanawake alisema ameona mateso ya Maria aliyefiwa na mtoto wake, Yesu ambaye aliandamana naye hadi pumzi yake ya mwisho.

Majeneza yenye miili ya watu waliokuf kutokana na maporomoko huko kisiwani Ischia,Italia
Majeneza yenye miili ya watu waliokuf kutokana na maporomoko huko kisiwani Ischia,Italia

Kwa hiyo Kardinali Krajewski alibusu mikono ya wanawake hao, hivyo kushiriki katika jeraha hilo, ambalo lilifunguliwa ghafla mnamo Novemba 26 iliyopita wakati mto wa ardhi na matope yake yalishuka kutoka Mlima Epomeo. Familia ya kwanza ambayo kadinali huyo aliitembelea ilikuwa ya jamaa za Valentina Castagna na Gianluca Monti, wazazi wa Michele, Francesco na Maria Teresa ambao walikuwa na umri wa miaka sita tu. Sala, na  rozari iliyotolewa na Papa, baraka za Kardinali zilikuwa ni nyakati za hisia ya nguvu  ya ziara hiyo  ya busara lakini iliyojaa ukaribu wa Kanisa na Papa Francisko.

Misa ya mazishi ya watu waliokufa huko Ischia kutokana na maparomoko
Misa ya mazishi ya watu waliokufa huko Ischia kutokana na maparomoko

Mara tu baada ya wakati mwingine wa kugusa, sana kusimama katika Kanisa la Annunziata, huko Lacco Ameno, ambapo miili ya waathirika  wengine imehifadhiwa. Kardinali Krajewski alisali mbele ya jeneza jeupe la mwathirika mdogo zaidi wa janga hilo. Giovangiuseppe alikuwa na umri wa siku 22 tu na alizaliwa mnamo Novemba 4. Maporomoko ya ardhi yalimchukua pamoja na wazazi wake Maurizio Scotto na Giovanna Mazzella. Tarehe 7 Desemba mazishi ya Eleonora Sirabella na Salvatore Impagliazzo yalifanyika ambao ni ya wachumba. Na  Mazishi ya Maria Teresa Arcamone, mwanamke mwenye umri wa miaka 31 aliyepatikana wa mwisho, na Nikolinka Gancheva Blangova yanasubiriwa. Kwa mujibu wa Kardinali alisema wengi walimuuliza kwanini  hilo limetoke  na  alijibu kwamba yeye hana jibu kwa sababu hatujuhi siku wala saa, bali ni kuwa na tumaini tu katika ufufuko. Kwa bahati amesema, walio wengi wanaamini na kumtumaini Mungu ambalo ni jambo zuri kutoka kwa hazina ya imani, ana  uhakika, wanaweza kuanza  kwa upya.

Tetemeko la ardhi katika kisiwa cha Ischia mnamo 2015

Kardinali Krajewski, tayari mnamo Desemba 2015, alikuwa amekwenda kwenye kisiwa hicho Ischia, miezi 4 baada ya tetemeko la ardhi la daraja la nne katika kipimo cha Richter, tena kwa agizo la Papa Francisko. Tetemeko hilo lolisababisha vifo vya watu wawili na kuharibika kwa majengo mengi ya watu yakiwemo ya Casamicciola, Lacco Ameno na Forio, yenye karibu watu 2,500 waliokimbia makazi yao. Baadaye Msimamizi wa sadaka ya Kitume alikutana nao, akisikiliza historia zao ngumu na kwa kupeleka mkumbatia kwao kutoka kwa papa Francisko.

Kikosi cha waokoaji huko Kisiwani Ischia
Kikosi cha waokoaji huko Kisiwani Ischia
08 December 2022, 16:49