Umetengenezwa mfumo pacha wa kidijitali katika Kanisa kuu ili kufuatilia muundo wake
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Kuchora ramani na kuzichambua picha katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa kutumia teknolojia za kidijitali na kuifanya iweze kuwa mada ya ufuatiliaji wa siku zijazo: ni mpango unaotumia teknolojia ya juu ya kampuni ya uhandisi ya Nguzo ya Miundombinu ya Kikundi cha Reli cha Taifa la Italia, ambayo imeruhusu kuundwa kwa pacha hizo za kidijitali za Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican. Utafiti huo, uliofanywa kwa ushirikiano na Fabbrica di San Pietro, ambao ulichukua hatua zake za kwanza mnamo Julai na Agosti 2022, na ulipofungwa kwa umma na vipimo vya kwanza vilihitaji kukusanya zaidi ya takwimu 3.1 terabytes.
Awamu ya kwanza ya uchunguzi ilihitaji masaa 18 za kupiga picha, ndani na nje, kwa kutumia ndege isiyo na rubani na puto la hewa moto, picha 15,000 kwa (Giga Pixels 630) zilizopatikana, miezi 2 ya uchunguzi na miezi 2 kwa ufafanuzi wa maendeleo ya mitindo ya habari ya BIM. Hatimaye, wiki 2 za usindikizaji na usimamizi wa takwimu hizo kwenye jukwaa la pamoja. Hizi ndizo idadi ya uzinduzi wa mpango changamano ambapo teknolojia ya hali ya juu na uwekaji digitali hupatikana mchanganyiko wa sanaa, imani na utamaduni unaolindwa na Kanisa Kuu la Vatican.
Ndani ya takwimu za Pacha ya Kidijitali (Digital Twin) ya Kanisa Kuu kutakuwapo na takwimu zinatolewa hata kwenye Mfuko wa Mtakatifu Petro (Fabrica di San Pietro) iitwao mpango wa kuthibiti wa siku zijazo katika huduma ya Kanisa Kuu. Kwa njia ya hatua kwa hatua maalum ya hesabu, itawezekana kuchunguza uwezo wa kukabiliana na kazi kwa ajili ya matatizo ya utulivu ya nguvu, kuwa na ujuzi kamili wa hali ya afya ya miundo na kuendelea na muundo wa mfumo wa kudumu wa ufuatiliaji wa miundo. Ili kusaidia mpango huo , chombo hicho cha Italferr kimeshirikiana na kampuni zilizo na ujuzi sana kama vile Italdron Air Service Srl, inayoungwa mkono na CAD Connect, kwa ajili ya shughuli za uchunguzi katika nyanja hiyo, na Sacertis Ingegneria s.r.l kwa kubuni mfumo wa ufuatiliaji. Mpango utaoneshwa kwa umma mara tu awamu ya kwanza ya ukusanyaji wa data itakapokamilika.