Papa Montini -Papa Paulo VI Papa Montini -Papa Paulo VI  Tahariri

Barua ya Papa Francisko na ya mtangulizi wake Paulo VI

Mnamo mwaka wa 2018, katika kitabu kilichohaririwa na Mons. Leonardo Sapienza, kinaelezea barua ambayo mnamo 1965 Papa Montini alikuwa ameeleza kwamba angejuzulu upapa wake ikiwa ugonjwa mbaya au kizuizi kingine kikubwa kingemzuia kutekeleza majukumu yake kikamilifu kwa ajili ya wema wa Kanisa.

Na ANGELLA RWEZAULA, - VATICAN

Francisko ni kama Paulo VI. Katika mahojiano na gazeti la Uhispania la ABC, Papa alitaka kuonesha wazi  kwamba anaishi kama mtangulizi wake wa Brescia ambaye Yeye mwenyewe alimtangaza kuwa mtakatifu. Na alisema kwamba alimpatia Katibu wa Vatican wa wakati huo, Tarcisio Bertone barua ya kujiuzulu ikiwa ni katika "kizuizi cha kiafya". Hatujui tarehe kamili ya hati hiyo, lakini kumbukumbu ya Bertone kama Katibu wa Vatican inajikita katika miezi ya kwanza ya upapa, ikizingatiwa kwamba tayari mnamo Oktoba 2013, Kardinali Pietro Parolin alikuwa amechukua jukumu la mshiriki mkuu wa Askofu wa Roma. Ishara ya Francisko inafuata ile ya Papa Montini. Mashuhuda kadhaa katika miongo kadhaa iliyopita walikuwa wamezungumzia kuhusu barua za Paulo VI za kujiuzulu, lakini hadi mwezi Mei 2018 hazikuwa zimetolewa kwa umma. Aliyekuwa Mwakilishi wa Nyumba ya Kipapa, Monsinyo Leonardo Sapienza, msomi wa maandiko ya Papa Montini na mwandishi wa vitabu vingi vya Papa wa Brescian ambaye aliongoza Kanisa kuanzia  1963 hadi 1978, ambaye alikamilisha Baraza la Kiekumene, la Mtaguso wa II wa Vatican na miaka kumi na tatu ya kwanza ya matumizi yake, ndiye anaandika katika  Kitabu ambacho kina hati hizo za Paulo VI kinachoitwa: “Mtumbwi wa Paulo” (Toleo la Mtakatifu Paulo).

Katika kurasa hizo tunasoma: “Sisi, Paulo VI ... tunatangaza, katika hali ya udhaifu, ambayo inachukuliwa kuwa isiyoweza kupona, au ya muda mrefu ... kujiuzulu katika ofisi yetu”. Barua hiyo iliandikwa kwa maandishi ya wazi kabisa ya Papa Montini na ni ya tarehe 2 Mei 1965 na kwa hiyo iliandikwa kwa mkono na Papa wa Brescia sio kwamba alipokuwa mzee au mgonjwa, lakini miaka miwili tu baada ya kuchaguliwa kwake, huku Mtaguso ukiwa bado umefunguliwa. Kwa andiko hilo, Papa anataka kulilinda Kanisa kutokana na udhaifu wake wa muda mrefu: barua ya kujiuzulu mapema, ambayo kwa hali hiyo ilikuwa imekabidhiwa kwa Kadinali decano ili aweze kuwajulisha makadinali wengine, kuwa na uwezo wa kutangaza juu ya Papa. Barua za Papa Montini kiukweli zilikuwa mbili, kwa sababu pamoja na ile ya kujiuzulu kuna barua inayoambatana kwa kuelekeza kwa Katibu wa Vatican ambayo kwa hakika inawakilisha maandishi yenye nguvu zaidi. Na ni muhimu kwamba waraka huo pia ulitolewa maoni yake na Papa Francisko, ambaye katika mchango uliochapishwa katika kitabu kilichohaririwa na Sapienza anaandika: “Nilisoma kwa mshangao barua hizi za Paulo VI ambazo zinaonekana kwangu kuwa ushuhuda wa unyenyekevu na wa kinabii wa upendo kwa Kristo na kwa ajili ya Kanisa lake; na uthibitisho zaidi wa utakatifu wa Papa huyu mkuu… Kilicho muhimu kwake ni mahitaji ya Kanisa na ya ulimwengu. Na Papa anayezuiliwa na ugonjwa mbaya sana  hawezi kutekeleza huduma yake ya kitume ipasavyo”.

Maandishi ya barua kuu ‘ni ya siri’ na kuelekezwa kwa Dekano ambaye ni Mkuu wa Makardinali , kwenye karatasi yenye moto wa  upapa, inafunguliwa kwa maneno haya: “Sisi Paulo wa sita, kwa Maongozi ya Mungu Askofu wa Roma na Papa wa Kanisa la ulimwengu wote, mbele ya Utatu Mtakatifu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, anayeombwa kwa  jina la Yesu Kristo, Bwana wetu, Bwana wetu na Mwokozi wetu ...”. Inafuatia kujikabidhi kwa Maria na Yosefu. Baadaye  maneno halisi ya kujiuzuli kwa maelezo. “Tunathibitisha: katika kesi ya hali ya udhaifu, unaodhaniwa kuwa hauwezi kuponywa, au wa muda mrefu, na ambao unatuzuia kufanya kazi za kutosha za huduma yetu ya kitume; au ikitokea kwamba kizuizi kingine kikubwa na cha muda mrefu kwa hili ni kikwazo vile vile, kujiuzulu ofisi yetu takatifu na ya kisheria, kama Askofu wa Roma na kama Mkuu wa Kanisa Takatifu Katoliki, mikononi mwa Kadinali Dekano... kumwachia yeye, kwa pamoja angalau na Makardinali wanaosimamia Curia Romana na Makamu  wetu  Kardinali kwa mji wa Roma ... kitivo cha kukubali na kutekeleza kujiuzulu kwetu, ambacho ni faida kubwa zaidi ya Kanisa Takatifu anapendekeza kwetu”.  Chini, saini na tarehe iliyoandikwa kwa mkono, katika Kanisa la Mtakatifu Petro, Dominika  ya Mchungaji Mwema, ikiwa ni dominika ya II ya Pasaka, 2 Mei 1965, ya Upapa wetu”.

Inashangaza kutambua kwamba Paulo VI hairejei ugonjwa tu, bali pia uwezekano wa “kizuizi kingine kikubwa na cha muda mrefu”. Msisitizo ambao, watu mbalimbali kutoka katika kundi la karibu zaidi la Montini wamependekeza, unaweza kuhusishwa na kile, kulingana na baadhi ya mashuhuda  wenye mamlaka, Pius XII alikuwa ameweka wakati huo: kujiuzulu kwake katika tukio la kutekwa nyara na Hitler katika awamu ya kilele cha kuhitimishwa kwa Vita ya II ya Dunia. Hili lingewaruhusu makadinali kukutana, labda katika nchi isiyo na upande wowote na salama, kumchagua Askofu mpya wa Roma, kuchukua mahali pa yule aliyekuwa mfungwa wa udikteta wa kinazi. Hatimaye, ni vyema kutambua kwamba katika kesi ya Papa Paulo VI na ile ya Papa Fransisko, tunazungumzia barua ya kuzuia, yaani, inayohusishwa na ukweli kwamba Papa amezuiwa kuwa na uwezekano wa kujinyima kwa uhuru na kujuzulu kwa dhamiri kamili. Kwa hivyo hizi ni barua ambazo hazina uhusiano wowote na kujiuzulu kwa  Papa Mstaafu Benedikto XVI, kulikofanyika karibu miaka kumi iliyopita.

18 December 2022, 16:36