2022.12.14  CCEE: Uwakilishi wa  awamu ya pili Sinodi kwa Bara la Ulaya 2022.12.14 CCEE: Uwakilishi wa awamu ya pili Sinodi kwa Bara la Ulaya  

Awamu ya bara la Ulaya ya kisinodi itafanyika Prague mnamo Februari 2023

Tarehe 14 Desemba limewakilishwa tukio ambalo wajumbe 200 kutoka mabaraza 39 ya kitaifa ya maaskofu na hali halisi muhimu zaidi ya kikanisa watashiriki awamu ya II ya Sinodi kwa Bara la Ulaya,huku nyuma yake kuna vita Ulaya ya Mashariki.Askofu Grušas,rais wa Ccee:‘kile kinachotokea Ukraine pia kinathiri maisha ya kikanisa’.Kardinali Hollerich:'Sinodi ya maamuzi kwa ajili ya Kanisa la kimisionari’.

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

Ushirika, ushiriki na utume, ndiyo maneno makuu matatu yatakayo endelea kuongoza awamu ya bara la Kisinodi kuhusu Ulaya, itakayofanyika huko Prague kuanzia tarehe 5 hadi 12 Februari 2023. Tukio hilo lililowasilishwa asubuhi tarehe 14 Desemba 2022 kwenye makao makuu ya Radio Vatican - Vatican News, na ambalo limeandaliwa na Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Ulaya (CCEE), Baraza la Maaskofu wa Cheki na Jimbo kuu la Prague, kwa kuongozwa na maongozo ya hatua ya kibara, iliyochapishwa hivi karibuni na ambayo inaleta pamoja tafakari za watu wa Mungu kuhusu mada za sinodi katika ngazi ya kitaifa na kijimbo

Washiriki katika hatua ya bara la Ulaya

Katika mji mkuu wa Jamhuri ya Cheki kutakuwa na wajumbe 200 watakaohudhuria, yaani marais 39 wa mabaraza ya maaskofu wa kitaifa, kila mmoja akiandamana na wawakilishi watatu, na wawakilishi 44 wa hali halisi ya kikanisa zinazowakilisha zaidi katika ngazi ya Ulaya, walioalikwa moja kwa moja na CCEE.  Kwa hawa wataongezwa washiriki 390 wa mbali, kumi kwa kila baraza la maaskofu. Zaidi ya hayo, baadhi ya wajumbe kutoka katika madhehebu mengine ya Kikristo pia watashiriki katika kazi hiyo. Mkutano huo utagawanywa katika awamu mbili: ya kwanza kuanzia tarehe 5 hadi 9 Februari  2023 ambayo itahusisha wajumbe wote, na  hatua ya pili, kuanzia tarehe  9 hadi 12 Februari 2023 itahusishwa marais tu wa mabaraza ya maaskofu.

Kutembea pamoja

Askofu Gintaras Grušas, askofu mkuu wa Vilnius na rais wa CCEE, ambaye pia alikumbusha Sinodi mbili za Ulaya zilifanywa na Mtakatifu Yohane Paulo II baada ya vita baridi na mwanzoni mwa milenia mpya alisema: “Tunataka kutembea pamoja, kama Baba Mtakatifu Francisko alivyotuhimiza, kupata uzoefu wa Kanisa linalopokea na kuishi karama ya umoja na inayojifungua yenyewe kwa sauti ya Roho kuwa kweli Kanisa la Sinodi, Kanisa la kusikiliza, Kanisa la ukaribu.”  

Wazo juu ya vita vya Ukraine

Hatua ya bara la Ulaya ya mchakato wa Sinodi itafanyika chini ya mwaka mmoja tu mara baada ya kuanza kwa uvamizi wa Urussi nchini Ukraine. “Sote tunahisi uzito wa vita, ambayo pia inagusa maisha yetu ya kikanisa kwa umakini mwingi wa hisani na sala kusaidia watu wa Ukraine, kusimamisha vita na kuleta amani”,  alisisitiza Askofu Grušas kwa Vatican News, ambaye ni mzaliwa wa Lithuania ambaye ameona uhamisho wa wakimbizi. “Kama askofu mkuu wa Vilnius ninafurahishwa na mwitikio wa watu wa Kanisa kwa hitaji la Ukraine”, alisema kwa kuongezea kuwa “tumefanya makusanyo mbalimbali. Tumechukua wakimbizi wengi sana na  kuwasaidia. Mioyo ya watu imefunguliwa ili kuwafikia watu wa Kiukrene jirani kwa maombi na usaidizi wa hisani na hii pia inaonesha sisi ni akina nani kama Kanisa”.

Kwa Kanisa la wamisionari

Kardinali Jean-Claude Hollerich, Askofu mkuu wa Luxembourg na makamu  rais wa CCEE alisema:  “Sinodi italisaidia Kanisa kuwa wamisionari wa kweli. Tuna mdororo wa Ukristo barani Ulaya na Sinodi hii isitunyime kuwa wamisionari wapya. Dhamira ya Kanisa ni kumtangaza Kristo, kutangaza ahadi yetu kwa uumbaji, lakini pia kwa haki na amani, dhamana ya watu wote wa Mungu”, alisema Kardinali, na akisisitiza tena kwamba: “Kanisa la Sinodi kwanza ni Kanisa zima la kimisionari”.

hatua ya II ya kisinodi barani Ulaya
16 December 2022, 09:57