Askofu Msaidizi António Manuel Bogaio Constantino, wa Jimbo kuu la  Beira, Msumbiji. Askofu Msaidizi António Manuel Bogaio Constantino, wa Jimbo kuu la Beira, Msumbiji. 

Askofu Msaidizi António Manuel Bogaio Constantino Jimbo Beira,

Askofu msaidizi mteule António Manuel Bogaio Constantino, M.C.C.J., alizaliwa tarehe 9 Novemba 1969, Msumbiji. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kitawa na Kikasisi, tarehe 10 Juni 2000 akaweka Nadhiri zake za daima, huku akiendelea na masomo yake Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian, kilichoko mjini Roma. Tarehe 13 Juni 2001 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre! Beira!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa sana Padre António Manuel Bogaio Constantino, M.C.C.J., wa Shirika la Wamisionari wa Comboni wa Moyo Mtakatifu wa Yesu kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Beira nchini Msumbiji. Hadi kuteuliwa kwake, alikuwa ni Mkuu wa Kanda wa Shirika la Wamisionari wa Comboni wa Moyo Mtakatifu wa Yesu na Rais wa Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume, Baraza la Maaskofu Katoliki Msumbiji. Itakumbukwa kwamba Askofu msaidizi mteule António Manuel Bogaio Constantino, M.C.C.J., alizaliwa tarehe 9 Novemba 1969, Jimbo Katoliki la Tete, Msumbiji. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kitawa na Kikasisi, tarehe 10 Juni 2000 akaweka Nadhiri zake za daima, huku akiendelea na masomo yake Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian, kilichoko mjini Roma. Tarehe 13 Juni 2001 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre, Jimbo kuu la Beira.

Hija ya Kitume ya Papa Francisko nchini Msumbiji.
Hija ya Kitume ya Papa Francisko nchini Msumbiji.

Tangu wakati huo, alibahatika kuendelea na masomo na hatimaye kujipatia Shahada ya Uzamivu katika Tasnia ya Mawasiliano ya Jamii, fani ya uandishi wa habari, huko Madrid, Hispania kati ya mwaka 2001-2007. Ameshirikisha karama na mapaji yake kwenye Majarida mbalimbali ya Shirika. Amewahi kuteuliwa kuwa Paroko katika Parokia mbalimbali nchini Msumbiji zinazoongozwa na kusimamiwa na Shirika la Wamisionari wa Comboni wa Moyo Mtakatifu wa Yesu. Kuanzia mwaka 2016 akachaguliwa kuwa Mkuu wa Shirika la Wamisionari wa Comboni wa Moyo Mtakatifu wa Yesu, Kanda ya Msumbiji, Jimbo kuu la Maputo, Rais wa Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume tangu mwaka 2018-2019. Kuanzia mwaka 2019 hadi kuteuliwa kwake alikuwa ni Rais wa Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume, Baraza la Maaskofu Katoliki Msumbiji.

Uteuzi Msumbiji

 

14 December 2022, 16:38