Tafuta

2022.11.19-20 Ziara ya Papa huko Asti 2022.11.19-20 Ziara ya Papa huko Asti  

Ziara ya kichungaji ya Papa huko Asti:Shukrani za Askofu Pastraro

Askofu Marco Pastraro wa Asti amemshukuru Papa kwa moyo wote kwa uwepo wake kati yao na katika muda aliojikita nao.Shukrani kwa kuwaimarisha imani yao na upendo kwa namna ya pekee alio uonesha kwao.”Tunapenda kufikiria kuwa Asti ni mwanzo wa ulimwengu kwa sababu leo hii tunapyashwa jitihada zetu za kimisionari kupeleka furaha ya Injili hadi miisho ya dunia,kwa kila pembe ya maisha ambayo tutakutana nayo.”

Na Angella Rwezaula, – Vatican.

Mara baada ya maadhimisho ya Ekaristi Takatifu katika  Dominika ya Siku Kuu ya Kristo Mfalme, tarehe 20 Novemba 2022, katika Kanisa Kuu la Asti nchini Italia, Askofu Marco Pastraro wa Jimbo hilo amemshukuru Baba Mtakatifu Francisko kwa maadhimisho na ujio wake.  Akianza Amesema anamshukuru kwa niaba ya jumuiya nzima ya Asti kwa mkutano huo ambao waliutamani sana. Alipochaguliwa amesema kama Papa, alitamka kwamba alichukuliwa karibu kutoka mwishoni mwa dunia. Kwa njia hiyo siku hiyo  Askofu Pastraro amesema wao wamefurahi  na wataka kufikiria  Asti ambayo  ni ardhi yenye mizizi ya familia yake kama kwamba inaweza kuwa mwanzo wa ulimwengu.

Ziara ya kichungaji ya Papa Francisko huko Asti
Ziara ya kichungaji ya Papa Francisko huko Asti

Na ni kweli kwa sababu amethibitishwa siku hiyo wao wamepyaisha mizizi ya imani yao, kuanzia na ekaristi, Neno la Mungu, huduma ya kharifa wa mtume Petro, Udugu ambao unawafanya kuwa jumuiya, uwepo wa maskini ambao ni mwili wa Kristo, yote hayo yamezungumza uwepo wa Yesu kati yao; na wa Yesu ambaye daima anazaliwa na anazaliwa tena kwa furaha.

Ziara ya kichungaji ya Papa Francisko huko Asti
Ziara ya kichungaji ya Papa Francisko huko Asti

Askofu akiendelea amesema kiukweli ni “hapa, mwanzo wa ulimwengu, leo hii tunapyashwa jitihada zetu za kimisionari kupeleka furaha ya Injili hadi miisho ya dunia, kwa kila pembe ya maisha ambayo tutakutana nayo”. Kwa maana hiyo amerudia kushukuru kwa moyo wote kwa uwepo wake kati yao na katika muda aliojikita kuwa nao; Shukrani kwa kuwaimarisha imani yao na upendo kwa namna ya pekee alio uonesha kwa ajili yao. Amemshukuru kwa ziara yake na kumwomba arudi tena akipenda kwa sababu pale ni mji wake na wakati huo huo amemwakikishia kuendelea kusali kwa ajili yake.  Baada ya shukrani hiyo,  Papa Francisko amemzawadia kikombe (calice)cha kuandhimisha misa.

Askofu wa Asti amshukuru Papa
20 November 2022, 12:29