Tafuta

Kwa mwaka, huu basi, Huduma ya  Tiba Shufaa [Palliative Cure[ pia  imeingia kikamilifu katika  mtaala wa mafundisho ya chuo kikuu cha Kitivo cha Tiba na Upasuaji. Kwa mwaka, huu basi, Huduma ya Tiba Shufaa [Palliative Cure[ pia imeingia kikamilifu katika mtaala wa mafundisho ya chuo kikuu cha Kitivo cha Tiba na Upasuaji. 

Siku ya Kitaifa ya Tiba shufaa sambamba na Kumbu kumbu ya Mtakatifu Martino wa Tours

Katika siku ambayo Mama Kanisa anamkumbuka Mtakatifu Martino wa Tour ni siku inayokwenda sambamba na Siku ya Huduma ya Tiba Shufaa kitaifa.Italia imetambua umuhimu wa Huduma ya Tiba Shufaa na leo hii kuna sheria ya 38/2010 ambayo inahusu Huduma hiyo na tiba ya maumivu. Kwa mwaka,huu pia huduma hiyo imeingia kikamilifu katika mtaala wa mafundisho ya chuo kikuu cha Kitivo cha Tiba na Upasuaji.

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Huduma ya Tiba shufaa inajikita katika umuhimu wa utamaduni ambayo unasaidia kusindikiza na kuchukua wajibu katika mateso ya mtu mgonjwa, kwa kuhusisha mpango tiba na usindikizwaji  kiroho. Amethibitisha hayo Askofu Mkuu Vincenzo Paglia, Rais wa Taasisi ya Elimu kwa ajili ya Maisha katika fursa ya   Liturujia siku katika kumbumkuka Mtakatifu Martino wa Tours ambayo  uadhimisha kila ifikapo tarehe 11 Novemba,  sambamba na Siku ya Kitaifa ya Huduma ya Tiba Shufaa nchini Italia. Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Paglia amesema Italia imetambua umuhimu wa Huduma ya Tiba Shufaa na leo hii kuna  sheria ya  38/2010  ambayo inahusu Huduma ya Tiba Shufaa na tiba ya maumivu.  Kwa mwaka,  huu basi, Huduma ya  Tiba Shufaa  [Palliative Cure[ pia  imeingia kikamilifu katika  mtaala wa mafundisho ya chuo kikuu cha Kitivo cha Tiba na Upasuaji. Kwa upande wake, Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya Maisha ina mpango mmoja maalumu unaojikita kueneza na kuhamasisha Huduma ya Tiba shufaa ulimwenguni.

Hati kuhusu matatizo ya mwisho wa maisha na hudumua ya tiba shufaa

Kwa kuanzishwa mnamo 2017 wameandika kitabu kiitwacho cheupe kwa lugha ya kiingereza na kikundi cha Kimataifa cha wataaalam na kutafsiriwa kwa lugha ya Kiingereza, Kifaransa na kijerumani, na muda si mrefu kitakuwa katika  lugha ya kispanyola na kireno na kufanya makongamano tofauti ya kimataifa. Mnamo tarehe 28 Oktoba 2019 katika mchakato wa mkatano huko Casina Pio IV, jijini Vatican, walitia saini Hati moja ya pamoja kuhusu matatizo ya mwisho wa maisha na kueneza juu ya Huduma ya Tiba Shufaa kwa upande wa Dini Tatu kuu za Ibrahimu ambazo ni [Kiyahudi, Kikristo na Kiislamu]. Kwa maana hiyo Huduma ya Tiba shufaa kwa mujibu wa Askofu Mkuu Paglia amesema inawakilisha nafasi moja ya matendo ya kulinda na kutetea maisha ya binadamu, huku ikipinga ukaidi usio na maana kama vile (kuendelea kwa matibabukwa nguvu zote ) na euthanasia. Huduma ya tiba shufaa inaturuhusu kushinda upweke wa mgonjwa na ukimya wa jamii yetu kuelekea hatua za mwisho za kuwepo duniani. Kifo cha mwanadamu, kwa ajili yetu sisi waamini, ni nafasi kubwa ya uwazi kuelekea utimilifu huo wa maisha unaotungoja kwa msingi wa ahadi ya Yesu ”. Alisisitiza Askofu Mkuu Paglia.

Mosi Desemba mkutano kuhusu Huduma ya Tiba shufaa kwa watoto kabla ya kuzaliwa 

Naye Askofu Renzo Pegoraro, Kansela wa Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya maisha amesema mpango utakaofuata ni wa Mkutano wa mpango wa tarehe Mosi Desemba  itajaojikita na mada  “Perinatal Palliative Care, Foundation&Experiences”yaani  Huduma ya Tiba shufaa kwa watoto kabla ya kuzaliwa, Msingi na uzoefu. Miongoni mwa watakaoshiriki Mkutano huo mchana watakuwa ni wataalamu muhimu wa kimataifa ili kuchukua tathmini ya suala la mipaka, kutoa Huduma ya  Tiba Shufaa na usindikizaji mzuri wakati wa kuzaliwa, katika muktadha wa magonjwa makubwa sana ambayo mara nyingi hayaendani na maisha. Kwa njia hiyo, wanatoa msaada  na wenye thamani kwa wazazi kukubali hali hiyo ya ulemavu mkubwa wa mtoto ambaye hajazaliwa na kutoa usaidizi mzuri, kuepuka aina za tiba ya kuendelea au kuanguka katika hali ya euthanasia au kifo laini.

Huduma ya Tiba shufaa ina tahamani kubwa isiyoonekana kwa macho

Yote haya yanaenea kwa mtazamo mpana wa Huduma ya Tiba shufaa kwa Watoto, ikiweka umakini maalum kwa mateso ya watoto na usaidizi wa kisaikolojia na kiroho kwa wazazi wanaohusika katika uzoefu kama huo mgumu, alihitimisha  Askofu Pegoraro. Mnamo mwaka 2015, katika hotuba yake kwa Baraza Kuu la Chuo cha Kipapa cha Maisha, Baba Mtakatifu Francisko alikuwa amesema: “Ninawahimiza wataalamu na wanafunzi kujishughulisha na aina hii ya misaada ambayo kiukweli ina thamani kubwa hata kama inafikiriwa ni sio kutokana na ukweli kwamba ‘haiokoi maisha’. Utunzaji wa utulivu hutimiza jambo muhimu sawa: humthamini mtu. (…). Ni uwezo huu wa huduma kwa maisha na hadhi ya mgonjwa, hata akiwa mzee, ndio hupima maendeleo ya kweli ya dawa na jamii kwa ujumla. Mnamo mwaka wa 2018, katika Ujumbe wa Katibu wa Jimbo la Kongamano kuuu Huduma ya tiba Shufaa  Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican alikuwa amebainisha kuwa "Wakati rasilimali zote za 'kufanya' zinaonekana kumalizika, basi ndipo kipengele muhimu zaidi katika uhusiano wa kibinadamu kinaibuka ambacho  ni kile cha kuwa, kuwepo, kuwa karibu na kukaribisha.

Siku ya Kitaifa Italia ya Huduma Shufaa
11 November 2022, 16:26