Papa Francisko akutana na Shevchuk mjini Vatican-ukaribu wa sala kwa Ukraine
Na Angella Rwezaula, – vatican.
Katika nchi ya Ukraine ambapo kuliibuka vita tangu tarehe 24 Februari hadi leo hii na kugeuza kwa namna moja au nyingine kipande cha Ulaya kuwa na mabadiliko katika kambi ya mapambano, Baba Mtakatifu Francisko hachoki kamwe kusisitiza juu kuwaombea watu wa Ukraine ambao wanazidi kuteseka. Na hatua hiyo ya wito wake wa kuomba imejithihirisha kila mara katika kila wakati wakati wa sala ya Malaika wa Bwana kwa kila Dominika, wakati wa kumaliza Katekesi yake ya kila Jumatano na wakati mwingine inapowezekana kwenye mikutano na hata katika ziara ya kitume.
Kwa maana hiyo, Jumatatu tarehe 7 Novemba 2022, mwakilishi wa Kanisa la nchi hiyo, ya Ukraine Askofu Mkuu wa Kanisa la Kigiriki -katoliki Sviatoslav Shevchuk, amevuka mipaka ili kuleta kwa mara ya kwanza jijini Roma tangu mwanzo wa vita, hisia za Watu wa Ukriane moja kwa moja mbele ya Baba Mtakatifu. Mkutano huo umefanyika katika maktaba ya faragha ya kutume katika Jumba la Kitume Vatican ambapo baadaye kwa mujibu wa taarifa shuhuda zilitolewa kuhusu hali halisi ya huko ambayo inatolewa karibu miezi minake kila siku kupitia kwa Askofu Mkuu wa Kiev-Halic.
Shukrani kwa Papa kwa yote atendayo kwa watu wa Ukraine
Kiongozi huyo mara baada ya mkutano huo na Papa alithibitisha kumshukuru Papa kwa yote ambayo amekuwa akitenda katika kusimamisha vita na kuwambea na kutuma wawakilishi wake kwa ajili ya kutafuta amani na zaidi kuwaondoa watu mateka na wafungwa, ikiwa ni pamoja na kuwahakikishwa kwamba Yeye haachi kamwe kuwa karibu na watu wa Ukraine katika sala na matendo ya dhati.
Zawadi ya kipende cha mlipuko hatari
Katika kubadilishana zawadi kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa ni kwamba kwa upande wake, Askofu Shevchuk alimletea Papa Francisko kipande kimojawapo kati ya vipande vya mlipuko wa hatari kutoka Urussi ambacho mnamo mwezi Machi mwaka huu kiliharibu uso wa jengo la Kanisa la Kigiriki-Katoliki la Ukraine katika jiji la Irpin. Kipande hicho kilicho sababaisha hatari kwa mujibu wa maandishi yanasomeka, kwamba kilitolewa kutoka katika miili ya askari wa Kiukreni, raia na watoto, ambayo ni ishara inayoonekana ya uharibifu na kifo na ambacho vita vinasababisha kila siku.