Papa ameteua Wanawake wengine wawili kushika ngazi kuu za Vatican
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Papa Francisko Ijumaa tarehe 25 Novemba 2022 amefanya teuzi mbali mbali ambazo zimeona mabadiliko na mapya ambayo Papa anapendelea kufanya katika Kanisa, hasa kwa kuwateua wanawake wengine wawili katika ngazi kuu ya Vatican. Awali ya yote Baba Mtakatifu Francisko amemteua Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Utaduni na Elimu, Profesa Antonella Sciarrone Alibrandi, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Msaidizi wa Mkuu wa Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu (Italia). Prof. Sciarrone Alibrandi alizaliwa Milano mnamo tarehe 2 Mei 1965. Profesa Kamili wa Sheria ya Kiuchumi katika Kitivo cha Benki, Sayansi ya Fedha na Bima ya Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu huko Milano na Rais wa Chama cha Walimu wa Sheria wa Uchumi. Yeye pia ni mwanachama wa mashirika mengi kama vile Jumuiya ya Ulaya ya Sheria za Benki na Fedha, Bodi ya Mafunzo ya Taasisi ya Benki ya Ulaya na Kundi la Wataalamu wa Vikwazo vya Udhibiti wa Ubunifu wa Kifedha. Baba Mtakatifu aidha amemteua Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kipapa ya Mtakatifu Tomas wa Akwino Profesa Luca Tuninetti, ambaye alikuwa mkuu wa Kitivo cha Falsafa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana Roma Italia.
Katika teuzi hizo pia amepyaisha miongoni mwa Wajumbe wa Tume ya Kipapa ya Akiolojia au Sanaa Takatifu na wakati huo huo akamteua Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo ya Kipapa, Daktari Raffaella Giuliani, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa Afisa wa Taasisi hiyo. Baba Mtakatifu aidha amemtaua Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Vatican kwa Tathmini na Ukuzaji wa Ubora wa Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu vya Kikanisa. (AVEPRO) Padre Roberth Alexander Hernández Gómez, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Afisa wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu.
Uteuzi wa Washauri wa Baraza la Kipapa la Makleri
Katika uteuzi huo pia amewatueua washauri wa Baraza la Kiapa la Waklri Askofu Alejandro Arellano Cedillo; Monsinyo Branislav Koppal; Waheshimiwa Padre Riccardo Battocchio; Padre Hubertus Blaumeiser; Padre Anthony R. Brausch; Padre Francisco Javier Insa Gómez; Padre Emilio Lavaniegos González; Padre Raffaele Ponticelli; Padre Stefan Ulz; Dario Vitali; Waheshimiwa Mapadre wa mashirika: Fabio Ciardi, O.M.I.; Fernando Domingues, M.C.C.J.; Hugh Lagan, S.M.A.; Mhehimiwa Sr. Lidia Ramona González Rodríguez, F.M.H.; Madaktari: Berardino Guarino na Chiara D’Urbano; na Profesa Rosalba Erminia Paola Manes.